Mjane mwingine aibukia wanahabari na Zigo la nyaraka
Mjane Farida Saleh Amrani amejitokeza mbele ya vyombo vya habari na
kulalamika kudhulumiwa nyumba yake aliyoachiwa na marehemu mme wake
aliyefariki mwaka 2011.
Akizungumza na kuonesha hati halali za nyumba hiyo yenye kitalu namba
2111 iliyopo Mbezi Beach Kata ya Maliasili, Farida alisema kuwa katika
nyumba hiyo walihamia mwaka 2002 na hati ya nyumba hiyo ilikuwa kwa
mwanasheria kipindi chote hata pale marehemu mumewe alipofariki.
Amesema kuwa, baada ya mume wake kufariki mtoto wa marehemu mkubwa
aliambiwa afungue mirathi lakini akawa anasema taratibu za kabila la
kihaya ni baada ya mwaka mmoja kumalizika.
Farida ameeleza kuwa, mumewe Alfred Kyoma alifariki akiwa safarini
Bukoba na amemuacha na watoto wawili ambao baada ya kumalizika kwa msiba
familia nzima walikubaliana nyumba ipangishwe ili fedha
zitakazopatikana ziwasomeshe watoto,ambao mmoja yupo kidato cha tano
sasa hivi na mwingine cha kwanza.
Nyumba hiyo kwa Yusuph Shaban Omari ambaye ni mmiliki wa Royal Village
Hotel iliyopo Temeke na ameuziwa na kaka wa marehemu lakini katika hati
ya mauzo ikidaiwa kuandikwa jina la Alfred Athanas Kyoma akishirikiana
na mtoto wa Marehemu.
Majirani wa nyumba hiyo Wamesema kuwa siku chache zilizopita waliona
watu wakivunja nyumba na kuingia ndani na kutoa vitu ndani vya mpangaji
anayekaa hapo ambaye alikuwa amesafiri.
Kwa sasa nyumba hiyo imewekwa mlinzi ambaye jitihada za kumwambia
afungue zilishindikana baada ya kugoma kuruhusu watu kuingia ndani,aidha
inadaiwa kuwa nyumba hiyo imeuzwa kwa kiasi cha shilingi milion sitini
(60).
Mjane Farida Saleh Amrani akizungumza na waandishi wa habari
akilalamika kudhulumiwa nyumba aliyoachiwa na mumewe aliyefariki 2011,
ambapo inadaiwa kuwa kaka wa marehemu alibadili hati ya nyumba na
kuiuza.
Hati halali iliyokuwa kwa mwanasheria ambapo marehemu alitoa maagizo ya
kupatiwa mkewe kama likitokea tatizo lolote akabidhiwe mkewe.
Muonekano wa nyumba husika,ambayo Mlinzi alikwemo ndani lakini alikataa kufungua geti
Baadhi ya Majirani wakijaribu kumwomba mlinzi afungue mlango ili waingie ndani
Comments
Post a Comment