TANESCO Wakata Umeme Kambi ya JWTZ , Magereza na Polisi.......Ofisi ya Mkuu wa Mkoa nayo Nusura Ikatiwe
Agizo la Rais Dk. John Magufuli la kulitaka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuzikatia umeme taasisi za Serikali zinazodaiwa jumla ya Sh bilioni 8.6 limeanza kufanya kazi mkoani Arusha. Ofisi zilizoanza kuonja machungu ya kukosa umeme kuanzia jana hadi zitakapolipa madeni ni Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Oljoro, Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jeshi la Magereza, Hospitali za Serikali na Taasisi za Maji. Nyingine zilizokatiwa umeme ni Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha ikiwamo Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha na Kituo Kikuu cha Polisi cha Arusha. Wakati ofisi hizo zikikosa umeme, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ilinusurika baada ya kuanza kulipia deni lake la Sh milioni sita 6 kwa awamu. Akithibitisha kufanyika kwa operesheni hiyo iliyotajwa kuwa endelevu kwa ofisi hizo mkoa mzima, Ofisa Uhusiano wa Tanesco mkoani hapa, Saidy Mremi, alisema inalenga kukusanya madeni yote ya miaka iliyopita. “Tunatekeleza agizo ...