Faida ya majani ya mparachichi
Siku chache zilizopita tuliangazia macho katika kuona faida za kula
parachichi, ni amani yangu kwamba ulijifunza jambo kubwa sana, hivyo
naomba siku ya leo naomba tuangalie faida majani ya mmea wa parachichi
katika mwili wa mwadamu.
Zifuatazo ni faida ya majani ya mparachichi.
Majani ya parachichi humsaidia mwanamke ambaye hupata maumivu wakati wa hedhi.
Unachotakiwa kufanya ni;
Chukua majani kiasi ya mparachichi, kisha yachemshe kwenye maji lita
moja, ukijiridhisha yamekwisha chemka epua kisha yaache yapoe, kisha
anza kunywa maji hayo kiasi cha nusu kikombe cha chai, kunywa muda wa
asubuhi na jioni kwa muda wa wiki moja utaona mabadiliko.
1. Majani ya mparachichi husaidia sana kuongeza kiwango cha maziwa kwa kinamama.
2. Unachotakiwa kufanya ni
Tatatafuna jani moja la parachichi kila siku, lakini hakikisha jani unalotafuna liwe katika hali ya safi na umeliosha vizuri.
Tatatafuna jani moja la parachichi kila siku, lakini hakikisha jani unalotafuna liwe katika hali ya safi na umeliosha vizuri.
3. Pia majani haya ya mparachichi ni msaada sana katika kutibu majeraha,
ili kufanikiwa katika hili unapaswa kusaga majani hayo kisha weka
kwenye sehemu yenye jeraha na utaona mafanikio,
4.Majani ya mparachichi pia husaidia kuimarisha kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali.
Hizo ni faida chache kati ya nyingi ambazo hutibika na majani ya parachichi.
Comments
Post a Comment