Posts

Showing posts from June 10, 2015

ISIS WAMWUA MFUNGWA BAADA YA KUJICHIMBIA KABURI LAKE

Image
Mfungwa akichimba kaburi lake. ...Akiwa amepewa fursa ya kuongea na watu awatakao. Mfungwa (mguu wake ukionekana kushoto chini) akiwa ameanguka kaburini baada ya kuuawa. Muuaji akifukia mwili wa mfungwa aliyeuawa. MFUNGWA ambaye wapiganaji wa kundi la ISIS lilimtuhumu kuwa jasusi wa Israel (Mossad) hivi majuzi aliuawa kwa kupigwa risasi kichwani katika jangwa la Sinai, Misri. Kwa mujibu wa video zilizopatikana, mfungwa huyo anaonekana akiwa amesimama katika shimo akichimba kaburi lake, akapigwa risasi nyuma ya kichwa na kusukumiziwa katika kaburi hilo. ISIS wamesema mtu huyo alikuwa anafanya ujasusi na kuripoti kwa serikali ya Israel kuhusu shughuli za ISIS eneo hilo la Misri.

ANGALIA HAPA KUONA NAFASI ZA AJIRA KUTOKA JESHI LA POLISI 2015

Image
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI JESHI LA POLISI TANZANIA TANGAZO LA AJIRA Jeshi la Polisi Tanzania linatangaza nafasi za ajira kwa mwaka wa fedha 2015/2016 kwa vijana wenye elimu ya vyuo vya elimu ya juu, waliosomea ujuzi/fani mbalimbali toka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali na wahitimu wa kidato cha sita wa mwaka 2014 waliopitia Jeshi la Kujenga Taifa kwa mujibu wa sheria. Wahusika watajaza fomu baada ya kujazwa kikamilifu wataambatanisha vivuli vya vyeti na kutuma Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kwa njia ya Posta kabla ya tarehe 31/06/2015. Kwa anuani ifuatayo: Inspekta Jenerali wa Polisi, Makao Makuu ya Polisi, S.L.P. 9141, DAR ES SALAAM. SHAHADA Maendeleo ya Jamii(Community development),Ushauri Nasihi [Counselling Psychologist](2) Uchumi(Economy)(10)Ualimu(Education)(2)Menejimenti ya Rasilimali watu(HRM), Utawala katika Utumishi wa Umma(Public Administration)(3) Usimamizi na Utekelezaji wa Sheria[BaLE](12) Sher...

KAJALA AFUNGUKA MAZITO KUHUSU WEMA NA PETITMAN..HEBU MSIKIE HAPA TUU USHANGAE

Image
Binadamu tuliumbwa kuishi katika misingi ya ubinadamu na sio unyama kama waishivyo wanyama wa porini leo naomba kusema kutoka moyoni mwangu.. Najua kabisa nina wazazi wangu ndugu zangu na zaidi sana Mungu wangu ila kuna watu mpaka nakufa kamwe sintowasahau katika kuta za moyo wangu katika kipindi changu kigumu nilichopitia mlikuwa nembo namboni kubwa katika kuokoa maisha yangu... Napenda kusema kuwa hata kwa haya yote tunayopitia bado ni madogo sana kuficha thamani yenu mliyoijenga juu yangu. Nakumbuka sana mlipojitoa kwa ajili yangu mlipojinyima kwa ajili yangu mlipopigana kwa ajili yangu,mlivyofedheheka kwa ajili yangu yote hayo nayakumbuka na namshukuruu mungu kwani naona kabisa mliletwa duniani kwa sababu nyingi na moja ya sababu ilikuwa kuniokoa katika kipindi kigumu katika maisha yangu. Leo hii tarehe 25.5.2015 napenda kusema kwa umma na zaidi kwa Mungu wangu kuwa nawathamini nawapenda na nashukuruuu sana kwa yote mliyofanya juu yangu. Nawaombea kwa Mungu muendele...

WEMA SEPETU AMKEJELI MSANII WA BONGO FLEVA LINAH!

Image
Staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu ‘Madame'. NI shiida! Siku chache baada ya msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Esterlina Sanga ‘Linah’ kulalamika juu ya kitendo cha Wema Sepetu ‘Madame’ kumchukua aliyekuwa bwana’ake Nangari Kombo, muigizaji huyo ameibuka na kutoa maneno yanayoashiria kejeli, kuwa aache presha, kwani zile ni picha tu! Katika gazeti la Risasi Jumamosi, toleo lililopita, iliripotiwa na kuchapishwa habari na picha zilizomuonyesha Madame akiwa amepozi kitandani na kijana huyo, aliyepata umaarufu baada ya kuingia ndani ya eneo la kuchezea katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam mwaka 2010, wakati wa mechi kati ya Brazil na Taifa Stars na kumkumbatia kiungo nyota wa mabingwa hao wa zamani wa dunia, Kaka. Lakini Risasi Mchanganyiko lilipotaka kujua maoni yake juu ya shutuma hizo, Wema alisema kupiga picha na Nangari hakumaanishi mapenzi, kwani yeye ni mtu wa watu na picha kama hizo hupiga na marafiki zake wengi tu, hivyo Linah asiwe na sh...

LOWASA KAMA RAIS-TIZAMA ALIVYOTUA NYUMBANI KWA BABA WA TAIFA

Image
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, akisalimiana wanachama wa CCM waliofika kumpokea katika Uwanja wa Ndege Musoma mkoani Mara jana kwa ajili yakutafuta wanachama wakumdhani kugombea Urais.    Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, akiwapungia mkono wanachama wa CCM waliofika kumpokea katika Uwanja wa Ndege Musoma mkoani Mara jana kwa ajili yakutafuta wanachama wakumdhani kugombea Urais. Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, akizungumza na wanachama wa Chama Chama Mpinduzi(CCM )nje ya Ofisi ya Wilaya ya Bunda mkoani Mara baada wakati alipofika kwa ajili yakutafuta wanachama wakumdhani kugombea Urais.  Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, akiweka shahada la maua kwenye Kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere Butiama baada ya kutembelea makazi ya Mwalimu wakati akiwa mkoni humo kwa ajili yakutafuta wanachama wakumdhani kugombea Urais. Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, akiwasha  mshumaa kwenye Kaburi la Baba wa...