Posts

HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI YAJIDHATITI KUIMARISHA MAWASILIANO NA WANANCHI

Image
Kiongozi wa ujumbe kutoka Chama cha maafisa Habari na Mawasiliano  Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari MAELEZO  Bi. Gaudensia  Simwanza akisisistiza jambo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara Bi.  Changwa Mkwazu      wakati wa ziara ya ujumbe huo katika halmashauri hiyo uliolenga kuona utendaji kazi wa Maafisa  Habari na Mawasiliano na namna wanavyokabiliana na changamoto mbalimbali ili kuweza kuisemea Serikali kimkakati. Kiongozi wa ujumbe kutoka Chama cha maafisa Habari na Mawasiliano  Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari MAELEZO Bi. Gaudensia Simwanza akisisitiza jambo kwa Afisa Habari na Mawasiliano wa Halmashuri ya Wilaya ya Masasi Bi mara baada ya ziara ya ujumbe huo katika Halmashuri hiyo. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara Bi. Changwa Mkwazu akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya  ujumbe  wa viongozi wa Chama cha maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Ha

Nyumba mbili zachomwa Moto Mwanza kisa wizi

Image
Na Paschal D.Lucas, Mwanza Wananchi waliojichukulia sheria mkono wamechoma nyumba mbili za familia moja na nyingine kuziharibu katika mtaa wa Nyakabungo "A" kata ya Isamilo wilayani Nyamagana Mkoani Mwanza  baada ya kuona watoto wa familia zile wanajihusisha na uhalifu hapo mtaani hapo mara kwa mara. Maamuzi hayo yamekuja baada ya wananchi kudai kuwa watoto hao wamekuwa wakikamatwa na kupelekwa mahakamani kushitakiwa lakini mara nyingi wamekuwa wakiachiwa kwa dhamana na kurudi mtaani kuendelea tena na tabia hiyo kitendo ambacho kimekuwa ni kero kubwa  kwa wananchi wa eneo hilo. Tukio hilo lilitokea majira ya saa 3 usiku wa tarehe 25,Julai 2018 ambapo katika tukio hilo nyumba mbili zilizoharibiwa ni mali ya Selina Francis (50) na Abdallah Mwita wote wakiwa ni wakazi wa Nyakabungo mkoani humo. Vile vile nyumba moja mali ya Manka Francis James iliharibiwa vibaya na kundi hilo kwa kuvunjwa milango na madirisha na kuharibu vitu mbalimbali vilivyokuwemo ndan

Tambwe Afunguka Mazito Yanga

Image
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe ameibuka na kusema wanaumizwa na hali inayoendelea katika timu hiyo lakini haiwafanyi washindwe kupigana huku wakiwaomba mashabiki kuwa kitu kimoja kabla ya mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia ya Kenya. Yanga inatarajiwa kurudiana na Gor Mahia Jumapili ya wiki katika mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar baada ya ku­fungwa mabao 4-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Kenya. Akizungumza na Championi Jumatano , Tambwe alisema kwa sasa bado wanapita katika kipindi kigumu lakini hawezi kuwafanya washindwe kufanya vizuri katika mchezo huo wa maru­diano huku akiwaomba mashabiki wasichoke kuwasapoti. “Tunajua matokeo hayakuwa mazuri kwetu katika mchezo wa kwanza kwa sababu hakuna ambaye alitege­mea tutapoteza tena kwa idadi kubwa ya mabao lakini kwa kuwa wenzetu walitumia mapungufu yetu kupata ma­tokeo. “Nadhani huu ni wakati wa kuende­lea kushikamana, mashabiki wetu hawa­paswi kuendelea kuka

Mbelgiji Aanza Kukiunga Kikosi Upya

Image
KOCHA Patrick Aussems raia wa Ubelgiji ameanza kutoa mafunzo ya mfumo anaotaka kuutumia katika msimu wa 2018/19 akiwa na Simba. Simba imeweka kambi ka­tika mji mdogo wa Kartepe ambao uko mlimani kabisa, sehemu maalum kwa ajili ya kambi za timu. Aussems ameanza kukinoa kikosi chache akiwafundisha mifumo na namna ya uchezaji katika masuala mbalimbali. Kocha huyo amekuwa aki­waonyesha wachezaji wake namna ya kulinda lakini pia kushambulia kwa tahadhari. Wakati Simba ilipotua hapa, kocha huyo alianza kutoa mafunzo ya kawaida, zaidi wachezaji wakioneka­na kupasha misuli kawaida. Inaonekana ame­kuwa akiongeza mazoezi taratibu huku akichanganya na aina ya uche­zaji. Makocha wengi huanza kufundisha mifumo baada ya timu zao kupata mazoezi ya kuto­sha. Lakini Mbelgiji huyo anaonekana kuwa tofauti ki­dogo akienda anachangan­ya mazoezi ya kawaida na mifumo, taratibu.

Beki Simba atua Singida United kwa mkopo

Image
Klabu ya soka ya Singida United imethibitisha kuwa imemsajili mchezaji Jamaly Mwambeleko kutoka Simba kwa usajili kamili tofauti na taarifa zilizoeleza kuwa wamemchukua kwa mkopo, huku wakiweka wazi kuwa wamemwongeza mwaka mmoja na sasa ni mchezaji wao kwa miaka miwili. Mkurugenzi wa Singida United Festo Sanga ameeleza kuwa walifanya mazungumzo na Simba na kumalizana nao kisha kumpa mkataba wa mwaka mmoja Jamaly Mwambeleko lakini baadae walimwongeza mwaka mmoja na kuwa miwili. ''Tumemsajili Mwambeleko kwa usajili kamili wala hajaja kwetu kwa mkopo, ila awali mazungumzo yalikuwa hivyo lakini kocha Hemed Morocco akapendekeza tuwe naye kwa muda mrefu ndio akasaini mkataba wa kuitumikia Singida United kwa miaka miwili'', - amesema. Jamaly Mwambeleko ambaye anacheza nafasi ya mlinzi wa kushoto ni sehemu ya wachezaji walioachwa na Simba katika usajili huu kwa kile kilichoelezwa ni kutokuwa na nafasi ya kucheza hususani nafasi yake pale Simba kuwa na w

Jafo azitaka halmashauri kutoweka riba mikopo ya wajasiriamali

Image
Waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa Selemani Jafo amezitaka halmashauri za miji na majiji kutoweka riba katika fedha za mikopo zinatolewa kwa ajili ya vikundi vya wajasiriamali hapa nchini. Akizungumza wakati wa kukabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 950 zilizotolewa na jiji la Dodoma kwa wajasiliamali, Mheshimiwa Jafo amesema serikali ya awamu ya tano inalenga kuwawezesha watanzania hivyo haikubali wananchi kutozwa riba. Akizungumza katika tukio hilo, naibu waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera,bunge,ajira kazi vijana na watu wenye ulemavu Mhe. Anthony Mavunde amesema jiji la Dodoma ni kati ya halmashauri chache nchini zilizoweza kutimiza sheria ya kuhakikisha linatoa mikopo kwa vikundi vya kina mama,vijana na watu wenye ulemavu ili Kuwawezesha kuondokana na umaskini. Akielezea kuhusu fedha hizo, mkurugenzi wa jiji la Dodoma Bw.Godwin Kunambi amesema jiji la Dodoma limevuka malengo ya ukusanyaji wa mapato ya ndani kutoka

KINDA WA LEICESTER CITY AITWA SERENGETI BOYS KUCHEZA MICHUANO YA CECAFA

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limemualika mchezaji wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 16 ya Leicester City ya England, Anthony Starkie kuja kujiunga na timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys. Taarifa ya TFF usiku wa Jumatano imesema kwamba Starkie anatarajiwa kuwasili Alhamisi mjini Dar es Salaam baada ya kuruhusiwa na Leicester City, mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu ya wakubwa England. Atajiunga na Serengeti Boys ambayo inajiandaa kushiriki michuano maalum ya vijana Afrika Mashariki na Katik ijulikanayo kama CECAFA Zonal Qualification. Wazi uamuzi wa TFF kumuita kijana huyo unafuatia agizo la Mkurugenzi wa Michezo, Dk. Yusuphu Singo kwamba wafuatilie vipaji vya wachezaji wa Kitanzania wanaocheza nje. Singo alitoa kauli hiyo kufuatia mshambuliaji Yussuf Yurary Poulsen, anayezaliwa na baba kutoka Tanga  kuichezea Denmark, nchi ya mama yake kwenye fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu nchini U

Makamu wa Rais aahidi Serikali kutatua changamoto ya barabara Mbeya

Image
MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wakazi wa Mkoa wa Mbeya kwamba serikali imejipanga kutekeleza na kutatua changamoto muhimu za kimaendeleo, ikiwemo ya miundombinu ya barabara. Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati akizungumza na mamia ya wananchi katika eneo la Mbalizi Wilayani Mbeya eneo linalotajwa kuongoza kwa matukio ya ajali za barabarani.  Amesema, katika kulitekeleza hilo, tayari serikali imeshughulikia changamoto ya ujenzi wa barabara ya mchepuko ya kilomita 40 ambayo itasaidia kupunguza au kudhibiti ajali za barabarani zinazotokea kwenye barabara kuu ya Tanzania na Zambia (TAZAMA).  “Mwaka juzi mlifanya kazi kubwa sana, tumekuja kuwahikikishia kwamba serikali itatekeleza yale yote tuliyo ahidi, nadhani spidi mnaiona,”amesema. Mama Samia pia amewataka wananchi kuendelea kudumisha amani kwani ndio sialaha ya maendeleo na kuwasisitiza kuchaguai viongozi watakaoendana na kasi ya rais na waioendekeza tama wakati wa uchaguzi wa viongozi

BREAKING: SANGA ATANGAZA RASMI KUACHIA NGAZI YANGA

Image
Kaimu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga, ametangaza rasmi kujiuzulu wadhifa wake katika klabu hiyo. Sanga amejiuzulu wadhifa huo kutokana na kutokuwa na maelewano mazuri baina yake na viongozi wenzake ndani ya klabu hiyo ikiwemo wale wa Kamati ya Utendaji kueleza hana ushirikiano mzuri. Kiongozi huyo aliyekuwa akikaimu nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, alikuwa akitupiwa lawama na viongozi wa Kamati ya Utendaji akiwemo Khalfan Hamis ambaye amejiuzulu juzi akidai Sanga amekuwa si mweledi wa mambo. Mbali na kukosa maelewano, Sanga ameeleza kuwa kuna CLIP ameiona mitandaoni inayohamasisha watu kumvamia kwa mapanga ni moja ya sababu zilizopelekea kufanya uamuzi wa kuachia ngazi. Aidha,wiki kadhaa zilizopita Mjumbe mwingine kutoka kamati hiyo, Salum Mkemi naye aling’atuka kuendelea na wadhifa huo ndani ya Yanga na akisalia kuwa mwanachama pekee kutokana na kutokuwa na kukosa maelewano mazuri baina yake na wanachama wa klabu. Ukiachana na Sanga, Kati

Rais Magufulia atoa agizo kwa Mkandarasi Daraja la Salender

Image
Rais John Magufuli amemuagiza Mkandarasi aliyepewa kazi wa kujenga daraja kubwa la Selander Bridge kutoka Coco Beach mpaka Agha Khan litakalogharimu shilingi bilioni 250 kwa ufadhili wa Serikali ya Korea kusini kukamilisha kazi hiyo kwa wakati ndani ya miezi 36 aliyopangiwa  kufanya kazi. Rais Magufuli ametoa agizo hilo baada ya kushuhudia mkataba wa utiaji saini ujenzi wa darala hilo ambalo litakuwa na urefu wa kilomita 6.23 mbele ya Waziri Mkuu wa Korea Kusini Mh.0 Lee Nak-Y eon Ikulu jijini Dar es Salaam na kusema kukamilika kwa daraja hilo kutaendelea kubadilisha taswira mpya ya Jiji la Dar es Salaam katika miundombinu ya barabara. Katika tukio jingine, hivi sasa Rais Magufuli anapokea gawio la kipindi cha mwaka 2017/18 kutoka Wakala, Kampuni, Taasisi na Mashirika ya Umma 47 ambayo Serikali inamiliki hisa.

Tanga: Diwani wa CUF Avuliwa Udiwani kwa Kutofika Vikaoni

Image
HALMASHAURI ya Jiji la Tanga imemuondoa kwenye nafasi yake, Diwani wa Kata ya Ngamiani Kusini, Mussa Mbarouk,  ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini, baada ya kupoteza sifa kwa kutohudhuria vikao sita mfululizo. Kata hiyo sasa imetangazwa kuwa wazi. You May Like

Madiwani wapita bila kupingwa Uchaguzi mdogo wa Udiwani- Mbulu.

Image
  Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mbulu ndugu Hudson S. Kamoga akisoma taarifa ya maamuzi ya rufaa za Wagombea Udiwani katika kata za Tumati na Hayderer . Akiongea na vyombo vya habari hii leo ofisini kwake Msimamizi wa Uchaguzi   jimbo la Mbulu, ndugu Hudson Stanley Kamoga amewatangaza Madiwani wawili wa kata ya Tumati ndugu Paulo Emanuel Axwesso (CCM) na ndugu Justine Sidamuy Masuja Hayderer(CCM),wamepita bila kupingwa   baada ya Wapinzani wao kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kushindwa rufaa waliokata Tume ya Taifa ya Uchaguzi dhidi ya Uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi.   Msimamizi msaidi wa jimbo la Mbulu ndugu Michael Faraay(wa kwanza kushoto) akiwa na mratibu wa uchaguzi ndugu Stedvant Kileo wakimsikiliza kwa makini msimamizi wa uchaguzi (hayupo pichani)wakati wakusoma maamuzi ya rufaa Akitoa taarifa juu ya maamuzi ya rufaa hiyo iliyotolewa na tume ya taifa ya Uchaguzi,msimamizi wa uchaguzi halmashauri ya Wilaya ya Mbulu amesema amewaita wagom

Nafasi za Kazi 17 Mamlaka ya Maji Musoma

Image
Musoma Water Supply and Sanitation Authority (MUWASA) is a utility established under section 9 of the Water Supply and Sanitation Act No. 12 of 2009 with the objective of provision of Water Supply and Sanitation services in Musoma Municipality. In this respect, the activities of MUWASA have specifically expanded and the authority now invites application from suitably qualified and skilled individuals who are dynamic and result oriented to fill the following posts:- 1:0 Position: Assistant Technician II 6 Post 1:1 Reporting to: Production Engineer 1:2 Duties and Responsibilities 1) Customer Plumbers i. To repair all water leakages. ii. To assist in connecting new water customers as scheduled. iii. To report on unauthorized water connection. iv. To report of sewerage pipe faults to responsible officers. v. To assist in carrying out water disconnections and re-connections. vi. To reconnect water debtors as assigned timely. 2) Technical Plumbers i. To attend to cust

Mama Afungwa Jela kwa Kuruhusu Wanaume Kumbaka Mwanaye

Image
MWANAMKE Azzie Watson (25) wa Independence, Kansas City, Marekani, ameshitakiwa kwa kuuruhusu wanaume kumbaka mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka miwili. Mahakama iliambiwa kwamba mtuhumiwa huyo alikuwa kila mara anasema alimpeleka mtoto wake huyo kwenye nyumba fulani ambako alibakwa mara tano.  Maneno hayo yanadaiwa yalinaswa na rafiki yake wa kiume kwenye kinasa sauti. Watson alikana madai hayo, lakini pia akasema hajui ni kwa nini mtoto wake huyo aliambukizwa ugonjwa wa zinaa. Mtoto huyo wa mtuhumiwa na mdogo wake wa kiume walichukuliwa na kwenda kulelewa na watu maalum wakati kesi ilipoanza kuunguruma. Wakiwa huko, Juni 29, mwaka huu, mama anayemlea alimsikia binti huyo, wakati anamvua nepi, akimlalamikia mwanamme ambaye mlezi huyo hakumjua. “Baba inaumiza.  Baba, usiwe katili.  Baba, inaumiza,” alikuwa akilalamika mtoto huyo. Polisi wamemkata mwanamme mmoja Charles Green (43) kwa mashitaka mawili ya kuhatarisha maisha ya mtoto.  Mtu huyo anadaiwa kuw

JPM ATOA POLE KWA KIKWETE KUFIWA NA BABA MKEWE

Image
Rais John Magufuli akilakiwa na rais mstaafu Jakaya Kikwete alipofika kutoa pole kwa kufiwa na baba mzazi wa mkewe Mama Salma Kikwete, marehemu Rashid Mkwachu, nyumbani kwa wafiwa Msasani jijini Dar es Salaam leo Julai 21, 2018. Mke wa Rais Magufuli, Mama Janeth Magufuli, akilakiwa na Kikwete kwenye msiba huo. Magufuli akimpa pole mke wa Kikwete,  Mama Salma Kikwete.  Magufuli  na Kikwete wakati wa dua.  …Dua ya familia kwa ajili ya marehemu. Rais na mkewe wakiagana na wafiwa. …Akiendelea kuagana na waliofika msibani. Magufuli na mkewe wakisindikizwa.  RAIS  John Magufuli na  mkewe Mama Janeth Magufuli , wamefika nyumbani kwa rais mstaafu, Jakaya Kikwete,   kutoa pole kwa kufiwa na baba mzazi wa mkewe Mama Salma Kikwete, marehemu Rashid Mkwachu, nyumbani Msasani jijini Dar es Salaam leo Julai 21, 2018. Picha na IKULU

Naibu Meya, Madiwani CHADEMA Wajiuzulu Mbeya

Image
IKIWA ni saa chache baada ya uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani Mbeya kupendekeza kuwavua uanachama madiwani watatu wa chama hicho mkoani humo kwa utovu wa nidhamu waliouonyesha, madiwani hao wamejiuzulu nyadhifa zao hizo. Madiwani hao na kata zao katika mabano ni Geofrey Kajigili (Sisimba), Newton Mwatuboje (Manga)na Hamphrey Ngalawa (Iwambi). Madiwani hao wamejiuzulu leo Jumamosi  Julai 21, 2018 baada ya Mwenyekiti wa Chadema Mbeya Mjini, Obadia Mwaipalu,  kutangaza uamuzi huo  katika mkutano wake na waandishi wa habari na kubainisha kuwa  vikao halali vya chama vilivyoketi mara kadhaa kujadili hatua stahiki dhidi ya madiwani vimefikia uamuzi huo. Amesema kutokana na utovu wa nidhamu, kukiuka katiba ya Chadema na kukaidi utekelezaji wa maazimio ya uongozi, wamepeleka mapendekezo yao kwa uongozi wa chama hicho Kanda ya Nyasa ili  hatua zichukuliwe. Aliyekuwa Naibu Meya na Diwani wa Kata ya Nsalaga Mjini Mbeya, Mchungaji David Ngogo (

Simba Kufikia Kambi ya Kishua Uturuki

Image
JUMLA ya wachezaji 26 wa kikosi cha Simba, wanatarajiwa kuondoka kesho Alfajiri kuelekea Uturuki kuweka kambi ya takribani wiki mbili kabla ya kurejea hapa nchini Agosti 5, mwaka huu. Wachezaji wa Simba ambao watakuwa kwenye safari hiyo jana Ijumaa walikuwa na zoezi la upimwaji wa afya kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar. Katika nyota hao 26 watakaosafiri, kiungo mkongwe, Mwinyi Kazimoto, hatakuwepo kwenye msafara huo ambao utaongozwa na kocha mpya wa kikosi hicho, Patrick Aussems raia wa Ubelgiji. Msafara mzima wa Simba unaotarajiwa kwenda Uturuki kwenye kambi hiyo, utakuwa na jumla ya watu 35. Chanzo cha uhakika kutoka ndani ya Simba, kimelidokeza Championi kuwa, mbali na Kazimoto, pia Mosses Kitandu, Jamal Mwambeleko, Ally Shomary na Said Mohammed ‘Nduda’ nao watabaki hapa nchini. “Kama ambavyo imepangwa, kikosi kitaondoka Jumapili alfajiri ambapo baada ya kocha mpya kutangazwa jana (juzi Alhamisi), yeye ndiye atakuwa anawaongoza vijana wake

Nafasi Ya Kazi Kwa IT Kutoka Car & General Trading Limited

Image
Car & General Trading Limited is looking for well qualified and competent candidates for the following post: IT Person Qualifications: • Minimum 2 yrs experience in IT • Web graphic and animation design • Knowledge in database programming • Knowledge of Web and Mobile Applications • Good communication skills • Excellent diagnostic and problem solving • Knowledge in Software development • Technical Support Skills/IT Support Education Qualification: Degree in computer Science, Engineering or relevant field Persons with proven experience in IT are encouraged to apply before 20/712018. Package: An attractive salary to be offered to experience candidate. Apply to: HR Manager, Car & General Trading / Tanzania Limited. P.O. Box: 1552, Dar Es Salaam. Tanzania. Source: The Guardian July 11, 2018

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Makame Mnyaa Mbarawa kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Eng. Isack Kamwelwe kuwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Kangi Lugola kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Meja Jenerali Jacob Kingu kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Kailima Ramadhani kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Jaji Thomas Mihayo kuwa Kamishn

SALAMBA,KAGERE WAIPELEKA SIMBA ROBO FAINALI YA KOMBE LA KAGAME CUP 2018

Image
Washambuliaji wapya wa  klabu ya Simba wameisaidia timu hiyo kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya APR  ya Rwanda Mchezo wa Michuano ya Kagame inayoendelea jijini Dar Salaam kwenye viwanja vya Chamazi na Taifa. Katika mchezo huo uliokuwa na mashambulizi ya zamu kwa zamu, ulimalizika dakika 45 za kwanza bila timu yoyote kuona bao. Mara baada ya kuanza kwa kipindi cha pili, timu zote zilionesha kukamiana zikiwa na lengo la kucheka na nyavu ambapo mnamo dakika ya 66, Kinzingabo aliweza kuiandikia APR bao la kwanza. Ilichukua takribani dakika 6 baadaye Simba kuweza kusawazisha ambapo katika dakika ya 72, mshambuliaji aliyesajiliwa kutoka Lipuli ya Iringa, Adam Salama alifunga na kuufanya ubao wa matokeo kusomeka 1-1. Wakati mpira ukiwa katika dakika za nyongeza, straika hatari mpya, Meddie Kagere aliifungia Simba bao la pili na la ushindi kwa njia ya penati baada ya kiungo Said Ndemla kuangushwa katika eneo la hatari. Kwa Matokeo hayo Simba na Singida a