Faida za kutumia juisi ya miwa katika kuimarisha afya zetu

Bila shaka unaifahamu juisi ya miwa, watu wengi tumekuwa tunakunywa na wengine tukiwa tunaibeza pia, hii ni kwasababu tumekuwa hatujui faida zitokanazo na unywaji wa huisi hiyo. Leo nataka nikupashe japo kwa uchacje faida za kunywa juisi ya miwa katika afya zetu.

Kunafaida nyingi za juisi ya miwa. Baadhi ya faida hizo ni kama zifuatazo;

1. Juisi ya miwa inauwezo mkubwa wa kuipatia miili nguvu kwa haraka na kukata kiu ya maji. 
Hii ni kwa sababu juisi ya miwa ina sukari "sucrose" ambayo kazi yake kuu ni kutengeneza nguvu mwilini. Kwahiyo wakati mwingine ukiwa na nguvu au uchovu, badala ya kunywa vinywaji vya viwandani tafuta juisi ya miwa.

2.  Husaidia figo kufanya kazi vizuri.
Juisi ya miwa inasaidia kuongeza kiwango cha protein mwilini na ku-imarisha ufanyaji kazi wa figo.
Juisi a miwa iliyochanganywa na maji ya Nazi husaidia kupunguza maumivu hasa yanayosababishwa  na mawe yaliyopo kwenye figo.

3. Hupunguza uwezrkano wa kupata ugonjwa wa kansa.
Juisi ya miwa ina kiwango kikubwa cha madini ya calcium, magnesium, potassium, chuma n manganese. Madini haya yana uasili wa ualkali ambao husaidia kupunguza uwezekano wa kupata kansa kama vile kansa ya Tezi dume "Prostate cancer" na kansa ya maziwa "Breast Canser"

4. Huepusha magonjwa ya ini.
Juisi ya miwa husaidia kulinda maini yasipate maambukizi. Hii ndo maana Madaktari hushauri matumizi ya juisi ya miwa kwa wingi.

5.Huzuia meno kuoza.
Uchunguzi unaonyesha juisi ya miwa husaidia kuzuia meo kuoza na matatizo ya kupumua kutokana na kuwa na kiasi kikubwa cha madini. Kwa hyo kama unafikiria kwenda kwa daltari kung'arisha meno yako, kunywa juisi ya miwa mara kwa mara.

6. Husaidia kulinda ngozi dhidi ya mogonjwa ya ngozi.
Juisi ya miwa husaidia katika kupambana na mabaka mabaka na kung'arisha ngozi. Juisi ya miwa huweza kutumika kama " face mask na scrub" kwa kuipaka kwenye ngozi na hivyo kusaidia katika kuing'arisha na kuiimarisha.

Comments

Popular posts from this blog