Posts

TAARIFA YA UTEUZI WA WAGOMBEA WA UJUMBE WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI

Image
1.     Tarehe 17 Machi, 2017 nilitoa Tangazo kwenye Gazeti la Serikali Namba 376 kuhusu Siku ya uteuzi na Siku ya Uchaguzi. Katika Tangazo hilo, nilipanga Siku ya tarehe 30 Machi, 2017, saa Kumi (10.00) Jioni kuwa Siku ya Uteuzi wa Wagombea na pia siku ya tarehe 04 Aprili, 2017 saa Tano (5.00) Asubuhi kuwa Siku ya Uchaguzi wa Wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki. 2.     Aidha, natoa shukrani zangu za dhati kwa wadau wote hususan Vyama vyote vya siasa nchini kwa ushirikiano mzuri nilioupata kutoka kwao katika zoezi zima la mchakato wa uteuzi wa wagombea. 3.     Vile vile, navipongeza na kuvishukuru vyama vyote vya siasa vyenye haki ya kushiriki uchaguzi kwa kuendesha mchakato wa uteuzi wa wagombea kwa uwazi na demokrasia kubwa. 4.     Pia navishukuru vyombo vya habari na wanahabari wote kwa ujumla kwa kuhabarisha umma kuhusu mchakato huu muhimu kwa Bunge na Taifa kwa ujumla. 5.     Kipekee nawashukuru na kuwapongeza wananchi wote waliojitokeza kupi

BREAKING NEWS : RAIS MAGUFULI AMTEUA PROF KITILA MKUMBO KUWA KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAJI NA UMWAGILIAJI

Image

Ridhiwani amwangukia Majaliwa

Image
MBUNGE wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete (CCM), amemwangukia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kwa kumuomba amsaidie kutatua changamoto ya maji inayowakabili kwa muda mrefu wananchi wa jimboni kwake. Ridhiwani alitoa ombi hilo juzi katika ziara ya Waziri Mkuu Majaliwa aliyoifanya jimboni humo kwa lengo la kutembelea chanzo cha maji kilichopo Mto Wami, kama sehemu ya kukagua utekelezaji wa mradi wa maji wa awamu ya tatu wa Wami-Chalinze. “Changamoto ya upatikanaji wa maji jimboni Chalinze, bado ni kubwa na inahitaji nguvu ya ziada ili kufikia malengo ya kuhakikisha wananchi wanapata maji kama ilivyokusudiwa na Serikali. “Suala la maji kwa Jimbo la Chalinze, imekuwa kama sehemu ya siasa na si huduma kwa kuwa tangu mradi wa awamu ya kwanza wa Wami –Chalinze uanze kutekelezwa, ni vijiji 20 tu vya mwanzo ndivyo vilivyopata maji. “Ieleweke kwamba, Mkoa wa Pwani ni mkoa ambao unakua kwa kasi na una viwanda vingi. Hivyo basi, mahitaji ya maji ni makubwa zaidi ukilinganisha na

Mjane mwingine aibukia wanahabari na Zigo la nyaraka

Image
Mjane Farida Saleh Amrani amejitokeza mbele ya vyombo vya habari na kulalamika kudhulumiwa nyumba yake aliyoachiwa na marehemu mme wake aliyefariki mwaka 2011. Akizungumza na kuonesha hati halali za nyumba hiyo yenye kitalu namba 2111 iliyopo Mbezi Beach Kata ya Maliasili, Farida alisema kuwa katika nyumba hiyo walihamia mwaka 2002 na hati ya nyumba hiyo ilikuwa kwa mwanasheria kipindi chote hata pale marehemu mumewe alipofariki. Amesema kuwa, baada ya mume wake kufariki mtoto wa marehemu mkubwa aliambiwa afungue mirathi lakini akawa anasema taratibu za kabila la kihaya ni baada ya mwaka mmoja kumalizika. Farida ameeleza kuwa, mumewe Alfred Kyoma alifariki akiwa safarini Bukoba na amemuacha na watoto wawili ambao baada ya kumalizika kwa msiba familia nzima walikubaliana nyumba ipangishwe ili fedha zitakazopatikana ziwasomeshe watoto,ambao mmoja yupo kidato cha tano sasa hivi na mwingine cha kwanza. Nyumba hiyo kwa Yusuph Shaban Omari ambaye ni mmiliki

Mh! kwa Nape Hapana!- UWOYA

Image
IRENE Uwoya amekataa katakata kuzungumzia chochote kuhusiana na kutumbuliwa kwa aliyekuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye na kusema chochote ambacho kipo, kiendelee kubaki hivyo hivyo lakini kwa upande wake ameziba mdomo. Gazeti hili lilikuwa likimtaka Uwoya kuzungumzia kuachwa kwa waziri huyo katika mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri yaliyofanywa hivi karibuni na Rais Dk. John Pombe Magufuli na nini mtazamo wake kwa waziri mteule, Harrison Mwakyembe, lakini muigizaji huyo alikataa katakata. “Jamani mimi kwenye hilo sitaki kuzungumzia chochote jamani mambo ya siasa mimi hapana kwa sasa kilichopo ndicho kiendelee hivyohivyo,” alisema Uwoya.

Dkt Mwele Aliyetumbuliwa na JPM, achukuliwa umoja wa mataifa

Image
Dkt. Mwele Malecela aliyekuwa Mwanamke wa kwanza kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NIMR na kisha 'kutumbuliwa' baada ya kutangaza uwepo wa homa ya Zika nchini, sasa anakuwa Mkurugenzi wa Vituo vya kuzuia na kudhibiti magonjwa Afrika wa Umoja wa Mataifa (WHO-AfRO) Mwele alipata kuwa mwanamke wa kwanza kuongoza Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu(NIMR), baadae uteuzi wake ulitenguliwa.

KAIRUKI: SERIKALI HAITAMVUMILIA MTUMISHI MWENYE VYETI FEKI

Image
Inakadiriwa kuwa watumishi 4,300 wapya wanataajiriwa kuajiriwa katika kada ya elimu na wasanifu wa maabara ambapo ajira hizo mpya zinakuja baada ya kukamilika kwa zoezi zima la kuhakiki watumishi hewa.Hayo yamebainishwa mkoani Tabora na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma Mh. Angela Kairuki, wakati akizungumza na watumishi na wanachuo, ambapo amesema kwa muda mwingi taifa limekuwa likikabiliwa na changamoto ya watumishi hewa huku likipoteza fedha nyingi.Aidha Mhe. Kairuki amesema kuwa kamwe serikali haitamvumilia mtumishi ambaye atabainika kuwa na vyeti feki, huku akiwataka watanzania kutambua madhara ya vyeti hivyo kuwa ni kutopatikana kwa huduma stahiki.Amewataka wahitimu katika kada mbali mbali kutowaonea haya watu ambao wanataka kupora ajira za wenzao.

RAIS MAGUFULI: OLE WAKE ATAKAYEIZUIA KAMATI YA KUCHUNGUZA MCHANGA WA DHAHABU

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli jana tarehe 01 Aprili, 2017 aliwaapisha wajumbe wa kamati maalum ya kuchunguza kiwango na aina ya madini yaliyomo kwenye mchanga wenye madini ulio ndani ya makontena yaliyopo katika maeneo mbalimbali hapa nchini. Hafla ya kiapo kwa wajumbe wa kamati hiyo imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Mcheche Masaju, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi John Kijazi, Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Harold Nsekela na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama. Kamati hiyo ya wanasayansi 8 walioteuliwa na Mhe. Rais Magufuli tarehe 29 Machi, 2017 inaongozwa na Mwenyekiti wake Prof. Abdulkarim Hamis Mruma na itafanya kazi ya uchunguzi kwa siku 20 kisha kuwasilisha ripoti yake kwa Mhe. Rais. Akizungumza baada ya kuwaapisha, Mhe. Rais Magufuli amesema ameamua kuunda kamati hiyo yenye wasomi waliobobea katika

RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AMPOKEA WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA ALIYEWASILI MCHANA HUU JIJINI DAR

Image
Waziri Mkuu wa Ethiopia ,Hailemariam Dessalegn akishuka kwenye ndege mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere mapema leo mchana,na baadae kupokelewa na mwenyeji wake Rais Dkt John Pombe Magufuli,Waziri Mkuu Kassim Majliwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa. Imeelezwa kuwa ujio wa Waziri huyo Mkuu wa Ethiopia ni pamoja na kukuza mahusiano mazuri yaliyopo baina ya Tanzania na Ethiopia pamoja ‎na kujadili fursa zaidi za ushirikiano katika maeneo mbalimbali ikiwemo uwekezaji na biashara.Mhe. Dessalegn atakutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa mazungumzo na kushuhudia uwekwaji saini wa mikataba ya ushirikiano kwenye maeneo mbalimbali kabla ya kuzungumza na Waandishi wa Habari. Rais Dkt John Pombe Magufuli akimpokea mgeni wake ,Waziri Mkuu wa Ethiopia ,Hailemariam Dessalegn,aliyewasili hivi punde katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,jijini Dar Es Salaam.   Waziri

HIVI NDIVYO "BOMBARDIER" ZA ATCL ZILIVYOKUSANYA BILIONI 9 KWA MIEZI MINNE TU

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la ATCL, Bw. Lasislaus Matindi anasema wamefanikiwa kukusanya Shilingi Bilioni 9 kwa Miezi minne tu kwa kutumia ndege hizo mbili zilizonunuliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, nakuleta utata mkubwa na wapinzani wa siasa nchini waliodai kuwa hazikuwa na tija kwa Taifa.  Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) ilianzishwa mwezi Novemba 2002 baada ya Serikali kubinafsisha lililokuwa Shirika la Ndege la Tanzania (Air Tanzania Corporation, ATC); katika Shirika hilo, Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) lilinunua hisa asilimia 49 ndani ya ATC. Hata hivyo ubia kati ya ATCL na SAA ulikabiliwa na matatizo ya kiuendeshaji na kulazimika kusitishwa mwezi Agosti 2006 na ATCL kurejeshwa tena Serikalini kwa asilimia 100. KUMBUKUMBU: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na maafisa na viongozi wengine mbalimbali akikata utepe kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa n

TANZIA: MBUNGE DKT. ELLY MARKO MACHA AFARIKI DUNIA

Image

KESI YA MALKIA WA MENO YA TEMBO KUSIKILIZWA TENA WIKI IJAYO

Image
Kesi inayomkabili raia wa China, Yang Feng Glan (66) maarufu kama Malkia wa tembo inayosikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam itaendelea kusikilizwa kuanzia Aprili 5 hadi 7, mwaka huu. Wakili wa Serikali, Elia Athanas alidai katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi, Huruma Shaidi kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kusikilizwa na kwamba mawakili wanaosikiliza kesi hiyo hawapo. Hata hivyo, Wakili wa utetezi, Hassan Kiangio alidai kuwa kesi hiyo imeahirishwa kwa mara ya pili tangu mshitakiwa Manase Philemon (39) kudai amepigwa na kuteswa wakati akichukuliwa maelezo yake, ambapo upande wa mashitaka ulitakiwa kuleta mashahidi ili kuthibitisha tuhuma hizo. Hatua ya upande wa mashitaka kuleta mashahidi ni kusikiliza kesi ndogo ndani ya kesi kubwa baada ya shahidi Sajenti Beatus (46) kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kudai kuwa aliandika maelezo ya mshitakiwa huyo na baadaye mshitakiwa kupinga kupokelewa kw

Utata waibuka malori ya mafuta yaliyoibwa Arusha

Image
Arusha. Utata waghubika kuibwa na kupatikana kwa magari mawili ya mafuta mali ya Kampuni ya Mount Meru. Taarifa za kuibwa kwa magari hayo mkoani Arusha yakiwa na mafuta aina ya dizeli lita 77, 000 na kupatikana siku ya pili yakiwa wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro zinaelekeza kuwa kamera maalumu za (CCTV) ziliondolewa sehemu yalipokuwa yameegeshwa magari hayo. Meneja Mkuu wa Kampuni ya Ulinzi ya Ultimate, Eliuta Mwanjawike alisema kampuni yao baada ya kupata taarifa ya kuibwa magari hayo na walinzi wake wawili, waliunda kamati ya uchunguzi iliyobaini upungufu ukiwapo wa tofauti ya taarifa kati ya meneja mkuu wa kampuni hiyo na mkurugenzi. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Yusuph Irembo alikiri kupata taarifa za magari hayo kuibwa na kudai kuwa wameamua kuyaondoa eneo la polisi. “Magari hayo tumemkabidhi mmiliki kwa sababu yalikuwa na mafuta mengi na tusingeweza kukaa nayo hapa ila kesi ikishafika mahakamani basi yataletwa hapa,” alisema Yusuph. Mkurugenz

BREAKING: Mahakama kuu yaamuru Mbunge wa Chadema aliyefungwa miezi 6 jela aachiwe huru

Image
Mahakama Kuu Dar es Salaam imetengua hukumu iliyotolewa na Mahakama ya W/Kilombero dhidi ya Mbunge Peter Lijualikali, amekutwa hana hatia. Mahakama Kuu kanda ya Dar ES Salaam imetengua hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Wilaya Kilombero dhidi ya Mbunge Peter Lijualikali baada ya kukubaliana na warufani kwamba hati ya mashtaka iliyomtia hatiani ilikuwa na upungufu. Uamuzi huo umetolewa leo mbele ya Jaji Ama- Isaria Munisi baada ya kupitia sababu za kupinga mbunge huyo kutiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miezi sita jela. Peter aliwakilishwa mahakamani na Wakili Tundu Lissu na Fred Kiwelo wakati Jamhuri ilikuwa ikiwakikishwa na Wakili wa Serikali, Faraja Nchimbi. Mshtakiwa mwingine aliyehukumiwa kifungo cha nje, Stephani Mgatta adhabu yake pia imetenguliwa. January 2017, Mahakama ya wilaya ya Kilombero ilimuhukumu kwenda jela miezi sita Mbunge wa jimbo la Kilombero, Peter Lijualikali (30) kwa kosa la kufanya fujo na kusababisha taharuki kati

Dakika 180 za Makonda Bungeni zilikuwa hivi...

Image
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda jana alihojiwa kwa saa tatu mfululizo na Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kwa tuhuma za kuingilia haki, uhuru na madaraka ya chombo hicho cha kutunga sheria. Makonda aliwasili Bungeni Dodoma majira ya saa nne asubuhi kuitikia wito wa Kamati hiyo uliotokana na Azimio la Bunge lililotolewa Februari 8 na kuhojiwa na kamati hiyo kwa muda wa saa tatu kuhusu tuhuma zinazomkabili. Katika kikao hicho, Bunge liliamua Makonda aitwe kujieleza kwenye Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga na Madaraka kwa tuhuma za kukashfu chombo hicho.Sambamba na uamuzi huo, pia Bunge liliagiza mbunge yeyote ambaye kwa namna yoyote anadhani amekashfiwa na Makonda, awasilishe malalamiko yake kwa Spika ili hatua zaidi zichukuliwe. Hatua ya kutaka Makonda aitwe mbele ya kamati hiyo, ilitokana na mwongozo uliotolewa na Mbunge wa Mkuranga(CCM), Abdallah Ulega, kwa Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge, aliyedai mkuu huyo wa mkoa

KIJANA WA KITANZNAIA ANAYEISHI UJERUMANI AJA NCHINI KUTOA MAFUNZO YA KUCHEZA

Image
Mtanzania Emanuel Houston akizungumza na waandushi wa habari kuhusiana na mafunzo ya kucheza yatakayoendeshwa nae hapo kesho chini ya Unleashed Academy, kushoto ni msanii na mratibu wa mafunzo hayo Bernad Paul 'Ben Pol' na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Unleashed  Academy Halila Mbowe. Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii. Watanzania wenye vipaji wametakiwa kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza na wamewataka wajitokeze kwa wingi katika mafunzo ya kucheza yatakayoendeshwa na Mtanzania Emanuel Houston anayeishi Nchini Ujerumani.Emanuel ameambatana na baba yake Luis Houston ambao wote wanaishi nchini Ujeruami na wataendesha mafunzo hayo kupitia taasisi ya Unleashead Academy iliyo chini ya Halila Mbowe.Akizungumza na waandishi wa habari, Emanuel amesema kuwa anafurahi kuja kuwafundisha vijana wa kitanzania namna ya kucheza na watapata fursa ya kumuuliza kitu chochote.Emanuel amesema kuwa, kuja kwake nchini Tanzania anategemea kuona vijana wengi kuja kujifunza

Watuhumiwa wa ugaidi waigomea mahakama

Image
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha leo imesikiliza malalamiko ya watuhumiwa 61 wanao kabiliwa na kosa la ugaidi, ambapo ni shauri lililofunguliwa mwaka 2014. Wakizungumza leo mahakamani hapo watuhumiwa hao wamesema kuwa leo ndiyo itakuwa mwisho wao kufika kwenye viwanja vya mahakama hiyo mpaka upande wa jamuhuri utakapo kamilisha upelelezi wao. Wamesema wamekuwa wakifika mahakamani kwa muda ambapo wengi wao familia zinateseka na kusambaratika sababu ya kukaa mahabusu kwa miaka minne kwa makosa ya kusingiziwa. Aidha wamesema wamekuwa wakipewa ahadi  hewa na mkuu wa upelelezi  kuwa angeshughulikia shauri hilo ndani ya miezi mitatu na kwamba suala la mahakama kushindwa kutekeleza wajibu wake  wa kikatiba linaleta ukakasi kwa wananchi. Hakimu Mfawidhi Nestory Baro wa mahakama hiyo amewataka watuhumiwa kuwa na subira wakati wakishughulikia shauri lao ambapo kesi itatajwa April 11 mwaka huu na amewataka kufika mahakamani siku hiyo bila kukosa wakati akifanya utaratibu

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA PROF PALAMAGAMBA KABUDI AWASILI OFISINI MJINI DODOMA

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof.Palamagamba Kabudi akipokea shada la maua kutoka kwa mtumishi Joyce Mtuma mara baada ya kuwasili Wizarani mjini Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof.Palamagamba Kabudi akiangaalia kadi ya Pongezi iliyoasiniwa na watumishi wa wizara mara baada ya kuwasili Wizarani mjini Dodoma WaziriwaKatibanaSheriaMhe. Prof.Palamagamba Kabudi akisalimiana naNaibu Katibu Mkuu Bw. Amon Mpanju mara baada ya kuwasili Wizarani mjini Dodoma Waziri wa Katiba na SheriaMhe. Prof.Palamagamba Kabudi akisalimiana na Jaji mfawidhi Kanda ya Dodoma Mhe. Mwanaisha Kwariko alipowasili Wizarani mjini Dodoma WaziriwaKatibanaSheriaMhe. Prof.PalamagambaKabudiakisikilizamaelezombalimbalialipokutananawatendajiwaWizaranaMahakamakatikaukumbiwamikutanoWizaranimjini Dodoma. ……………….. WaziriwaKatibanaSheriaProf.PalamagambaKabudiamewasilikatikaOfisizaMakaomakuuyaWizarazilizokondaniya Chuo Kikuu cha Dodoma nakulakiwanawatumishiwaWiza

SAKATA LA RC PAUL MAKONDA KUVAMIA CLOUDS LAVUKA MIPAKA YA TANZANIA

Image
Asasi za kiraia 33 barani Afrika zimelaani kitendo cha kuvamiwa kwa studio za televisheni ya Clouds na kulazimisha maudhui yasiyostahili yarushwe hewani. Tamko la asasi hizo limetolewa ikiwa ni siku chache baada ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, (THBUB), Jukwaa la Wahariri (TEF) na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kulaani kitendo hicho kinachodaiwa kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari. Asasi hizo zinazohusika na utawala bora, demokrasia, haki za binadamu na uhuru wa habari zilikutana hivi karibuni mjini Kampala nchini Uganda katika mkutano uliokuwa ukizungumzia uhuru wa kujieleza na kupata habari. Tanzania kwenye mkutano huo iliwakilishwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) , miongoni mwa mijadala iliyotawala ni kukemea vitisho na vitendo vya kunyanyasa waandishi. Pia, wajumbe katika mkutano huo waligusia mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri yaliyofanywa na Rais John Magufuli kwa kumtoa Nape Nnauye kwenye