RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AMPOKEA WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA ALIYEWASILI MCHANA HUU JIJINI DAR

Waziri
Mkuu wa Ethiopia ,Hailemariam Dessalegn akishuka kwenye ndege mara
baada ya kuwasili katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere mapema
leo mchana,na baadae kupokelewa na mwenyeji wake Rais Dkt John Pombe
Magufuli,Waziri Mkuu Kassim Majliwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa.
Imeelezwa
kuwa ujio wa Waziri huyo Mkuu wa Ethiopia ni pamoja na kukuza mahusiano
mazuri yaliyopo baina ya Tanzania na Ethiopia pamoja na kujadili fursa
zaidi za ushirikiano katika maeneo mbalimbali ikiwemo uwekezaji na
biashara.Mhe. Dessalegn atakutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa mazungumzo na
kushuhudia uwekwaji saini wa mikataba ya ushirikiano kwenye maeneo
mbalimbali kabla ya kuzungumza na Waandishi wa Habari.
Rais
Dkt John Pombe Magufuli akimpokea mgeni wake ,Waziri Mkuu wa Ethiopia
,Hailemariam Dessalegn,aliyewasili hivi punde katika uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere,jijini Dar Es Salaam.

Comments
Post a Comment