Posts

Showing posts from September 27, 2016

Majina Ya Wanafunzi Waliochaguliwa Vyuo Vikuu Mbalimbali 2016/2017

Image
Chuo  Kikuu Cha Mwalimu Nyerere   <<bonyeza Hapa>>   Chuo  Kikuu Cha  Udsm,duce Na Muce   <<bonyeza Hapa>> Chuo  Kikuu Cha  Tumaini Makumira    <<Bonyeza Hapa>>      Chuo  Kikuu Cha Udom  <<bonyeza Hapa>>   Chuo  Kikuu Cha Ifm <<Bonyeza Hapa>>   Chuo Kikuu Marian << Bonyeza Hapa>>    Chuo Kikuu Cbe        << Bonyeza Hapa>>   Tumaini-mbeya     << Bonyeza Hapa>> & <<hapa>>    Chuo Kikuu Mum         << Bonyeza Hapa>>   Chuo Mum(Diploma) <<Bonyeza Hapa>>    Chuo- Stella Maris   << Bonyeza Hapa>>    Chuo- Kampala-kiu  << Bonyeza Hapa>>

Polisi Wakamata Silaha, Jambazi Hatari Dar

Image
Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam CP, Simon Sirro akizungumza na wanahabari (hawapo pichani). …Akisikiliza maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wanahabari. Kamanda Simon Sirro akionyesha baadhi ya silaha zilizokamatwa. Kamanda Sirro akionyesha gari lililokamatwa na magunia ya bangi . Taswira ya mbele ya gari hilo lililokamatwa na magunia ya bangi. Wanahabari wakichukua tukio hilo. JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI JESHI LA POLISI TANZANIA TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI  27.09.2016   KUPATIKANA KWA SMG 01, MARK IV 01, BASTOLA 01 NA RISASI 12  KUKAMATWA KWA JAMBAZI  HATARI ANAYESHIRIKIANA NA MKEWE KATIKA MATUKIO YA UJAMBAZI WAKUTUMIA SILAHA Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar Es salaam kupitia Kikosi Maalum cha Kupambana na Ujambazi wa kutumia silaha kimefanikiwa kumkamata jambazi hatari anayehusika kwa makosa ya ujambazi wa kutumia silaha katika maeneo mbalimbali Jijini Dar Es Salaam. Mnamo tarehe 23/09/2016 saa nane

Tetemeko Mkoani kagera,Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba na Katibu wa Mkoa Watumbuliwa

Image
Rais John Magufuli. Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Amantius Msole na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba Steven Makonda baada ya kubaini kuwa wamefungua akaunti nyingine ya benki kwa kutumia jina linalofanana na akaunti rasmi ya kuchangia maafa iitwayo “Kamati Maafa Kagera” kwa lengo la kujipatia fedha. Pia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa Mkoa wa Kagera Simbaufoo Swai kutokana na kuhusika katika njama hizo. Taarifa hiyo  iliyotolewa na Waziri Mkuu, Majaliwa muda mfupi baada ya kupokea hundi ya msaada kutoka kwa Waziri Mkuu wa India imeeleza kuwa pamoja na kutengua uteuzi huo Rais Magufuli ameagiza vyombo vya dola vichukue hatua dhidi ya wote waliohusika katika njama za kufungua akaunti hiyo. Kadhalika Rais Magufuli leo amepokea msaada wa Shilingi Milioni 545milioni kutoka kwa Waziri Mkuu wa India Narendra Modi kwa ajili ya kusaidia wananchi wa Mkoa wa Kagera waliopatwa na maa

Mdahalo Wagombea Urais Marekani Watawaliwa Na Kejeli Na Vijembe

Image
Donald Trump na Hillary Clinton kabla ya kuanza kwa mdahalo huo. NEW YORK , MAREKANI: Homa kubwa nchini Marekani kwasasa ni uchaguzi mkuu wa rais wa nchi hiyo unaotarajia kufanyika Novemba 4, 2016. Homa hiyo inachangiwa kwa kiasi kikubwa na wagombea wa pande zote mbili, mwanamama Hillary Clinton wa Chama Cha Democratic na Donald Trump wa Chama Cha Republican ambao kura za maoni zinaonesha wanakabana koo kuwania nafasi hiyo muhimu. Usiku wa kuamkia leo wagombea hao wamepambana vikali katika mdahalo wa kwanza wa televisheni ambapo wamepingana katika masuala mbali mbali ikiwemo masuala ya sera, kodi, ajira na uchumi. ….Wagombea hao wakiwa kwenye mdahalo huo. Vilevile wote wamezungumzia kuhusu Vita vya Iraq na juhudi za kukabiliana na kundi linalojiita Islamic State ambalo inadaiwa chimbuko lake kubwa ni kutokana na vita hivyo. Msimamizi wa mdahalo huo, Lester Holt alimwuliza Donald Trump mbona hadi kufikia sasa bado hajaweka wazi taarifa zake za ulipaji kodi. Mwanamama H

Papa Francis Akutana Na Rais Kabila Vatican

Image
Papa Francis akizungumza na Rais Kabila ndani ya maktaba yake. Papa Francis akiagana na Rais Kabila baada ya mazungumzo kumalizika. VATICAN CITY : Papa Francis amekutana na kufanya mazungumzo ya faragha na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mazungumzo hayo yalifanyika kwenye makazi ya Papa Francis yaliyoko jijini Vatican. Kwenye mazungumzo hayo Rais Kabila amesema atahakikisha anafanikisha mazungumzo ya pande zote zinazokinzana nchini Congo yamalizike kwa amani. Kwenye mazungumzo hayo yaliyochukua dakika 20, Papa Francis hakwenda kusalimiana na mgeni wake huyo kwenye chumba maalum cha wageni maalum na kumsubiri kwenye maktaba yake. Vatican wamesema Papa Francis amesisitiza ni lazima mazungumzo ya amani yafanyike baina ya serikali na wapinzani ili kuliepusha taifa hilo kuingia kwenye machafuko. Na Leonard Msigwa/GPL.

Wabunge EU Wamuunga Mkono Magufuli

Image
Rais John Magufuli wa Tanzania. WAKATI Rais John Magufuli wa Tanzania akishikilia msimamo kuwa nchi yake haitasaini Mkataba wa Ushirikiano wa Kiuchumi (EPA) na Umoja wa Ulaya (EU) mpaka dosari kadhaa zitakaporekebishwa, baadhi ya wabunge wa EU wamemuunga mkono na kutahadharisha mkataba wa sasa utaua viwanda vya ndani. Siku kadhaa zilizopita, msimamo wa Tanzania na Burundi ulilazimisha nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kukubaliana kusogeza mbele makubaliano ya ama zote zisaini mkataba huo au la ili kuruhusu uchambuzi zaidi. Tayari nchi za Kenya, Uganda na Rwanda zimekubaliana na mkataba huo wa EPA huku Tanzania na Burundi zikitoa sababu nzito za kiuchumi, zinazolenga kuhakikisha kuwa kabla ya kusaini mkataba huo, ni vyema suala la ulinzi wa viwanda vya ndani likazingatiwa. Mkataba huo unapaswa kusainiwa na nchi zote ili uanze kutumika katika ukanda mzima. Chini ya mkataba huo ambao majadiliano yake yalianza tangu mwaka 2007, EU inaahidi kuzipatia bidhaa kutok

RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AMUAPISHA DKT ZAINABU CHAULA KUWA NAIBU KATIBU MKUU TAMISEMI

Image
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Zainabu Chaula kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Dkt. Zainabu Chaula mara baada ya kumuapisha kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU