MFAHAMU JOHN STEPHEN ,MTANZANIA MAARUFU ULIMWENGUNI KULIKO HAPA TANZANIA


John Steven Akhwari ni mwanariadha mstaafu. Alizaliwa mwaka 1938 kule Mbulu- Mkoani Manyara. Aliiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Olimpic mwaka 1968 nchini Mexico, katika mashindano ya riadha ya kilomita 42. Washiriki walikuwa 75, lakini waliomaliza shindano ni 57 pekee, huku John Steven Akhwari akimaliza wa mwisho kabisa.
Kwa nini alimaliza wa mwisho? 
Baada ya mbio kuanza, walipofika kilomita ya 19, mshiriki mojawapo alimparamia, kumsukuma na kuanguka vibaya mno. Aliumia begani, na goti la mguu wa kulia lilitenguka. Gari la huduma ya kwanza lilimfikia na kumpa matibabu, akaweza kusimama tena na kuendelea na riadha.Umaarufu wake duniani. Watu waliomhudumia walimlazimisha kuaihirisha shindano na apande kwenye gari lakini alikataa katakata. Aliendelea na riadha huku akichechemea. Alifanikiwa kumaliza kilomita zote 42, jioni ya saa 1 kwa saa za Mexico. Watu wachache waliokuwa wamebakia uwanjani walimshangilia sana.
Mwishoni kabisa, waandishi wa habari walimuuliza, Kwa nini aliendela kukimbia ili hali ameumia kiasi hicho? Aliwaambia Nchi yangu Tanzania haikunituma maili 5000 kuja Mexico kuanza hili shindano bali walinituma kumaliza shindano.
Katika mashindano ya Olimpic na mpaka hivi leo Bwana John Stephen Akhwari anatambulika kama 'The Greatest Last- Place Finish Ever'. Japo hakushinda tuzo yoyote lakini ameonyesha uvumilivu, ujasiri na wenzetu wamekuwa wakimtumia kufundishia watoto na vijana wao kwamba they must struggle to finish the race, not just to start it.
Kwa bahati mbaya sana, watanzania walio wengi hawamjui. Huyu ni mfano wa kuigwa, ilistahili kauli yake hiyo ingekuwa nukuu muhimu kwa vijana wetu.

Comments

Popular posts from this blog