Utata waibuka malori ya mafuta yaliyoibwa Arusha



Arusha. Utata waghubika kuibwa na kupatikana kwa magari mawili ya mafuta mali ya Kampuni ya Mount Meru.

Taarifa za kuibwa kwa magari hayo mkoani Arusha yakiwa na mafuta aina ya dizeli lita 77, 000 na kupatikana siku ya pili yakiwa wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro zinaelekeza kuwa kamera maalumu za (CCTV) ziliondolewa sehemu yalipokuwa yameegeshwa magari hayo.

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Ulinzi ya Ultimate, Eliuta Mwanjawike alisema kampuni yao baada ya kupata taarifa ya kuibwa magari hayo na walinzi wake wawili, waliunda kamati ya uchunguzi iliyobaini upungufu ukiwapo wa tofauti ya taarifa kati ya meneja mkuu wa kampuni hiyo na mkurugenzi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Yusuph Irembo alikiri kupata taarifa za magari hayo kuibwa na kudai kuwa wameamua kuyaondoa eneo la polisi.

“Magari hayo tumemkabidhi mmiliki kwa sababu yalikuwa na mafuta mengi na tusingeweza kukaa nayo hapa ila kesi ikishafika mahakamani basi yataletwa hapa,” alisema Yusuph.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Mount Meru, Atuli Mittaal mwishoni mwa wiki iliyopita  alisema magari yake yaliibwa saa sita usiku yakiwa na mafuta na yalikutwa  yametelekezwa mkoani Kilimanjaro, huku walinzi wawili wa Kampuni ya Ulinzi ya Ultimate wakiwa hawajulikani walipo.

Comments

Popular posts from this blog