KWELI UALIMU KAZI -"MWANAFUNZI MMOJA WA KIKE AMTAKA MWALIMU WAKE KIMAPENZI"
Mimi ni mwalimu wa shule moja ambayo sitaitaja. mwezi uliopita mwanafunzi wangu wa kike ambaye yuko kidato cha tatu alinifuata na kuniambia anataka kunipa zawadi... Sikuwa na hili wala lile, hivyo nilimwambia ni poa tu kama ameamua kunikumbuka mwalimu wake.. Zawadi aloniletea ilinifanya nishike kichwa maana sikutegemea.Yule mwanafunzi aliniletea chupi aina ya boxer 3 na tangu siku hiyo kila akiniona ananifanyia vituko mpaka ananikalia nusu uchi darasana nikiwa nafundisha kwa vile anakaa viti vya Mbele.... Nikiwa kama mwalimu, nimejaribu kutumia viboko ili kumuonesha kwamba sina mpango naye lakini bado imeshindikana.. Nifanyaje ndugu zangu? Maadili ya kazi yananibana.Hata hivyo, mwanao ni mwanetu sote.