
Aunt Ezekiel
MUIGIZAJI wa kitambo kwenye tasnia ya filamu, Aunt Ezekiel, ambaye
pia ni mzazi mwenzie na dansa maarufu wa Wasafi Classic Baby (WCB),
Moses Iyobo, amesema kuwa hana mpango wa kufunga ndoa na dansa huyo
japokuwa wameshakaa wote zaidi ya miaka mitatu kwani kikubwa
wanachokiangalia ni kulea mtoto wao Cookie.

Aunt Ezekiel akiwa na mzazi mwenzie na dansa maarufu wa Wasafi Classic Baby (WCB), Moses Iyobo
Akizungumza na
Amani, Aunt alisema kuwa
siyo kwamba mtu akifunga ndoa ndiyo anaweza kuishi vizuri na mwanaume
wake, bali ni kwamba anachojua kuishi vizuri ni sifa moja kubwa ya
kuendelea kuwa pamoja ni kupeana heshima na kila mmoja kutambua
anachokifanya.
“Mimi sitaki hata kukuficha wala sijawahi kufikiria kufunga ndoa na
Iyobo leo wala kesho kikubwa tunaishi vizuri na tunalea mtoto wetu
ipasavyo hilo ndilo ninalolitaka na si vinginevyo kwani kuolewa siyo
ishu kikubwa malezi ya mtoto tu,” alisema Aunt.
STORI NA IMELDA MTEMA | GPL
Comments
Post a Comment