Posts

Vilio vya Mastaa kwa Wanafunzi Waliokufa Arusha

Image
M AJONZI yamegubika nchi nzima kufuatia tukio la kihistoria la ajali ya basi lililosababisha vifo vya wanafunzi 33, walimu wawili na dereva iliyotokea Karatu mkoani Arusha. Taarifa zinasema kuwa basi hilo aina Toyota Coaster lililokuwa limebeba wanafunzi, walimu na dereva ambalo ni mali ya Shule ya Lucky Vincent liliacha njia na kutumbukia katika Mto Marera uliyopo kilometa 25 kutoka kwenye geti la Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro. Mbali na ajali hiyo kuwagusa wengi ndani na nje ya nchi, mastaa kutoka kwenye tasnia mbalimbali nchini wameibuka na kuzungumza na Wikenda, wakiweka wazi hisia zao za namna walivyoguswa na ajali hiyo. Wasikie; PROFESA JAY: Mungu azilaze roho za marehemu pema peponi. Kiukweli hili ni pigo kubwa sana kwa taifa letu, natoa pole sana kwa ndugu, jamaa wa marehemu na viongozi wote wa Mkoa wa Arusha kwa msiba huu mkubwa. Kwa mara nyingine tena kama taifa tunapoteza watoto wetu kwa idadi kubwa sana ambao wangeweza kuja kuwa hazina kubwa kwa

LIVE: Yanayojiri Arusha Kuaga Miili ya Wanafunzi Waliofariki kwa Ajali

Image
Makamu wa Rais wa Tanzania,  Samia Suluhu Hassan (kushoto) ,  akipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha (kulia), Mrisho Gambo,   baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)  atakapoongoza  wananchi wa Mkoa wa Arusha na Watanzania  kuaga miili ya wanafunzi, na waalimu waliofariki kwenye ajali ya gari juzi Karatu.  Tukio  hilo linafanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha. Jeshi la Wananchi na polisi wakiwa uwanjani katika taratibu za  kupokea miili ya wanafunzi waliofariki. Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoa salam za rambirambi kwa wafiwa na Watanzania wote. Viongozi wa dini,  watakaoendesha ibada  wamewasili mahali pa tukio ikiwa ni pamoja na viongozi wa serikali mkoani, akiwemo Waziri wa Fedha na Mipano Philip Mpango. Pia kuna walimu 30 kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Vikosi vya usalama vikiwa eneo litakalofanyika hafla ya kuwaaga marehemu. Uwanja wa Sheikh Amri Abaid umejaa watu  ambapo viko

Picha za wanafunzi 32 waliofafiki katikia ajali Arusha

Image
Juzi wanafunzi 32 wa darasa la saba, walimu 2 na dereva wa gari la shule ya msingi iitwayo Lucky Vicent ya Arusha walifariki dunia majira ya saa 3 asubuhi baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali katika eneo Rhotia Marera, Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha.

Gwajima ataka Bunge lisimame kuombeleza vifo vya wanafunzi 32

Image
Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephath Gwajima amemtaka Spika wa Bunge kuahirisha kikao cha Bunge siku ya kuaga miili ya watoto waliofariki kwa ajali ya jana. Amesema kama Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta aliamuru viongozi kusimama kwa kuwakumbuka watoto hao itakuwa ajabu kwa bunge kuendelea na vikao vya Bunge Amesema Spika akiahirisha Bunge kwa siku moja itatoa nafasi kwa wabunge hao kwenda Arusha ili kuomboleza pamoja.

NJAA YAMNYIMA SUBIRA MBUNGE WA CCM AFUNGUKA MBELE YA POLEPOLE

Image
Mbunge wa Mbulu Vijijini, Mh. Flatei G. Massay  Mbunge wa Mbulu Vijijini, Flatei Massay amemuomba Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole kufikisha kilio cha wananchi kwa Serikali ili wapatiwe chakula cha njaa. Massay amesema hayo leo baada ya Polepole kufanya ziara ya siku mbili wilayani Mbulu ya kukagua uhai wa chama,  kusikiliza kero na kuzungumza na Halmashauri Kuu ya CCM, Wilaya ya Mbulu. Amesema hivi sasa wananchi wana wakati mgumu kutokana na bei kubwa ya vyakula wanavyonunua kutokana na ukame uliotokea msimu uliopita hivyo Serikali iwapatie chakula cha bei nafuu. Amesema wananchi wa eneo hilo ni hodari kwa kulima mazao mbalimbali ya chakula na biashara, ila kutokana na ukame uliotokea msimu uliopita hivi sasa wanakabiliwa na upungufu wa chakula. “Kwa sababu chama ndiyo kinasimamia Serikali, kilio hiki cha wananchi tunakifikisha kwako ili tatizo lao limalizike, kwani wanataka chakula cha bei nafuu na siyo kile chakula cha bure,”

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Kuongoza Kuaga Wanafunzi Waliofariki Arusha Kesho

Image
  Makamu wa Rais, Samia Suluhu kesho saa mbili asubuhi ataongoza wakazi wa Arusha katika Uwanja wa Sheikh Abeid Karume kuaga miili ya wanafunzi waliofariki katika ajali ya gari Arusha ambapo serikali imegharamia sanda  na majeneza kwa wanafunzi wa shule Lucky Vincent waliopoteza maisha jana kwenye ajali. Akitoa taarifa hiyo leo Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro,  amesema taarifa za awali zinaonyesha tayari serikali imekwishalipia gharama za majeneza na sanda za kuhifadhia miili ya marehemu ambao kesho wanatarajiwa kufanyiwa ibada katika Uwanja wa heikh Amri Abeid. Mazingira ya shule hiyo. Aidha Lazaro amesema viongozi mbalimbali wakiwemo mawaziri na wabunge bado wanaendelea kukusanyika katika eneo la shule ya Lucky Vincent  kwa ajili ya kikao.

BREAKING: AJALI NYINGINE DUMILA MOROGORO YAACHA MASWALI

Image
Ikiwa bado watanzania tukiomboleza kutokana ajali ya jana mkoani A rusha iliyoondoka na wanafunzi 32, na kuacha majonzi kwetu na TAIFA ZIMA. Habari za hivi punde toka Morogoro Dumila Eneo la Kutoka mvomelo ukipita matuta ya mwanzo kabla hujafika Makunganya   kuna Gari ya abiria aina ya Eicher imegongwa na lori na inariportiwa kuwa hali mbaya sana.. Bado hakuna ripot ya kifo wala majeruhi @afande Anna Job kajulishwa   Tumwombe  Mungu atupiganie Tarifa kamili baada ya muda mfupi ujao.. Tayari AKISI TV iko njiani kuelekea eneo la tukio kukupa habari zaidi. Pia Tunarajia kupata taarifa kamili kutoka  jeshi la polisi.

HUMPHFEREY POLEPOLE AFUNGUKA HAYA KUHUSU MANGE KIMAMBI

Image
Baada ya Pole pole kuandika hiyo post hapo juu ikiwa imemtaja Mange Kimambi, Mange akaamua kumtolea  uvivu kama ifuatavyo : . #Regrann from #mangekimambi_ - : "PolePole Tokea uwe katibu uenezi wa CCM ile brain ya kuongea mapoint mazito mazito imetoweka kabisa Yani. Hivi PolePole unakumbuka ulivyokuwaga unawa-inspire watanzania kwa jinsi ulivyokuwaga unaongea mapoint mazitoooooo. Siku hizi unaongea kama Bashite. Huna point, unajibu vitu bila busara, unajibu mambo kiwepesi wepesi... Hivi Kweli Polepole kweli kati ya yote niliyosema point kubwaaaaa uliyoiona wewe ni Mimi kusema Kinana ameacha kufanya kazi za Chama???? And it's 100% true kinana amegoma kufanya mambo ya chama mpaka Baba Bashite A.k.a mwenyekiti wa CCM akamueleze why alimuitia TISS. Kinana alishikiliwa Na TISS nyumbani kwake for over 2 weeks... Kwa issue ya Kinana alivyokaaa vibaya kwa Sasa ilibidi nyinyi kama chama muwatoe hofu wana CCM Na watz kwa ujumla kwa kuweka wazi data kuw

BREAKING NEWS: WANAFUNZI 32 WAFARIKI KWA AJALI KARATU

Image
Saturday, May 06, 2017 Arusha. Wanafunzi zaidi ya 20 wanahofiwa kupoteza maisha  katika ajali ya basi iliyotokea wilayani Karatu leo asubuhi. Habahari zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa basi hilo lilikuwa likitokea Arusha Mjini kuelekea katika Mbuga za wanyama.  Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Therezia Mahongo amethibitisha tukio hilo. Tutaendelea kukujuza zaidi kuhusu taarifa hii.

TANESCO Wakata Umeme Kambi ya JWTZ , Magereza na Polisi.......Ofisi ya Mkuu wa Mkoa nayo Nusura Ikatiwe

Image
Agizo la Rais Dk. John Magufuli la kulitaka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuzikatia umeme taasisi za Serikali zinazodaiwa jumla ya Sh bilioni 8.6 limeanza kufanya kazi mkoani  Arusha. Ofisi zilizoanza kuonja machungu ya kukosa umeme kuanzia jana hadi zitakapolipa madeni ni Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Oljoro, Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jeshi la Magereza, Hospitali za Serikali na Taasisi za Maji. Nyingine zilizokatiwa umeme ni Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha ikiwamo Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha na Kituo Kikuu cha Polisi cha Arusha. Wakati ofisi hizo zikikosa umeme, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ilinusurika baada ya kuanza kulipia deni lake la Sh milioni sita 6 kwa awamu. Akithibitisha kufanyika kwa operesheni hiyo iliyotajwa kuwa endelevu kwa ofisi hizo mkoa mzima, Ofisa Uhusiano wa Tanesco mkoani hapa, Saidy Mremi, alisema inalenga kukusanya madeni yote ya miaka iliyopita. “Tunatekeleza agizo la R

Sugu Amvaa ‘Bashite’ Bungeni

Image
MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amemshambulia Bashite huku akisema kuwa mtu huyo alipaswa awe mahakamani na sio ofisini kwa madai kuwa amefoji vyeti vya elimu ya sekondari jambo ambalo ni kosa kisheria. Hayo ameyasema leo Bungeni Mjini Dodoma wakati akichangia hoja kuhusu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Aidha Sugu amemtaka Rapa ROMA Mkatoliki ajitokeze hadharani aeleze wazi kuhusu alivyotekwa na nani alihusika ili jamii ielewe na mamlaka husika iweze kuchukua hatua ikiwemo kuwabaini waliyotekeleza tukio hilo ambalo si la kibinadamu. Sugu aliwageukia wasanii wa Filamu Bongo ambao hivi karibuni waliandama wakipinga uingizwaji holela wa filamu za nje ambazo wanadai zinaporomosha soko la filamu za ndani. Sugu amewataka wasanii hao waache kutumika kisiasa na badala yake wafate misingi ya kazi zao.

Zitto: Tumethibitisha Kampuni ya Boeing wametuuzia ndege ya mwaka 2009

Image
Kwa Mujibu wa Zitto Kabwe ameandika Taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa Facebook "Tumeshathibitisha bila mashaka kuwa Kampuni ya Boeing wametuuzia ndege ya mwaka 2009 Kwa bei ya mwaka 2017. Kazi Kwa Watanzania ni kuishinikiza Serikali iseme imelipa kiasi gani? Nukuu kutoka mtaalamu wa ndege na picha ya uthibitisho wa terrible teen hiyo. Ninasikitika Sana kuwa Rais mwenyewe na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha ndio walikutana na watu wa Boeing kuhusu dili hili. Ina maana Boeing wamemdanganya Rais wetu. Sio sawa hata kidogo "Terrible Teen" LN19 iliondolewa kutoka was 45-12 na itakabidhiwa Air Tanzania itakapokuwa imemalizika mwishoni mwa Mwaka huu "

UMUHIMU MKUBWA WA KOMAMANGA (POMEGRANATE) JUU YA MARADHI YA KANSA

Image
Uchunguzi mpya umeonyesha kwamba, katika tunda la komamanga kuna kemikali zinazozuia kansa ya matiti isitambae mwilini. Uchunguzi huo uliochapishwa katika jarada la Utafiti la kuzuia Kansa umeonyesha kwamba, kemikali ziitwazo ellegitannins zinazopatikana kwa wingi kwenye komamanga, zinaweza kuzuia kimeng’enyo (enzyme) aina ya aromatase, suala ambalo huzuia kukua kwa Homoni ya estrogen inayopatikana katika kansa ya matiti. Shiuan Chen Kiongozi wa uchunguzi huo amesema kwamba, kemikali hizo hupunguza uzalishwaji wa estrogen, na kusaidia kuzuia seli za kansa ya matiti zisizaliane mwilini, pamoja na tezi la ugonjwa huo lisikue. Aromatase, ni kimeng’enyo ambacho hugeuza Homoni ya androgen kuwa estrogen, na kushambulia kimeng’enyo hicho ndio lengo kuu la dawa za kupambana na kansa za matiti zinazosababishwa na homoni ya etrogen. Huko nyuma pia uchunguzi ulionyesha kwamba tunda la komamanga lina faida kubwa kiafya hasa kwa kuwa na  anti Oxidant nyingi na vitamin mbalim

Bunge lafuta maneno kwenye hotuba ya Sugu kabla ya kusomwa

Image
Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu ameagiza Hotuba ya Kambi ya Upinzani kuhusu Bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ihaririwe na kufuta maneno yote katika kurasa 17. Zungu ametoa uamuzi huo leo asubuhi baada ya kipindi cha maswali na majibu, hata kabla ya bajeti yenyewe kuwakilishwa na Waziri Dk Harrison Mwakyembe. Zungu amesema amezipihitia hotuba zote na kubaini kuwa ile ya upinzani itakayowalishwa na Joseph Mbilinyi 'Sugu' ina masuala yaliyopo mahakamani ambayo yamekwishazuliwa katika bajeti zilizotangulia. Amesema maneno yenye mwelekeo huo yakisomwa atachukua hatua.

Faida ya majani ya mparachichi

Image
Siku chache zilizopita tuliangazia macho katika kuona faida za kula parachichi, ni amani yangu kwamba ulijifunza jambo kubwa sana, hivyo naomba siku ya leo naomba tuangalie faida majani ya mmea wa parachichi katika mwili wa mwadamu. Zifuatazo ni faida ya majani ya mparachichi. Majani ya parachichi humsaidia mwanamke ambaye hupata maumivu wakati wa hedhi. Unachotakiwa kufanya ni; Chukua majani kiasi ya mparachichi, kisha yachemshe kwenye maji lita moja, ukijiridhisha yamekwisha chemka epua kisha yaache yapoe, kisha anza kunywa maji hayo kiasi cha nusu kikombe cha chai, kunywa muda wa asubuhi na jioni kwa muda wa wiki moja utaona mabadiliko. 1. Majani ya mparachichi  husaidia sana kuongeza kiwango cha maziwa kwa kinamama. 2. Unachotakiwa kufanya ni Tatatafuna jani moja la parachichi kila siku, lakini hakikisha jani unalotafuna liwe katika hali ya safi na umeliosha vizuri. 3. Pia majani haya ya mparachichi ni msaada sana katika kutibu majeraha, il

Njia 10 muhimu ukitaka kuondoa sumu mwilini mwako

Image
Mwili wa binadamu unaweza kupatwa na sumu au takataka zisizohitajika na kwa namna mbili; kupitia mazingira tunayoishi kama vile viwanda, migodi na maeneo mengine hatarishi ama kupitia vyakula na vinywaji ambavyo tunatumia kila siku. Sumu au takamwili,zinaweza kuingia mwilini kupitia dawa mbalimbali hasa za kizungu tunazotumia kujitibu magonjwa mbalimbali. Mwili huzalisha sumu au takamwili (free radicals) kila mara kunapofanyika mmeng’enyo wa chakula mwilini mwako. Hizi ni ishara zinazoweza kuashiria mwili wako umeingiwa na takamwili: -Uchovu sugu -Maumivu ya maungio -Msongamano puani -Kuumwa kichwa kila mara -Tumbo kujaa gesi -Kufunga choo au kupata choo kigumu -Kukosa utulivu -Matatizo mbalimbali ya ngozi ikiwemo chunusi -Pumzi mbaya -Mzunguko wa hedhi usio sawa -Kuishiwa nguvu -Kushindwa kupungua uzito -Kupenda kula k

Watumishi wa zahanati mbili wote feki"

Image
Mbunge wa Mchinga (CUF), Hamidu Bobali amefunguka na kusema zahanati mbili katika halimashauri yao zimefungwa kutokana na watumishi wake wote kukutwa na vyeti feki, jambo ambalo linapelekea wananchi katika kata hizo kukosa huduma.  Mbunge wa Mchinga (CUF), Hamidu Bobali. Hamidu Bobali alisema hayo jana bungeni na kusema sakata la vyeti feki limeleta athari katika halimashauri yao "Hili suala la vyeti feki Mh. Mwenyekiti limeleta athari kubwa sana katika halimashauri yetu, hivi hapa napoongea kuna zahanati mbili zote zimefungwa kutokana na ukweli kwamba watumishi wake wote wameonekana na vyeti feki" alisema Hamidu Bobali  Mpaka sasa sakata la vyeti feki limeanza kuleta athari katika baadhi ya maeneo baada ya watumishi wengine kuamua kujiondoa wenyewe makazini kama amri ya Rais Magufuli ilivyoagiza kuwa wajiondoe wenyewe na kuachia nafasi hizo.