Makamu wa Rais aahidi Serikali kutatua changamoto ya barabara Mbeya


MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wakazi wa Mkoa wa Mbeya kwamba serikali imejipanga kutekeleza na kutatua changamoto muhimu za kimaendeleo, ikiwemo ya miundombinu ya barabara.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati akizungumza na mamia ya wananchi katika eneo la Mbalizi Wilayani Mbeya eneo linalotajwa kuongoza kwa matukio ya ajali za barabarani.

 Amesema, katika kulitekeleza hilo, tayari serikali imeshughulikia changamoto ya ujenzi wa barabara ya mchepuko ya kilomita 40 ambayo itasaidia kupunguza au kudhibiti ajali za barabarani zinazotokea kwenye barabara kuu ya Tanzania na Zambia (TAZAMA).

 “Mwaka juzi mlifanya kazi kubwa sana, tumekuja kuwahikikishia kwamba serikali itatekeleza yale yote tuliyo ahidi, nadhani spidi mnaiona,”amesema.

Mama Samia pia amewataka wananchi kuendelea kudumisha amani kwani ndio sialaha ya maendeleo na kuwasisitiza kuchaguai viongozi watakaoendana na kasi ya rais na waioendekeza tama wakati wa uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa.

Comments

Popular posts from this blog