Mh! kwa Nape Hapana!- UWOYA


IRENE Uwoya amekataa katakata kuzungumzia chochote kuhusiana na kutumbuliwa kwa aliyekuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye na kusema chochote ambacho kipo, kiendelee kubaki hivyo hivyo lakini kwa upande wake ameziba mdomo.
Gazeti hili lilikuwa likimtaka Uwoya kuzungumzia kuachwa kwa waziri huyo katika mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri yaliyofanywa hivi karibuni na Rais Dk. John Pombe Magufuli na nini mtazamo wake kwa waziri mteule, Harrison Mwakyembe, lakini muigizaji huyo alikataa katakata.
“Jamani mimi kwenye hilo sitaki kuzungumzia chochote jamani mambo ya siasa mimi hapana kwa sasa kilichopo ndicho kiendelee hivyohivyo,” alisema Uwoya.

Comments

Popular posts from this blog