HIVI NDIVYO "BOMBARDIER" ZA ATCL ZILIVYOKUSANYA BILIONI 9 KWA MIEZI MINNE TU
Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Ndege la ATCL, Bw. Lasislaus Matindi anasema
wamefanikiwa kukusanya Shilingi Bilioni 9 kwa Miezi minne tu kwa kutumia
ndege hizo mbili zilizonunuliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli,
nakuleta utata mkubwa na wapinzani wa siasa nchini waliodai kuwa
hazikuwa na tija kwa Taifa.
Kampuni
ya Ndege ya Tanzania (ATCL) ilianzishwa mwezi Novemba 2002 baada ya
Serikali kubinafsisha lililokuwa Shirika la Ndege la Tanzania (Air
Tanzania Corporation, ATC); katika Shirika hilo, Shirika la Ndege la
Afrika Kusini (SAA) lilinunua hisa asilimia 49 ndani ya ATC. Hata hivyo
ubia kati ya ATCL na SAA ulikabiliwa na matatizo ya kiuendeshaji na
kulazimika kusitishwa mwezi Agosti 2006 na ATCL kurejeshwa tena
Serikalini kwa asilimia 100.
KUMBUKUMBU:
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na maafisa
na viongozi wengine mbalimbali akikata utepe kuzindua rasmi ndege mbili
mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya
Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Dar es salaam Jumatano Septemba 28, 2016.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama
Janeth Magufuli pamoja na maafisa wengine waandamizi wakiwa kwenye ndege
mojawapo baada kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400
zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania
(ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam Jumatano
Septemba 28, 2016. PICHA NA IKULU.
Comments
Post a Comment