NJAA YAMNYIMA SUBIRA MBUNGE WA CCM AFUNGUKA MBELE YA POLEPOLE
Mbunge wa Mbulu Vijijini, Mh. Flatei G. Massay |
Mbunge wa Mbulu Vijijini, Flatei Massay amemuomba Katibu wa Itikadi na
Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole kufikisha kilio cha wananchi kwa
Serikali ili wapatiwe chakula cha njaa.
Massay amesema hayo leo baada ya Polepole kufanya ziara ya siku mbili
wilayani Mbulu ya kukagua uhai wa chama, kusikiliza kero na kuzungumza
na Halmashauri Kuu ya CCM, Wilaya ya Mbulu.
Amesema hivi sasa wananchi wana wakati mgumu kutokana na bei kubwa ya
vyakula wanavyonunua kutokana na ukame uliotokea msimu uliopita hivyo
Serikali iwapatie chakula cha bei nafuu.
Amesema wananchi wa eneo hilo ni hodari kwa kulima mazao mbalimbali ya
chakula na biashara, ila kutokana na ukame uliotokea msimu uliopita hivi
sasa wanakabiliwa na upungufu wa chakula.
“Kwa sababu chama ndiyo kinasimamia Serikali, kilio hiki cha wananchi
tunakifikisha kwako ili tatizo lao limalizike, kwani wanataka chakula
cha bei nafuu na siyo kile chakula cha bure,” amesema Massay.
CHANZO: MWANANCHI
Comments
Post a Comment