Posts

Uwoya awawashia moto wanaomsakama kuhusu Dogo Janja

Image
Mwanamama wa tasnia ya filamu za Kibongo, Irene Uwoya amejikuta akiwaka baada ya kuhojiwa sababu za kutomposti mumewe, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii kama ilivyokuwa zamani. Akizungumza na Risasi Jumamosi, Uwoya ambaye inadaiwa kuwa hayuko sawa na mumewe huyo alidai kuwa siyo lazima kila mara atamposti kwani ana mambo mengi ya kuandika na atafanya hivyo endapo tu imebidi. “Siyo kila mara nitakuwa natumia kurasa zangu kumposti Dogo, nina mambo mengine ya kufanya pia, itakapobidi kufanya hivyo nitafanya,” alisema Uwoya akionekana kuna jambo haliko sawa.  Uwoya alihojiwa hayo baada ya kila mara kuonekana akiposti picha za kuwa ndani ya ndege ambapo wapo waliosema kuwa kwa sasa amekuwa akisafiri na kumuacha mumewe huyo peke yake. “Siyo kweli, mimi sisafiri mara kwa mara, zile ni picha tu nimewahi kusafiri mara moja nilipokua nikienda Mwanza kwenye Miss Lake Zone,” alisema Uwoya

Uwoya awawashia moto wanaomsakama kuhusu Dogo Janja

Image
Mwanamama wa tasnia ya filamu za Kibongo, Irene Uwoya amejikuta akiwaka baada ya kuhojiwa sababu za kutomposti mumewe, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii kama ilivyokuwa zamani. Akizungumza na Risasi Jumamosi, Uwoya ambaye inadaiwa kuwa hayuko sawa na mumewe huyo alidai kuwa siyo lazima kila mara atamposti kwani ana mambo mengi ya kuandika na atafanya hivyo endapo tu imebidi. “Siyo kila mara nitakuwa natumia kurasa zangu kumposti Dogo, nina mambo mengine ya kufanya pia, itakapobidi kufanya hivyo nitafanya,” alisema Uwoya akionekana kuna jambo haliko sawa.  Uwoya alihojiwa hayo baada ya kila mara kuonekana akiposti picha za kuwa ndani ya ndege ambapo wapo waliosema kuwa kwa sasa amekuwa akisafiri na kumuacha mumewe huyo peke yake. “Siyo kweli, mimi sisafiri mara kwa mara, zile ni picha tu nimewahi kusafiri mara moja nilipokua nikienda Mwanza kwenye Miss Lake Zone,” alisema Uwoya

JPM Apiga Marufuku Wamachinga Kunyanga’nya Bidhaa

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Njia panda ya Bugando mjini Mwanza wakati akiwa njiani kuelekea Chato mkoani Geita. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Sengerema mkoani Mwanza kuelekea Chato mkoani Geita. Rais Dkt. John Magufuli amewapiga marufuku viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza kuwanyang’anya bidhaa wafanyabiashara wadogo na badala yake amewaagiza viongozi wote nchini kujielekeza katika kutatua kero zinazowakabili wananchi. Dkt. Magufuli ametoa kauli hiyo leo Agosti 18, 2018 alipokuwa anasalimiana na wananchi waliokusanyika mjini Sengerema akiwa njiani kuelekea Chato Mkoani Geita kwa mapumziko, ambapo wananchi hao walidai halmashauri ya Wilaya hiyo imekuwa ikiwanyang’anya matunda aina ya nanasi wakulima na wafanyabiashara wanaouza matunda yao mjini hapo. “Nilishasema viongozi wote niliowateua mimi msishereheke

KIFO CHA MAJUTO… KILICHOMTOA FAHAMU TAUSI CHA JULIKANA

Image
S IRI ya muigizaji Tausi Mdegela, kuangua kilio kupita kiasi kwenye msiba wa nguli wa vichekesho Bongo, Amri Athuman ‘King Majuto’ wiki iliyopita imebainika kuwa msanii huyo alikuwa ni baba yake wa hiari aliyemfundisha sanaa ambayo sasa inamweka mjini. Akizungumza na Ijumaa wa Wikienda, Tausi alisema kuwa, Majuto alikuwa baba yake aliyemlea katika maadili mema na aliyetamani sana kumuona anafika mbali kisanaa kwani ndio aliyemfundisha na alikaa naye nyumbani kwake Tanga kwa muda mrefu kama mwanaye wa kumzaa. “Mimi hapa nalia kwa uchungu mkubwa naumia mno kumpoteza baba yangu aliyenilea katika kazi kwa sababu ni mtu ambaye alikuwa anataka kujua hali yangu kila mara na alipenda mno kuona maendeleo yangu kila siku kama mwanaye,” alisema Tausi. Akiendelea kuzungumza na gazeti hili kwa uchungu, Tausi alisema kuwa Mzee Majuto hata wakati anakaribia kufariki yeye alikuwa ametoka nje kidogo ya Jiji la Dar lakini alipigiwa simu na dairekta Leah Mwendamseke ‘Lamata’ na ku

RAIS MAGUFULI AFANYA MABADILIKO MADOGO YA WAKUU WA WILAYA NA WAKURUGENZI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 13 Agosti, 2018 amefanya uteuzi wa Mkuu wa Wilaya 1, Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji 41, na amewahamisha vituo vya kazi Mkuu wa Wilaya 1 na Wakurugenzi wa Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji 19. Taarifa iliyotolewa leo tarehe 13 Agosti, 2018 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Ikulu Jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa Mhe. Dkt. Magufuli amemteua Bi. Senyi Simon Ngaga kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mkoa wa Mwanza. Bi. Senyi Simon Ngaga amechukua nafasi ya Mhandisi Mtemi Msafiri Simeon ambaye amehamishwa kituo cha kazi na kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chato Mkoani Geita, baada ya Mkuu wa Wilaya ya Chato aliyeteuliwa hivi karibuni Kanali Patrick Norbert Songea kwenda kwenye mafunzo ya kijeshi nje ya nchi. Uteuzi wa Bi. Senyi Simon Ngaga unaanza leo tarehe 13 Agosti, 2018 na Wakuu wa Wilaya wote wawili wanatakiwa kuripoti katika vituo vyao

RAIS MAGUFULI APONGEZA JIMBO LA MBULU KUPATA ASKOFU MPYA

Image
Waziri wa Katiba na Sheria profesa Palamagamba Kabudi na Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti na viongozi mbalimbali wakifuatilia misa Takatifu ya kumweka wakfu Askofu wa Jimbo la Mbulu Anthony Lagwen. Askofu wa Jimbo la Mbulu Anthony Lagwen akiwekwa wakfu kuwa askofu wa Jimbo hilo mjini Mbulu Mkoani Manyara jana. Askofu wa Jimbo la Mbulu Anthony Lagwen akiwa kwenye kiti chake baada ya kusimikwa kushika nafasi hiyo mjini Mbulu Mkoani Manyara jana, kushoto ni Askofu Mkuu wa Jimbo kuu katoliki la Dar es salaam mhadhama Polycap Kardinali Pengo na Askofu mwandamizi Yuda Thadeus Ruwaichi. Waziri wa Katiba na Sheria profesa Palamagamba Kabudi akimkabidhi Askofu wa Jimbo Katoliki la Mbulu Anthony Lagwen, zawadi iliyotolewa na Rais John Pombe Joseph Magufuli baada ya Askofu huyo kusimikwa jana mjini Mbulu Mkoani Manyara. RAIS John Magufuli amewapongeza wananchi wa wilaya za Mbulu, Babati na Hanang’ mkoani Manyara na Karatu mkoani Arusha zin

WASANII WAJITOKEZA KUMUAGA MZEE MAJUTO

Image
Msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul maarufu kama Diamond Platnumz (mwenye kanzu nyeupe) akibeba jeneza la mwili wa aliyekuwa nguli wa filamu za uchekeshaji nchini, Amri Athumani ‘King Majuto’ baada ya kumalizika kwa shughuli ya kuuaga mwili wake iliyofanyika leo tarehe 9 Agosti, 2018 kwenye viwanja vya Karim Jee vilivyoko jijini Dar es Salaam. Msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul maarufu kama Diamond Platnumz akibeba jeneza la mwili wa aliyekuwa nguli wa filamu za uchekeshaji nchini, Amri Athumani ‘King Majuto’. Msanii wa Bongo Movie, Jacob Steven ‘JB’ akizungumza na wanahabari wakati wa shughuli ya kuuaga mwili wa marehemu Mzee Majuto.  Msanii wa Bongo Movie, Single Mtambalike (wa kulia) akizungumza na msanii mwenzake, Mzee Hashim Kambi (wa kushoto).

Rich Mavoko Ashinda Kesi Dhidi ya WCB

Image
EXCLUSIVE: Msanii Rich Mavoko ameshinda kesi ya kujiengua katika Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB). Kesi hiyo ilikuwa ikisikilizwa katika Ofisi za Baraza la Sanaa Tanzania ( Basata). Takribani miezi miwili iliyopita taarifa zilianza kusambaa kuwa Mavoko ametimuliwa WCB huku nyingine zikieleza kuwa amejiengua mwenyewe. Aidha, viongozi wa lebo hiyo hawajataka kuweka bayana kinachoendelea dhidi ya Mavoko ambapo hivi karibuni, Mmoja wa viongozi hao, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ hivi karibuni alikaririwa akisema wakati wa kuzungumzia jambo hilo haujawadia.

Spika Wa Bunge Apokea Barua Ya Kujiuzulu Kwa Mbunge Wa Monduli

Image
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai amepokea barua ya kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiuzulu Ubunge wa Jimbo la Monduli kutoka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Julius Kalanga.

Shamsa: Akinipenda Chidi Inatosha!

Image
Shamsa Ford STAA mwenye mvuto Bongo Muvi, Shamsa Ford amesema kuwa hata kama leo watu watamchukia kwa jinsi alivyo au kwa kuzungumza ukweli hawezi kuumia hata siku moja kwa sababu anaamini aliyempenda kwa dhati ambaye ni mumewe Chidi Mapenzi yupo, inatosha. Staa huyo alizungumza na gazeti hili la Amani baada ya watu wengi kumshambulia kwenye mitandao ya kijamii kutokana na kutokelezea na nguo fupi kwenye 40 ya mtoto wa Zamaradi, na kusema kuwa ni ngumu kumridhisha kila mtu kwenye maamuzi yako. “Mimi Mungu kanijalia maneno sijali kabisa na isitoshe Chidi akinipenda na akakubaliana na maamuzi yangu kwangu inatosha kabisa siwezi kumridhisha kila mtu,” alisema Shamsa.

MKUU WA WILAYA YA ARUMERU, JERRY MURO AFANYA ZIARA ARUSHA

Image
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhe. Jerry Muro akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Meru na Arusha.  MKUU wa Wilaya ya Arumeru, Mheshimiwa Jerry Muro jana tarehe 01 Agosti, 2018 alifanya ziara ya kikazi pamoja utambulisho kwa watumishi wa Halmashauri Mbili za Meru yenye kata 26 na Arusha  yenye kata 27 zilizo katika Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha. Akiwa katika halmashauri hizo, Mhe. Muro aliwataka watumishi kufanya kazi kwa kuzingatia mahitaji ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambayo ndio anasimamia Utekelezaji wake katika halmashauri zote mbili zenye kata 53.  Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhe. Jerry Muro akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Meru na Arusha.  Katika Ziara Hiyo, Mhe Muro aliambatana na Mkuu wa wilaya ya Monduli, Mhe Iddi Hassan Kimanta aliyekuwa akikaimu Wilaya ya Arumeru, pamoja na Katibu Tawala, Bwana Timotheo Mzava pamoja na baadhi ya viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya

Picha ya Gadner na Mwanae Yazua Gumzo Mitandaoni

Image
 Kuna picha  aliweka Gadner akiwa amerepost kutoka katika akaunti ya binti yake Karen ikiwa inaonyesha akiwa amemkumbatia mtoto wake  huku wakiwa wamelala kwenye kochi, na kwa jinsi wao walivyochukulia ilikuwa ni kama mapenzi ya baba na mtoto. Lakini baada ya picha hiyo kwenda katika mitandao ya kijamii ilileta gumzo na kusemewa maneno mengi sana huku wadau na baadhi ya mashabiki wakisema kuwa hayo sio maadili ya kitanzania hasa kwa baba na binti yake. Huku wengine wakimtuhumu sana gadner na kusema kuwa hawamuamini sana kutokana na ukweli kwamba amekuwa akitoka kimapezni na wasichana wenye umri kama wa binti yake , hivyo hiyo inaleta picha mbaya kwa mashabiki wanaomuona akiwa anafanya hivyo. ==>>Tazama baadhi ya maoni hapo chini

Mke wa Babu Tale: Nina wivu kwa mume wangu akitoka bila mimi lakini

Image
Wiki weekend iliyopita kwa mara ya kwanza meneja wa Diamond Babu Tale alitoka na mama watoto wake na kwenda kwenye arobaini ya mtoto wa Zamaradi iliyofanyika huko Bunju B. Bongo5 ilifanya mahojiano na mke wa Babu Tale na kumuuliza anajisikiaje pale anapomuona mume wake akipiga picha na warembo mbalimbali wakati akiwa kwenye shughuli zake za kikazi. “Wivu upo lakini unategemea upo kwa kiwango gani na wivu ukiuendekeza mtakwama,” alisema mama watoto huyo wa Tale. Kwa upande wa Babu Tale alidai kwa kuwa yupo kwenye tasnia ya burudani kwa muda mrefu amejifunza hawezi tembea na mke wake kila sehemu. “Leo sijaja kazini nimekuja kwenye shughuli ndio maana unaona niko na mke wangu,” alisema Babu Tale.

AUNT ACHOMOA NDOA NA IYOBO

Image
Aunt Ezekiel MUIGIZAJI wa kitambo kwenye tasnia ya filamu, Aunt Ezekiel, ambaye pia ni mzazi mwenzie na dansa maarufu wa Wasafi Classic Baby (WCB), Moses Iyobo, amesema kuwa hana mpango wa kufunga ndoa na dansa huyo japokuwa wameshakaa wote zaidi ya miaka mitatu kwani kikubwa wanachokiangalia ni kulea mtoto wao Cookie. Aunt Ezekiel akiwa na mzazi mwenzie na dansa maarufu wa Wasafi Classic Baby (WCB), Moses Iyobo Akizungumza na Amani, Aunt alisema kuwa siyo kwamba mtu akifunga ndoa ndiyo anaweza kuishi vizuri na mwanaume wake, bali ni kwamba anachojua kuishi vizuri ni sifa moja kubwa ya kuendelea kuwa pamoja ni kupeana heshima na kila mmoja kutambua anachokifanya. “Mimi sitaki hata kukuficha wala sijawahi kufikiria kufunga ndoa na Iyobo leo wala kesho kikubwa tunaishi vizuri na tunalea mtoto wetu ipasavyo hilo ndilo ninalolitaka na si vinginevyo kwani kuolewa siyo ishu kikubwa malezi ya mtoto tu,” alisema Aunt. STORI NA IMELDA MTEMA | GPL

BETHIDEI YA TIFFAH KUFURU

Image
DAR ES SALAAM: Maandalizi ya pati ya kuzaliwa (birthday) ya bintiye ambaye ndiye uzao wake wa kwanza, Latifah Nasibu ‘Tiffah Dangote’ (3), yamemfanya baba’ke ambaye ni staa wa muziki wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kutoa kiapo kizito kuwa itakuwa ni shughuli ya kufuru, Risasi Jumamosi linakupa exclussive. Agosti 6, mwaka huu, Tiffah atatimiza umri wa miaka mitatu tangu alipozaliwa Agosti 6, 2015, lakini sherehe hiyo imesogezwa mbele ambapo sasa itafanyika Agosti 17 hadi Agosti 20, mwaka huu. DIAMOND NA RISASI JUMAMOSI Akizungumza na Risasi Jumamosi juu ya pati hiyo ya Tiffah ya kutimiza umri wa miaka mitatu, Diamond alisema kuwa, yupo tayari kufilisika, lakini ahakikishe mwanaye huyo ana furaha kwa kumfanyia pati hiyo ambayo itakuwa ya kihistoria. “Nimepanga iwe sherehe kubwa sana, acha nifilisike, lakini mwanangu afurahi,” ndivyo alivyoanza Diamond kwenye mahojiano hayo maalum na Risasi Jumamosi na kuongeza: “Nipo tayari kutumia sehemu ya pesa za

TAGCO NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZAPONGEZWA KWA UTENDAJI

Image
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Bw. Chiza Marando akisisitiza kuhusu namna Halmashuri hiyo ilivyojipanga katika kuimarisha mawasiliano ya kikakati hasa kutangaza miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali. Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Bw. Chiza Marando akisisitiza jambo kwa ujumbe wa chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari MAELEZO wakati wa ziara ya ujumbe huo katika Halmashauri hiyo kukagua na kujionea jinsi maafisa Habari wanavyotekeleza jukumu la kuisemea  Serikali katika Mikoa na Halmashuri zao. Kiongozi wa Ujumbe wa Viongozi wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Gaudensia Simwanza akisisitiza jambo kwa  Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Bw. Chiza Marando wakati wa ziara ya ujumbe huo katika Halmashuri hiyo uliolenga kukagua na kuweka mikakati ya pamoja katika

WAZEE WA NITUMIE PESA KWA NAMBA HII’… WANASWA

Image
I RINGA: Yawezekana wewe ni kati ya watu ambao walishawahi kutumiwa meseji za kitapeli kutoka kwa watu hao (pichani) ambao huandika hivi; ‘ile pesa nitumie kwenye namba hii, jina litatokea…, simu yangu ina tatizo’. Kama jibu ni ndiyo basi habari ikufikie kwamba, watuhumiwa wengine wapatao saba wa utapeli huo hivi karibuni wamenaswa mkoani Iringa baada ya kuwaliza watu wengi kwa muda mrefu. Watu hao wamekuwa wakiwatumia watu meseji na kuwaelekeza kuwa watume pesa, mazingira ambayo baadhi huenda walikuwa na watu ambao ilikuwa wawatumie pesa hivyo hutuma na kujikuta wametuma kwa matapeli hao. POLISI WATANGAZA VITA Kufuatia kushamiri kwa utapeli huo katika mikoa mbalimbali, jeshi la polisi kupitia kwa makamanda wa mikoa hivi karibuni lilitangaza vita dhidi ya uhalifu huo na kufanikiwa kuwanasa baadhi ya watu huku tahadhari ikitolewa kwa wananchi kuwa makini wanapokumbana na meseji za aina hiyo. WALIONASWA IRINGA Mbali na wale 15 wa hivi karibuni waliokamatw

MWANAMKE KUKOSA MSISIMKO WA TENDO LA NDOA

Image
T ATIZO hili la mwanamke kukosa msisimko wa tendo la ndoa kitaalamu tunaita ‘Female Sexual arousal disorder’. Mwanamke akiwa na hali hii huwa hajihisi hamu wala haja ya kuhitaji tendo hilo na wakati mwingine huona kama usumbufu endapo atakuwa katika mahusiano. Mwanamke wa aina hii kama yupo mwenyewe au ‘single’ haoni umuhimu wa kuwa na mpenzi au mwenza na hasa kama anajimudu kiuchumi. Wapo baadhi ya wanawake wenye hali hii ambao hawana watoto au wengine wanamtoto mmoja au zaidi na aidha wameachana na wenza wao au wenza wao walishafariki. Msisimko hupatikana baada ya hamu ya tendo la kujamiiana kuwa juu ya kiwango na kusababisha mabadiliko mwilini na kusaidia mwili uwetayari kwa tendo. Hali ya msisimko kwa mwanamke haina tofauti na hali ya mwanaume kusimamisha uume wake. Mwanamke aliyepoteza msisimko huwa hajisikii chochote wakati wa ’ Romance’ au maandalizi ya tendo la ndoa, wengine huwa hawapati hamu na wengine hupata hamu kwa kiasi kidogo lakini hawapati mguso au

Diamond azuiwa na Basata kwenda kufanya shoo nje

Image
BARAZA la  Sanaa Tanzania (BASATA) leo limemzuia mwanamuziki, Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwenda kufanya shoo nje ya nchi akiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam  kwa sababu msanii huyo hakuwa na kibali. Kaimu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) Onesmo Mabuye alipokuwa akizungumza na TBC, kuhusiana na sintofahamu hiyo kuwa ni kutokana na msanii huyo kukosakibali cha Basata. BASATA wamesema kwa sasa hivi kuna utaratibu mpya ni kuwa msanii akitaka kwenda kufanya shoo nje ya nchi ni lazima apitie kwa BASATA wampe kibali na kisha akirudi pia anatakiwa kuripoti kwao BASATA wamesema kumzuia Diamond wanataka iwe fundisho kwa wasanii wengine ili wanapoenda nje ya nchi wafuate taratibu zilizowekwa.

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBULU AGAWA BAISKELI KWA WALEMAVU

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndg. Hudson Kamoga ametoa msaada wa baiskeli sita kwa ajili ya walemavu ili kuwasaidia katika maisha yao ya kila siku. Kamoga amewashukuru marafiki zake waliochangia katika kuboresha maisha na kuwasaidia wananchi wanyonge wanaoishi katika mazingira magumu. Kamoga amesema “Serikali hii inawajali wanyonge na sisi kama viongozi lazima pia tufikiri zaidi ya ukomo wa kazi zetu za kila siku katika kuwahudumia wananchi wa hali ya chini. Nafasi hii niliyopewa na Mungu kupitia kwa Mh. Rais Dr. John Pombe Magufuli ni kwa ajili ya kuwatumikia na kuwasaidia watanzania hasa wanyonge,Nafasi hii ni kwa ajili ya watu ninaotakiwa kuwatumikia na si kwa ajili yangu binafsi,ndio maana ya utumishi”alisema Kamoga. Baiskeli hizo zimetolewa na marafiki wa mkurugenzi huyo wanaotambua mchango wake katika kulitumikia taifa na kuwajali watu wanaoishi kwenye mazingira magumu, Wadau hao wameahidi kutoa vifaa vingine kila watakapokuwa