KAIRUKI: SERIKALI HAITAMVUMILIA MTUMISHI MWENYE VYETI FEKI
Inakadiriwa
kuwa watumishi 4,300 wapya wanataajiriwa kuajiriwa katika kada ya elimu
na wasanifu wa maabara ambapo ajira hizo mpya zinakuja baada ya
kukamilika kwa zoezi zima la kuhakiki watumishi hewa.Hayo yamebainishwa
mkoani Tabora na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma Mh.
Angela Kairuki, wakati akizungumza na watumishi na wanachuo, ambapo
amesema kwa muda mwingi taifa limekuwa likikabiliwa na changamoto ya
watumishi hewa huku likipoteza fedha nyingi.Aidha Mhe. Kairuki amesema
kuwa kamwe serikali haitamvumilia mtumishi ambaye atabainika kuwa na
vyeti feki, huku akiwataka watanzania kutambua madhara ya vyeti hivyo
kuwa ni kutopatikana kwa huduma stahiki.Amewataka wahitimu katika kada
mbali mbali kutowaonea haya watu ambao wanataka kupora ajira za wenzao.
Comments
Post a Comment