HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI YAJIDHATITI KUIMARISHA MAWASILIANO NA WANANCHI
Kiongozi wa ujumbe kutoka Chama
cha maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari
MAELEZO Bi. Gaudensia Simwanza akisisistiza jambo kwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara Bi. Changwa
Mkwazu wakati wa ziara ya ujumbe huo katika halmashauri hiyo
uliolenga kuona utendaji kazi wa Maafisa Habari na Mawasiliano na namna
wanavyokabiliana na changamoto mbalimbali ili kuweza kuisemea Serikali
kimkakati.
Kiongozi wa ujumbe kutoka Chama
cha maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari
MAELEZO Bi. Gaudensia Simwanza akisisitiza jambo kwa Afisa Habari na
Mawasiliano wa Halmashuri ya Wilaya ya Masasi Bi mara baada ya ziara ya
ujumbe huo katika Halmashuri hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara Bi. Changwa Mkwazu akiwa kwenye picha
ya pamoja na sehemu ya ujumbe wa viongozi wa Chama cha maafisa Habari
na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari MAELEZO wakati
walipotembelea Halmashuri ya Wilaya hiyo ikiwa ni sehemu ya juhudi za
kuhamasisha Maafisa habari na Mawasiliano kutekeleza majukumu yao kwa
weledi na pia kuweka mikakati ya pamoja ya kutatua changamoto
zinazowakabili maafisa habari katika Sekretarieti za Mikoa na
Halmashuri.
Mwakilishi wa Idara ya Habari
MAELEZO Bw. Casmir Ndambalilo akiagana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara Bi. Changwa Mkwazu mara baada ya ziara ya
ujumbe kutoka Chama cha maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini
(TAGCO) na Idara ya Habari MAELEZO.
Na Frank Mvungi- MAELEZO
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya
Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara Bi. Changwa Mkwazu Amesema kuwa
Dhamira ya Halmashauri hiyo ni kuendelea kuimarisha Mawasiliano na
wananchi kuhusu miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na
Serikali.
Akizungumza na ujumbe wa Viongozi kutoka
chama cha maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya
Habari MAELEZO uliomtembelea Ofisini kwake Bi. Mkwazu amesema kuwa
Halmashuri hiyo inatambua umuhimu wa wananchi kupata taarifa za miradi
ya maendeleo kwa wakati kupitia vyombo vya habari.
“ Afisa Habari wetu anashiriki kikamilifu
katika jukumu hili la kuwajulisha wananchi kuhusu miradi ya maendeleo
inayoteklezwa na mikakati yetu ni kumuwezesha zaidi kadiri rasilimali
zitakavyopatikana kwa kumpatia vitendea kazi bora ili atekeleze jukumu
hili kwa ufanisi “ Alisisitiza Bi. Mkwazu
Akifafanua amesema kuwa mawasiliano ni
nyenzo muhimu katika kuwaletea wananchi maendeleo kwa kuwa wanapata
elimu kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo kilimo.
Aliongeza kuwa suala la mawasiliano katika
Halmashauri hiyo ni kipaumbele kwa kuwa ndiyo chachu ya maendeleo
katika Halmashauri hiyo.
Kwa upande wake Kiongozi wa Ujumbe huo Bi
Gaudensia Simwanza amesema kuwa ni wakati muafaka kwa maafisa habari na
mawasiliano Serikalini kuwa na mawasiliano ya kimkakati na kuangalia
namna bora ya kuwasiliana na wananchi kuhusu yale yanayoteklezwa na
Serikali katika maeneo yao.
“ Ni muhimu kwa afisa habari kuonesha umuhimu wa mawasiliano kwa kutekleza majukumu yake kwa weledi” alisisitiza Simwanza.
Ziara ya Viongozi wa chama cha Maafisa
Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari MAELEZO
inalenga kuimarisha utendaji wa Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini
katika Mikoa na Halmashuri hapa nchini.
Comments
Post a Comment