Mbelgiji Aanza Kukiunga Kikosi Upya

KOCHA Patrick Aussems raia wa Ubelgiji ameanza kutoa mafunzo ya mfumo anaotaka kuutumia katika msimu wa 2018/19 akiwa na Simba.


Simba imeweka kambi ka­tika mji mdogo wa Kartepe ambao uko mlimani kabisa, sehemu maalum kwa ajili ya kambi za timu.

Aussems ameanza kukinoa kikosi chache akiwafundisha mifumo na namna ya uchezaji katika masuala mbalimbali.
Kocha huyo amekuwa aki­waonyesha wachezaji wake namna ya kulinda lakini pia kushambulia kwa tahadhari.

Wakati Simba ilipotua hapa, kocha huyo alianza kutoa mafunzo ya kawaida, zaidi wachezaji wakioneka­na kupasha misuli kawaida.

Inaonekana ame­kuwa akiongeza mazoezi taratibu huku akichanganya na aina ya uche­zaji.

Makocha wengi huanza kufundisha mifumo baada ya timu zao kupata mazoezi ya kuto­sha. Lakini Mbelgiji huyo anaonekana kuwa tofauti ki­dogo akienda anachangan­ya mazoezi ya kawaida na mifumo, taratibu.

Comments

Popular posts from this blog