Posts

Showing posts from January 21, 2018

Mama wa Askofu Gwajima afariki Dunia

Image
Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima leo Januari 21, 2018 amepata pigo kwa kuondokewa na mama yake mzazi Ruth Basondole Gwajima ambaye amefariki asubuhi ya leo. Gwajima amesema kuwa mama yake mzazi amefariki akiwa na umri wa miaka 84 na kuwa mazishi ya mama yake mpendwa yatafanyika siku ya Alhamisi ya Januari 25, 2018 Salasala jijini Dar es Salaama. "Leo Saa mbili asubuhi mama yangu Mzazi, Bi Ruth Basondole Gwajima ametwaliwa na Bwana. Karudi Mbinguni akiwa na Umri wa Miaka 84. Kuna Furaha ya Ajabu Shujaa Wangu Amerudi kwao. Kwasababu katika maisha yake alimtumikia Mungu. Mazishi yatafanyika Alhamis Tarehe 25/01/2018; Salasala Dar es Salaam" alisema Gwajima. EATV.

Julitha Kabete Kukanyaga Miss World ni Mungu tu!

Image
Mrembo ambaye aliiwakilisha Tanzania katika mashindo ya Miss World 2017, Julitha Kabete. MREMBO ambaye aliiwakilisha Tanzania katika mashindo ya Miss World 2017, Julitha Kabete amesema kuwa mpaka kuweza kupata nafasi ya kwenda kuiwakilisha nchi yake sio kazi ndogo kama watu wanavyodhani kwani ameenda kuonesha ulimwengu kuwa hata taifa lake linaweza, haliko nyuma kitu ambacho kilimfanya asilale kwa ajili ya kuhakikisha anarudi na kitu ambacho kitaacha alama ya nchi yetu. Mrembo huyo amefanya mahojiano na Mikito Nusunusu na kuongea mengi kama ifuatavyo hapa chini: Mikito Nusunusu: Ni kitu gani kilikufanya uamue kwenda kushiriki Miss World nani alikusuma kufanya hivyo? <span style="display: inline-block; width: 0px; overflow: hidden; line-height: 0;" data-mce-type="bookmark" class="mce_SELRES_start"></span> Julitha: Miss World ilikuwa ndoto yangu tangu niko mdogo sana. Pia nilivyozidi kukua niliona kua plat

Faiza ampa somo Diamond

Image
Muigizaji wa Filamu nchini Tanzania, Faiza Ally amempa ushauri msanii wa muziki wa Bongo Fleva Diamond Platnumz kuwa kwa sasa ni muda wake wa kula ujana na kuizunguuka dunia na sio muda wa kujipa majukumu mazito ile hali umri wake bado mdogo. Faiza Ally amesema Diamond bado hajamaliza hata robo ya dunia hivyo ingawaje ana jina kubwa barani Afrika hivyo angefanya kwanza vitu kama hivyo kuizunguuka dunia ikibidi ajiweke kando na mambo ya mahusiano. “Diamond kijana mdogo sana anahitaji kuhave funny na watoto wenzie na sisi wadada wazima lazima taungalie watu wa kutoka nao, Go baba have a funny enjoy the world ndio useto down,“ameandika Faiza Ally kwenye ukurasa wake wa Instagram na kumshauri kuwa ikibidi ajiweke mbali na mahusiano. “Jiachie uwe huru ikibidi usiwe na mahusiano, bado hujaiona dunia hata robo wewe ni star hela ipo there is alot to see nasema with clean heart no hate kwa Zari au kwa yeyote.“ameandika Faiza. Ushauri huo umekuja ikiwa ni wiki sasa imepi

FT: RUVU SHOOTING 0-1 YANGA, KUTOKA UWANJA WA TAIFA

Image
Kiungo mahiri wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi (kushoto) akifanya yake na wachezaji wa Ruvu Shooting. MPIRA UMEKWISHA DAKIKA YA 93 SUB Dk 81 Abdulrahman Mussa anakwenda nje Hamisi Mcha anachukua nafasi yake Dk 80, Yanga wanacheza kindava nje kidogo ya nje ya lango lao. Inachongwa faulo, shuti kali linapigwa, goal kick Dk 78, Bofu anageuka vizuri, anapiga krosi safi, al manusura iingia nyavuni Dk 73, Ruvu wanapata kona hapa, inachongwa vizuri, Kanduru anaachia mkwaju, goal kick Dk 71, Dante yuko chini baada ya kusukumwa na Kanduru Tambwe akiwa kaweka mtu kati. DK 88, krosi safi ya Martin, Mahadhi yeye na nyavu, anapaishaa puuuuuu SUB Dk 86 Daud anakwenda benchi na nafasi yake inachukuliwa na Pato Ngonyani, Yanga wakiimarisha ulinzi SUB Dk 81 Abdulrahman Mussa anakwenda nje Hamisi Mcha anachukua nafasi yake Dk 80, Yanga wanacheza kindava nje kidogo ya nje ya lango lao. Inachongwa faulo, shuti kali linapigwa, goal kick SUB Dk 70 Buswita analambwa kadi ya njano ba

Waziri Mpina awasilisha majina ya Viongozi waliokaidi agizo la Serikali

Image
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amewasilisha majina ya viongozi wa halmashauri ambazo hazijaanza kutekeleza upigaji chapa mifugo na zile ambazo ziko chini ya asilimia 10 ya utekelezaji, Kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo ili zichukuliwe hatua. Mpina alibainisha hilo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa upigaji chapa mifugo nchini, mjini Dodoma. Alisema kwa tathmini iliyofanyika hadi sasa jumla ya ng’ombe 10,306,359 sawa na asilimia 59.3 wamepigwa chapa huku asilimia 40.7 wakiwa hawajapigwa chapa na zoezi hilo linatarajiwa kukamilishwa Januari 31, mwaka huu. “Halmashauri 100 zimepiga chapa zaidi ya asilimia 50, halmashauri 54 zimepiga kati ya asilimia 10 hadi 50, halmashauri 14 zimepiga chini ya asilimia 10 na Halmashauri 9 hazijaanza kupiga chapa,” alisema Mpina. Alizitaja halmashauri ambazo hazijaanza kabisa ni Tandahimba,

Anayecheza Na Moyo Wako ni Sawa Na Muuaji; Utamjuaje?

Image
WENGI wamejikuta kwenye majuto kwa kuwakabidhi watu wasiofaa mioyo yao. Wameambulia mateso makali, wamejikuta wamepoteza muda kwani wameachwa solemba wakati ambao hawakuutarajia. Ndugu zangu mapenzi yanauma. Yanauma kwelikweli hasa linapokuja suala la kumkabidhi mtu moyo wako ukiamini atakupenda, atakuthamini kama vile wewe unavyomthamini. Unakuwa na matumaini kwamba nipo na mtu sahihi. Mtu ambaye nitafanya naye maisha, mtu ambaye nitadumu naye katika shida na raha, mtu ambaye nitaingia naye kwenye ndoa mwisho wa siku anaingia mitini, inauma sana. Mapenzi ni uwekezaji. Unawekeza nguvu, akili na maisha. Unapokuwa na mwenzi wako unamuamini. Unapanga naye mipango ya kufika mbali kwani kila ambaye anawaza maisha, lazima atakuwa anaifikiria ndoa na mtu sahihi. Atafikiria familia kwa maana ya kupata watoto, kusomesha na mambo mengine yahusuyo familia. Hiyo ndio safari ya wapendanao, inayoanzia kwenye urafiki, uchumba na hata baadaye ndoa. Wahusika wanapoikamilisha safa

Waziri Mkuu atoa agizo kwa TAKUKURU

Image
Waziri Mkuu .Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa ameaagiza TAKUKURU kumkamata Meneja wa TBA wilaya ya Butiama mkoani Mara kutokana na uzembe na kutumia fedha za Serikali kinyume na maelekezo. Waziri Mkuu amefanya maamuzi hayo baada ya Serikali kupeleka fedha zaidi ya milioni 600 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la halmashauri lakini mpaka sasa fedha ujenzi huo haujaanza na fedha hizo kutumika katika miradi mingine ambayo haijapangwa na Serikali. "Tumeleta fedha milioni 600 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la halmshauri lakini mmezipeleka kwenye shughuli nyingine, kwanini hajajenga jengo hili ikiwa fedha zimeshaletwa? Tumeleta fedha milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa Wilaya, DAS na nyumba ya watumishi lakini mmejenga nyumba moja tu ya DC, nyumba zingine mbona hamjaanza kujenga? Waziri Mkuu baada ya kukosa majibu yanayoridhisha kutoka kwa viongozi hao ndipo alipoagiza TAKUKURU kumchukua moja ya mtumishi wa halmshauri hiyo na kusema kuwa serikali haiwezi ku

WAZIRI MKUU KUZAA BAADA YA KUINGIA OFISINI

Image
WAZIRI Mkuu wa New Zealand, Jacinda Ardern anategemea kujifungua mwezi Juni mwaka huu na kumfanya kuwa kiongozi wa kwanza duniani tangu 1990 kujifungua akiwa ofisini, jambo ambalo watu wengine wanadai ni tatizo. Tukio hilo hili halimhusu aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza, Tony Blair,  ambaye alipata mtoto aitwaye Leo, kutoka kwa mkewe Cherie,  jambo ambalo lilimfanya Blair ajikute ‘akimnyonyesha’ mtoto wake huyo kwa njia fulani huku akiwa anaendelea na kazi zake. Akiwa na mwenza wale, Clarke Gayford, wakitangaza ujauzito wake. “Mwaka huu tutaungana na wazazi wengi wanaovaa kofia mbili.  Nitakuwa waziri mkuu na mama, ambapo Clarke (Gayford) atakuwa Mwanamume wa Kwanza (mume wa waziri mkuu),” alitangaza Ardern mwenye umri wa miaka 37, akimtaja mwanamume huyo, mtangazaji katika kituo kimoja cha televisheni, kuwa ndiye mwenza wake katika ujauzito huo. Waziri Mkuu wa New Zealand, Jacinda Ardern. Clarke, ambaye pia ni mpenzi wa kuvua samaki, watashirikiana na

Snura: Mwanamke anayelea watoto mwenyewe ni elimu tosha Duniani

Image
MWANAMUZIKI anayefanya vizuri kwenye miondoko ya mduara, Snura Mushi, ameibuka na kudai kuwa mwanamke anayelea watoto mwenyewe ni elimu tosha duniani. Akizungumza na Mikito Nusunusu, Snura alisema kuwa, amepata changamoto nyingi sana kwenye kulea watoto wake lakini anashukuru amesimama vyema kama mwanamke shujaa na amejifunza mengi ikiwa ni pamoja na kuwa jasiri ambapo anaweza kusimama popote sasa na kujiamini. “Yaani kulea watoto mwenyewe kama mwanamke ni elimu tosha ya duniani na mimi najivunia hilo sana, mwanzo ilikuwa ni ngumu sana na sisi wanawake tumekuwa tukiwategemea sana wanaume wakiwepo lakini ukiyajaribu maisha ya ulezi peke yako na kuyashinda unajikuta jasiri ambaye unaweza

Joyce Kiria amwaga siri za mumewe hadharani

Image
Mwanaharakati na mwanamke shujaa nchini Tanzania, Joyce Kiria ameweka hadharani kuwa mahusiano yake kwa sasa na mumewe Henry Kileo ambaye alishawahi kushika nyadhifa mbalimbali CHADEMA. Joyce Kiria amesema kuwa kwasasa mahusiano yake hayapo sawa kwani yeye amekuwa ndiye baba na mama wa familia kwa kila kitu yaani kuhudumia familia nzima pamoja na mumewe. Akitoa taarifa hiyo kwa umma kupitia ukurasa wake wa Instagram huku akibubujikwa na majozi, Kiria amesema huwa anamshauri mumewe atafute japo kazi itakayowaingizia kipato ili kusaidiana kutunza familia lakini mumewe anakuwa mkali na kumpiga. “Sikutegemea kama ipo siku kwa mkono wako ungeunyanyua kunipiga (@kilewo2020mwanga) ukasahau kabisa! ukasahau yooote. Nimeharibu career yangu kupigania ndoto yako kwa kugawa watu wangu kwenye biashara zangu, nimepoteza ndugu jamaa na marafiki, umeniachia nimebeba mzigo wa familia kwa muda wote, Malipo yako ni kunipiga/ kunidhalilisha na kunitoa machozi, umenipiga kwa sababu