JPM ATOA POLE KWA KIKWETE KUFIWA NA BABA MKEWE

Rais John Magufuli akilakiwa na rais mstaafu Jakaya Kikwete alipofika kutoa pole kwa kufiwa na baba mzazi wa mkewe Mama Salma Kikwete, marehemu Rashid Mkwachu, nyumbani kwa wafiwa Msasani jijini Dar es Salaam leo Julai 21, 2018.
Mke wa Rais Magufuli, Mama Janeth Magufuli, akilakiwa na Kikwete kwenye msiba huo.
Magufuli akimpa pole mke wa Kikwete,  Mama Salma Kikwete.
 Magufuli  na Kikwete wakati wa dua. 
…Dua ya familia kwa ajili ya marehemu.
Rais na mkewe wakiagana na wafiwa.
…Akiendelea kuagana na waliofika msibani.
Magufuli na mkewe wakisindikizwa. 
RAIS  John Magufuli na  mkewe Mama Janeth Magufuli, wamefika nyumbani kwa rais mstaafu, Jakaya Kikwete,   kutoa pole kwa kufiwa na baba mzazi wa mkewe Mama Salma Kikwete, marehemu Rashid Mkwachu, nyumbani Msasani jijini Dar es Salaam leo Julai 21, 2018.
Picha na IKULU

Comments

Popular posts from this blog