UVUMILIVU NI SOMO LA MAISHA, UPO TAYARI KUJIFUNZA?
Kuna mtu mmoja alishawahi kusema hivi, “Mwonekano wako ni halisi unapojionyesha wakati wa mambo magumu, huwezi kuwa zaidi ya hivyo katika utu wako”. Ukiendelea kuwahukumu watu wengine kutokana na tabia zao huwezi ukaona kitu kizuri ndani yao. Badala ya kumwona mfanyakazi mwenzako ni mtata, msumbufu, katili , hana utu, jaribu kumwona mtu huyo kama mwema na anahitaji kueleweka. Tafuta kitu kizuri ndani yake na uweze kwenda naye kwa hicho kizuri. Ingawa mambo kama hayo yamejengeka kwa muda mrefu kutokana na wapi mtu huyo alizaliwa, maisha gani amepitia na mambo gani yameikabili familia yake akiwa mtoto, kama wazazi kupigana, kutoonyeshwa upendo kwa wazazi wake mwenyewe hivyo kuathirika na vitu vingi. Unapojaribu kuchukuliana na udhaifu wa mtu mwingine na jinsi alivyo unahitaji uvumilivu. Fikiria kwamba kuna mfanyakazi unataka abadiLike kutokana na tabia zake, je yuko hapo kukufundisha nini? je wanakupa mwangaza gani na wewe kujiona kwenye kioo? Mara nyingine ni...