Watumishi wa zahanati mbili wote feki"

Mbunge wa Mchinga (CUF), Hamidu Bobali amefunguka na kusema zahanati mbili katika halimashauri yao zimefungwa kutokana na watumishi wake wote kukutwa na vyeti feki, jambo ambalo linapelekea wananchi katika kata hizo kukosa huduma. 
Mbunge wa Mchinga (CUF), Hamidu Bobali.
Hamidu Bobali alisema hayo jana bungeni na kusema sakata la vyeti feki limeleta athari katika halimashauri yao
"Hili suala la vyeti feki Mh. Mwenyekiti limeleta athari kubwa sana katika halimashauri yetu, hivi hapa napoongea kuna zahanati mbili zote zimefungwa kutokana na ukweli kwamba watumishi wake wote wameonekana na vyeti feki" alisema Hamidu Bobali 
Mpaka sasa sakata la vyeti feki limeanza kuleta athari katika baadhi ya maeneo baada ya watumishi wengine kuamua kujiondoa wenyewe makazini kama amri ya Rais Magufuli ilivyoagiza kuwa wajiondoe wenyewe na kuachia nafasi hizo. 

Comments

Popular posts from this blog