Haji Manara Awapa Makavu Mashabiki wa Simba
Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara. Msemaji wa klabu ya Simba mwenye mbwembwe nyingi miongoni mwa klabu za soka nchini, Haji Manara, ameibuka kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuwapa makavu mashabiki wa Simba wanaoponda ushindi wao bao 1-0 dhidi ya Prisons walioupata jana uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar katika mchezo uliofungua pazia la Ligi Kuu mwaka huu. Alichokisema:- Wakati mwingine najiuliza nn wanadaamu wanataka?hasa washabiki wa Mpira!! Nimetalii kdogo kwenye magroup machache ya Wanasimba kwenye WhatsApp nimeshangaa baadhi yetu kutokuridhika na ushindi wa leo wa goli moja dhidi ya Prisons Wengine kwenye Instagram wanafika mbali zaidi eti mfumo wa kocha haufai!! Guys mpira ni sayansi kubwa kuliko kwenda mwezini au daktari kumfanyia upasuaji wa kichwa mtu,ukubwa wa Sayansi hii ni kwamba hujui mpinzani wako kajipangaje..hujui kama siku hyo wachezaji wako watacheza kwa kiwango gani lakini kubwa Sayansi hii haina jawabu la moja kwa moja kam