Marekani: FBI Aliyetambua Shamulio la Osama Afariki kwa Sumu
SHIRIKA la Uchunguzi la Marekani (FBI) limesema limempoteza mwanamama mmoja ambaye ni miongoni mwa waliotambua shambilizi la kigaidi la Septemba 11, 2001 lililofanywa na Osama BinLaden, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 48. Melissa S. Morrow alifariki juzi Alhamisi akiwa na miaka 48 kwa kansa ya ubongo huku ikielezwa kuwa, huenda kifo chake kilisababishwa na kuwekewa vitu vyenye sumu (kemikali). Mtaalam huyo wa uchunguzi, amefanya kazi ndani ya FBI kwa miaka 22, na wakati umauti unamfika alikuwa ana siku chache tangu ahamishiwe katika kituo kipya cha kazi, Kansas City. Taarifa ya FBI imeeleza kuwa, Morrow alikuwa amejitoa kwa kiasi kikubwa kulitumikia taifa lake kwa kuchunguza na kubaini ukweli wa shambulio la Spetemba 11, katika Makao Makuu ya Jeshi la Marekani, Pentagon,. Inadaiwa mama huyo baadaye alikutwa kwenye ghala lenye sumu mwaka 2013 jambo lilliloplekea kuzorota wa kwa fya yake licha ya kutibiwa kwa zaidi ya wiki 10 huku akikusanya taarif