LIVE: Yanayojiri Arusha Kuaga Miili ya Wanafunzi Waliofariki kwa Ajali


Makamu wa Rais wa Tanzania,  Samia Suluhu Hassan (kushoto) ,  akipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha (kulia), Mrisho Gambo,   baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)  atakapoongoza  wananchi wa Mkoa wa Arusha na Watanzania  kuaga miili ya wanafunzi, na waalimu waliofariki kwenye ajali ya gari juzi Karatu.  Tukio  hilo linafanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.

Jeshi la Wananchi na polisi wakiwa uwanjani katika taratibu za  kupokea miili ya wanafunzi waliofariki.


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoa salam za rambirambi kwa wafiwa na Watanzania wote.

Viongozi wa dini,  watakaoendesha ibada  wamewasili mahali pa tukio ikiwa ni pamoja na viongozi wa serikali mkoani, akiwemo Waziri wa Fedha na Mipano Philip Mpango.


Pia kuna walimu 30 kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.


Vikosi vya usalama vikiwa eneo litakalofanyika hafla ya kuwaaga marehemu.
Uwanja wa Sheikh Amri Abaid umejaa watu  ambapo vikosi vya usalama na Msalaba Mwekundu vipo sehemu zote za uwanja ambapo pia alipoingia uwanjani aliyekuwa waziri mkuu, Edward Lowassa umati wa watu ulimpigia makofi licha ya kuwepo masikitiko makubwa ya msiba.

Baadhi ya watu waliofika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Tayari miili ya wanafunzi 32, walimu 2, na dereva 1, waliofariki kwa ajali ya gari Karatu imewasili katika Viwanja vya Shehe Amri Abeid Karume Arusha kwa ajili ya kuagwa.
Miili yote ya marehemu imeshashushwa kwenye gari, na sasa utaratibu wa kuanza kuaga ndio unasubiliwa.

Comments

Popular posts from this blog