Madiwani wapita bila kupingwa Uchaguzi mdogo wa Udiwani- Mbulu.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mbulu ndugu
Hudson S. Kamoga akisoma taarifa ya maamuzi ya rufaa za Wagombea Udiwani katika
kata za Tumati na Hayderer.
Akiongea na vyombo vya habari hii leo ofisini kwake Msimamizi
wa Uchaguzi jimbo la Mbulu, ndugu Hudson
Stanley Kamoga amewatangaza Madiwani wawili wa kata ya Tumati ndugu Paulo Emanuel Axwesso (CCM) na ndugu Justine Sidamuy Masuja Hayderer(CCM),wamepita
bila kupingwa baada ya Wapinzani wao
kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kushindwa rufaa waliokata
Tume ya Taifa ya Uchaguzi dhidi ya Uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi.
Msimamizi msaidi wa jimbo la Mbulu ndugu Michael Faraay(wa kwanza kushoto) akiwa na mratibu wa uchaguzi ndugu Stedvant Kileo wakimsikiliza kwa makini msimamizi wa uchaguzi (hayupo pichani)wakati wakusoma maamuzi ya rufaa
Akitoa taarifa juu ya maamuzi ya rufaa hiyo
iliyotolewa na tume ya taifa ya Uchaguzi,msimamizi wa uchaguzi halmashauri ya
Wilaya ya Mbulu amesema amewaita wagombea kwa mujibu wa Sheria za Serikali za
Madiwani Sura namba 292 na Kanuni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa za mwaka
2015.
Mgombea Udiwani kwa kwa chama cha demekrasia na maendeleo ndugu Zakaria k. Hhaynihhi( kata ya Tumati) akipokea barua ya maamuzi ya Tume baada ya kupingwa rufaa yake.
Mbulu ni miongoni wa Majimbo ya Uchaguzi
yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa mujibu wa Sheria na Kanuni na
mnamo tarehe 14 ilitangazwa kuwa siku ya Uteuzi katika kata hizo mbili na
taratibu zilifanyika kama ilivyopangwa. Wanachama wanne toka vyama viwili vya
siasa walichukua fomu na kurejesha kwa mujibu wa sheria na kanuni za Uchaguzi.
Mshindi wa nafasi ya Udiwani kata ya Tumati ndugu Paulo E. Axwesso akipokea nakala ya barua toka tume ya Taifa ya Uchaguzi ikionesha majibu ya rufaa iliyompa ushindi wa kupita bila kupingwa.
Aidha Kamoga amesema
kuwa baada ya wagombea wote wanne kuteuliwa, Wagombea wawili wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo walipingwa kutokana
na sababu mbalimbali za ukiukaji wa ujazaji fomu namba 8 na msimamizi alichukua
hatua za kuwaondoa wagombea kwa mujibu wa sheria za uchaguzi.
Mshindi wa nafasi
ya Udiwani kata ya Hayderer ndugu Justine S. Masuja akipokea kwa furaha nakala ya
barua toka tume ya Taifa ya Uchaguzi ikionesha majibu ya rufaa
iliyompa ushindi wa kupita bila kupingwa.
Wagombea hao walikata rufaa tume ya taifa ya uchaguzi
na majibu hayo kurejeshwa ikionesha wagombea wote wawili kukataliwa, ikumbukwe
pamoja na kuondolewa kugombea nafasi hizo, mgombea wa Uchaguzi kwa kata ya
Hayderer kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo alishatangaza kujiondoa
kugombea nafasi hiyo kwa barua rasmi iliyo thibitishwa mbele ya mahakama.
Wagombea wa Uchaguzi wakiwa picha ya pamoja na wasimamizi wa uchaguzi hii leo mara baada ya kukabidhia majibu ya rufaa, kutoka kushoto ni mgombea udiwani CCM- Tuamati, Afisa uchaguzi, Msimamizi wa uchaguzi,mgombea udiwani kata ya Hayderer(CCM), Mratibu uchaguzi,na Mgombea udiwani Chadema- Hayderer
Uchaguzi mdogo wa Madiwani kwa kata mbili unafanyika
kufuatia waliokuwa Madiwani wa kata hizo kujivua nafasi zao za uwakilishi wa
Udiwani kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) na kuhamia Chama
cha Mapinduzi(CCM) ili kuunga juhudi za Serikali ya awamu ya tano ya Mhe. John
Pombe Magufuli na kuacha kata zao wazi.
Baada ya kuwatangaza rasmi Kamoga amasema utaratibu wa
kuwakabidhi vyeti vya ushindi wa Udiwani zinaendelea na watakabidhiwa mnamo
tarehe 12/08/2018 ambayo ilikuwa siku rasmi ya uchaguzi.
Comments
Post a Comment