Faida za Mchaichai kiafya

Faida za mchachai zipo nyingi sana wengi wetu hudhani mchaichai ni kuongo cha kuweka kwenye chai pekee, au ni dawa kwa ajili ya kuua mbu pekee, ila mchaichai huwa na faida lukuki zaidi ya hizo tu. Naomba uweze kusoma makala haya ili uone faida nyinginezo za mchaichai.

Zifuatazo ni faida za kutumia mchaichai kiafya.

1. Mchaichai ni kinga dhidi ya saratani.
Tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa kwenye kila gram 100 ya mchaichai, kuna viondosha
sumu ambavyo vina uwezo wa kuukinda mwili dhidi ya ugonjwa wa saratani. Mwaka 2006, timu ya watafiti kutoka Chuo kikuu cha Gurion, Israel waligundua mchaichai un uwezo wa kuua seli zinaweza kusababisha saratani.

2. Hutibu magonjwa ya kuhara.
Husaidia umeng’enyaji wa chakula Chai ya mchaichai hurahisisha utaratibu wa mmeng’enyo wa chakula na pia hutibu magonjwa ya kuhara na maumivu ya tumbo ikiwamo kujaa gesi.

Hurahisisha utaratibu wa kuondoa uchafu mwilini Katika matibabu, unatibu magonjwa mengi ikiwemo kushusha joto, hasa kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na malaria kali.

3. Husaidia kusafisha figo na mkojo.
Mchaichai pia una kazi ya kusafisha figo ambayo kazi yake kubwa ni kusafisha damu mwilini, kuondoa mafuta mabaya mwilini ambayo mengi yanatengenezwa na kemikali kiwandani na hivyo mwili kushindwa kuziondoa na baadaye kusasababisha magonjwa mbalimbali ikiwemo saratani.

Figo inapokuwa safi na imara, hata kazi nyingine kama kusafisha mkojo zinafanyika kirahisi kwani mkojo unapozidi kuwa mchafu mtu hujikuta akivimba mwili na wakati mwingine kufikia hata hatua ya kupoteza maisha.

4. Hupunguza maumivu wakati wa hedhi.
Mchaichai pia huwasaidia kina mama ambao wanaumwa na tumbo kipindi cha hedhi, ambao wengi wao huchukulia kama chango.

“Unapokunywa mchaichai, unawezesha kusafisha mirija ya uzazi na hivyo kuwezesha damu kupita kwa urahisi,”

5. Mchaichai hutibu vidonda vya tumbo na kupunguza kiwango cha gesi tumboni.
Hata hivyo kwa wagonjwa wanaosumbuliwa hasa na vidonda vya tumbo, mchaichai husaidia kuondoa gesi ambazo huwapata mara kwa mara.

Unachotakiwa kufanya ni ;
Kuendelea kutumia chai ambayo imepikwa kwa majani ya mchaichai mara kwa mara.

Comments

Popular posts from this blog