Sugu Amvaa ‘Bashite’ Bungeni
MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amemshambulia Bashite
huku akisema kuwa mtu huyo alipaswa awe mahakamani na sio ofisini kwa
madai kuwa amefoji vyeti vya elimu ya sekondari jambo ambalo ni kosa
kisheria.
Hayo ameyasema leo Bungeni Mjini Dodoma wakati akichangia hoja kuhusu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Aidha Sugu amemtaka Rapa ROMA Mkatoliki ajitokeze hadharani aeleze
wazi kuhusu alivyotekwa na nani alihusika ili jamii ielewe na mamlaka
husika iweze kuchukua hatua ikiwemo kuwabaini waliyotekeleza tukio hilo
ambalo si la kibinadamu.
Sugu aliwageukia wasanii wa Filamu Bongo ambao hivi karibuni
waliandama wakipinga uingizwaji holela wa filamu za nje ambazo wanadai
zinaporomosha soko la filamu za ndani. Sugu amewataka wasanii hao waache
kutumika kisiasa na badala yake wafate misingi ya kazi zao.
Comments
Post a Comment