Naibu Meya, Madiwani CHADEMA Wajiuzulu Mbeya
IKIWA
ni saa chache baada ya uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) mkoani Mbeya kupendekeza kuwavua uanachama madiwani watatu wa
chama hicho mkoani humo kwa utovu wa nidhamu waliouonyesha, madiwani hao
wamejiuzulu nyadhifa zao hizo.
Madiwani hao na kata zao katika mabano ni Geofrey Kajigili (Sisimba), Newton Mwatuboje (Manga)na Hamphrey Ngalawa (Iwambi).
Madiwani hao wamejiuzulu leo Jumamosi Julai 21, 2018 baada ya
Mwenyekiti wa Chadema Mbeya Mjini, Obadia Mwaipalu, kutangaza uamuzi
huo katika mkutano wake na waandishi wa habari na kubainisha kuwa
vikao halali vya chama vilivyoketi mara kadhaa kujadili hatua stahiki
dhidi ya madiwani vimefikia uamuzi huo.
Amesema kutokana na utovu wa nidhamu, kukiuka katiba ya Chadema na
kukaidi utekelezaji wa maazimio ya uongozi, wamepeleka mapendekezo yao
kwa uongozi wa chama hicho Kanda ya Nyasa ili hatua zichukuliwe.
Aliyekuwa Naibu Meya na Diwani wa Kata ya Nsalaga Mjini Mbeya, Mchungaji David Ngogo (Chadema),
amesema wamefikia uamuzi huo akidai kupingana na viongozi wao baada ya
kudaiwa kumwalika Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson kuchangia ujenzi wa
Shule ya Sekondari Uyole.
Comments
Post a Comment