TANESCO Wakata Umeme Kambi ya JWTZ , Magereza na Polisi.......Ofisi ya Mkuu wa Mkoa nayo Nusura Ikatiwe
Agizo
la Rais Dk. John Magufuli la kulitaka Shirika la Umeme Tanzania
(Tanesco) kuzikatia umeme taasisi za Serikali zinazodaiwa jumla ya Sh
bilioni 8.6 limeanza kufanya kazi mkoani Arusha.
Ofisi
zilizoanza kuonja machungu ya kukosa umeme kuanzia jana hadi
zitakapolipa madeni ni Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Oljoro,
Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jeshi la Magereza, Hospitali za
Serikali na Taasisi za Maji.
Nyingine
zilizokatiwa umeme ni Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha ikiwamo Ofisi ya
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha na Kituo Kikuu cha Polisi cha Arusha.
Wakati
ofisi hizo zikikosa umeme, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ilinusurika
baada ya kuanza kulipia deni lake la Sh milioni sita 6 kwa awamu.
Akithibitisha
kufanyika kwa operesheni hiyo iliyotajwa kuwa endelevu kwa ofisi hizo
mkoa mzima, Ofisa Uhusiano wa Tanesco mkoani hapa, Saidy Mremi, alisema
inalenga kukusanya madeni yote ya miaka iliyopita.
“Tunatekeleza
agizo la Rais Magufuli, hatutaziacha salama ofisi zote zinazodaiwa.
Tunafanya hivi ili kuiwezesha ijiendeshe pamoja na kutoa huduma bora kwa
wateja wetu,” alisema.
Mremi
alisema operesheni hiyo iliyoongozwa na Meneja wa Tanesco Kanda, Stella
Hizza na Meneja wa Mkoa, Gasper Msigwa, ilikata umeme katika vituo vya
polisi vilivyopo mjini hapa.
Pia
alivitaja vituo vya polisi vingine vilivyokatiwa umeme kuwa ni vituo
vya Polisi vya Unga Limited, Ngarenaro, Sakina na Ngaramtoni.
“Vituo
vingine ni Sekei, Fire, Kijenge, Chekereni, Olorien na Mbauda. Na vituo
vingine vya jeshi likiwamo Duka la Jeshi lililoko JKT Oljoro na Njiro
Nane Nane. Hii ni operesheni endelevu itakayowezesha shirika
kujiendesha,” alisema.
Akielezezea
kuhusu Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, alisema ofisi hiyo imeweza
kutoa ushirikiano wa hali juu katika kulipia deni lao.
“Hawa
tulikuwa tunawadai shilingi milioni sita hadi sasa wameweza kulipia
zaidi ya asilimia 80 ya deni lao, wametupa ushirikiano wa hali ya juu na
wameahidi kuendelea kulipa ili kumaliza deni lao,” alisema.
Mremi alisema madeni hayo ni ya miaka ya nyuma na yalitokana na taasisisi hizo kuyalimbikiza kisha yakahamia mwaka mwingine.
Aliyataja
madeni ambayo taasisi hizo zinadaiwa (kwenye mabano) kuwa JWTZ (Sh
milioni 538), JKT (Sh milioni 57), Jeshi la Polisi (Sh milioni 490),
Jeshi la Magereza (Sh Milioni 271), hospitali tofauti za Serikali (Sh
milioni 58) na taasisi nyingine ikiwamo za maji (Sh milioni 106).
“Taasisi
hizi za Serikali kwa ujumla wake zinadaiwa shilingi bilioni 8.6 sawa na
asilimia 28 na asilimia 72 inayobakia ipo kwa taasisi, mashirika na
watu binafsi,” alisema.
Kabla
ya kufikia hatua hiyo ya kuzikatia umeme taasisi hizo pamoja na wateja
wengine, alisema huwa wanatoa notisi kwa wateja wake ikiwamo kutangaza
matangazo katika vyombo vya habari.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Comments
Post a Comment