Posts

Showing posts from August 27, 2013

MAANDALIZI MKUTANO WA UCHAGUZI TFF

Image
Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inaendelea na maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Uchaguzi utakaofanyika Oktoba 26 na 27 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Awali mkutano wa uchaguzi ulikuwa ufanyike Februari 23 na 24 mwaka huu lakini tukauahirisha kusubiri maelekezo ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), hivyo tayari wajumbe wana taarifa rasmi kuhusu mkutano huo. hdg Orodha ya wajumbe iliyotumwa awali kwa ajili ya Mkutano tunayo, isipokuwa kama kuna wanachama wetu wana mabadiliko ya majina ya wajumbe watakaohudhuria wanatakiwa kutuma majina hayo kabla ya Septemba 30 mwaka huu. Wanachama wa TFF ni vyama vya mpira wa miguu vya mikoa, vyama shiriki na klabu 14 za Ligi Kuu ya Vodacom. WAWILI WAPINGWA UCHAGUZI WA TFF Wanamichezo wawili walioomba kuwania uongozi kwenye uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) utakaofanyika Oktoba 27 mwaka huu wamewekewa pingamizi. Waliopingwa n...

BAR/MGAHAWA WA SAMAKI SAMAKI WATEKETEA KWA MOTO

Image
Picha zikionesha Bar ya samaki samaki ilivyo

BONDIA WA DUNIA FRANCOIS BOTHA ATUA JIJINI DAR

Image
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bi.Juliana Yassoda akiwa na Bondia wa Dunia wa uzito wa juu Francois Botha alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuzungumzia masuala ya mchezo wa ndondi utakaofanyika 30 Agosti mwaka huu katika ukumbi wa Diamond. Bondia wa Dunia wa uzito wa juu Francois Botha akionyesha jinsi ya kupambana kulia ni Yasini Abdalla Rais wa Shirikisho la ndondi nchini ,kushoto ni mdau wa ndondi , uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo jijini Dar es salaam.

HII NDIO FIESTA ILIVYOJIRI KATIKA VIWANJA VYA USHIRIKA MOSHI

Image
Wasanii machachari Bongo Move Wema Sepetu (kushoto) na Aunt Ezekiel wakicheza muziki wa bongo Fleva uliokuwa ukishushwa na Msanii wa Bongofleva,Ferooz katika uzinduzi wa Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 Bhaaaaass! katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika Mjini Moshi usiku huu. Tamasha hilo limebamba ile mbaya.  Ferooz akiwa na mmoja wa mashabiki wake wakilishambulia jukwaa vilivyo. Sehemu ya wakazi wa mji wa Moshi wakiendelea kushuhudia makamuzi ya wasanii mbalimbali wanaotumbuiza usiku huu kwenye uzinduzi wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012. Prezoo akiwarusha mashabiki kibao (hawapo pichani) waliojitokeza jioni ya leo kwenye uzinduzi wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012 Pichani juu na chini ni mwanamuziki kutoka nchini Kenya na mmoja wa shiriki wa shindano la Big Brother Stargame,CMB Prezoo akitumbuiza jukwaani usiku huu kwenye uzinduzi wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012 ndani ya uwanja wa chuo cha ushirika mjini Moshi. Mm...

Wanafunzi wote wafeli mtihani wa sekondari

Image
fendall_campus Kwa mara ya kwanza katika historia ya Liberia, wanafunzi wote wamefeli mtihani wao wa mwisho wa sekondari na hivyo kumaanisha kuwa hakuna hata mmoja ambaye atafuzu kuingia chuo kikuu. Waziri wa elimu wa Liberia amesema ameshinda kufahamu ni kwa nini hakuna wanafunzi hao wamefeli kiasi hicho. Zaidi ya wanafunzi elfu ishirini na watano walianguka mtihani huo ambao ungewapa fursa ya kujiunga na chuo kikuu cha Liberia ambacho ni moja ya vyuo vikuu vinavyoendesha na serikali. Lakini wasimamizi wa chuo hicho wameiambia BBC kuwa wanafunzi hao hawakuwa makini na ufahamu mzuri wa lugha ya Kiingereza ambayo ilitumiwa kuwatahini. Taifa la Liberia linaendelea kujinasua kutokana na athari za mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyomalizika zaidi ya miaka kumi iliyopita. Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf, ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, amekiri kuwa mfumo wa elimu nchini humo bado ungali duni na unahitaji marekebisho ya dharura. Mwandishi ...

ETI YUPI MKALI KATI YA Hawa Wasanii 17 wa Kike wa Bongo Movie

Image
Kiwanda cha filamu Tanzania kimezalisha waigizaji wengi wenye majina makubwa sasa. Miongoni mwao, ni wasichana hawa ambao tungependa wewe utuambie ni yupi mwenye mvuto zaidi. Irene Uwoya Filamu alizocheza Question Mark, Apple,Safari,Zawadi Yangu, Innocent Case, Nyota Yangu, Last Card, Doa la Ndoa, Ngumi ya Maria, Chupa Nyeusi, Kiapo, Eagle Eyes, Diversion of Love, Fair Decision, Pretty Girl, Damu Moja, Shakira, Yolanda, Tanzanite Elizabeth Lulu Michael Filamu alizocheza Oxygen, Elizabeth Michael,House Boy, Ripple of Tears, Confusion,Ritazo, Family Disaster, Woman with Principal, Foolish Age nk Wema Sepetu Filamu alizocheza House Boy, Crazy Tenant, Basilisa, The Diary, Lerato, Tafrani, White Maria, Sakata, Family Tears Skyner Ally Filamu alizocheza What is It, Why I Did Love, I Hate My Birthday’, Kizungumkuti’, Unpredictable, Shahaada Yobnesh Yussuph aka Batulli Filamu alizocheza Kazi Yan...