SALAMBA,KAGERE WAIPELEKA SIMBA ROBO FAINALI YA KOMBE LA KAGAME CUP 2018

Washambuliaji wapya wa  klabu ya Simba wameisaidia timu hiyo kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya APR  ya Rwanda Mchezo wa Michuano ya Kagame inayoendelea jijini Dar Salaam kwenye viwanja vya Chamazi na Taifa.
Katika mchezo huo uliokuwa na mashambulizi ya zamu kwa zamu, ulimalizika dakika 45 za kwanza bila timu yoyote kuona bao.
Mara baada ya kuanza kwa kipindi cha pili, timu zote zilionesha kukamiana zikiwa na lengo la kucheka na nyavu ambapo mnamo dakika ya 66, Kinzingabo aliweza kuiandikia APR bao la kwanza.
Ilichukua takribani dakika 6 baadaye Simba kuweza kusawazisha ambapo katika dakika ya 72, mshambuliaji aliyesajiliwa kutoka Lipuli ya Iringa, Adam Salama alifunga na kuufanya ubao wa matokeo kusomeka 1-1.
Wakati mpira ukiwa katika dakika za nyongeza, straika hatari mpya, Meddie Kagere aliifungia Simba bao la pili na la ushindi kwa njia ya penati baada ya kiungo Said Ndemla kuangushwa katika eneo la hatari.
Kwa Matokeo hayo Simba na Singida ambao walishinda mchezo wao wa mapema wa goli 1-0 moja kwa moja wanatinga hatua ya Robo Fainali wote wakiwa na Pointi 6 huku Simba akiwa kileleni kwa idadi kubwa ya mabao ya kufunga.

Comments

Popular posts from this blog