Dk Mwakyembe: Televisheni, Redio kusoma vichwa vya habari tu kwenye magazeti kuanzia kesho


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe  

Mwanza.Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amezitaka Televisheni na Redio kuanzia kesho kusoma vichwa vya habari vya magazeti tu ili kuwavutia wasomaji kununua magazeti kwa habari kamili.

Dk Mwakyembe amesema hayo leo jijini Mwanza katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari nchini ambapo pia amesema ataendelea kutetea na kulinda haki za waandishi wa habari huku akiwahakikishia ulinzi waandishi wa habari za uchunguzi.

Pamoja na mambo mengine Dk Mwakyembe amehakikisha kuwepo kwa ushirikiano wa kutosha kwa wamiliki wa vyombo vya habari  na kwamba ameagiza idara ya mawasiliano kutengeneza mawasiliano ya kudumu na wawe wanakutana angalau mara moja kwa mwezi kujadili udhaifu unaoweza kujitokeza na kuchukua hatua lengo ni kuwekana  sawa.

Comments

Popular posts from this blog