Jafo azitaka halmashauri kutoweka riba mikopo ya wajasiriamali


Waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa Selemani Jafo amezitaka halmashauri za miji na majiji kutoweka riba katika fedha za mikopo zinatolewa kwa ajili ya vikundi vya wajasiriamali hapa nchini.

Akizungumza wakati wa kukabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 950 zilizotolewa na jiji la Dodoma kwa wajasiliamali, Mheshimiwa Jafo amesema serikali ya awamu ya tano inalenga kuwawezesha watanzania hivyo haikubali wananchi kutozwa riba.

Akizungumza katika tukio hilo, naibu waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera,bunge,ajira kazi vijana na watu wenye ulemavu Mhe. Anthony Mavunde amesema jiji la Dodoma ni kati ya halmashauri chache nchini zilizoweza kutimiza sheria ya kuhakikisha linatoa mikopo kwa vikundi vya kina mama,vijana na watu wenye ulemavu ili Kuwawezesha kuondokana na umaskini.

Akielezea kuhusu fedha hizo, mkurugenzi wa jiji la Dodoma Bw.Godwin Kunambi amesema jiji la Dodoma limevuka malengo ya ukusanyaji wa mapato ya ndani kutoka bilioni 20 hadi bilioni 21 na kulifanya kuongoza kwa mapato katika  majiji yote hapa nchini.

Comments

Popular posts from this blog