Waziri Mkuu Amwagiza CAG Kukagua Bandari na Benki ya CRDB......Makampuni 150 ya Uwakala Yafunguli
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali aende Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ili akague taarifa za mapato ambazo zilikuwa zikilipwa na mawakala wa forodha na bandari kupitia benki ya CRDB lakini hazionekani kwenye mifumo ya benki. Ametoa agizo hilo leo jioni (Jumatatu, Machi 17, 2016) wakati akizungumza na mamia ya mawakala wa forodha na bandari waliohudhuria mkutano aliouitisha ili kusikiliza kero zinazowapata katika utendaji kazi wao. Akizungumza na mawakala hao kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu alisema kuna dalili za kutupiana lawama baina TPA na CRDB kuhusu malipo yaliyikuwa yakifanyika benki halafu fedha hazionekana na wakala anaidaiwa kuwa hajalipia mzigo wakati alishaulipia. “Kimsingi bado liko tatizo baina ya Mamlaka ya Bandari pamoja na Benki ya CRDB. Naona kila mmoja hapa anamkana mwenzake. Nitamtuma CAG ili akafanye ukaguzi wa kina ili tujue ni nani kati yao amehusika na upotevu wa f...