BARAZA LA MITIHANI -NECTA LAFANYA MABADILIKO MTIHANI DARASA LA SABA
Wanafunzi wa darasa la saba ambao
watafanya mtihani mwaka huu watakutana na mabadiliko ya mfumo wa
utungaji wa mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi .
Mabadiliko hayo yamefanywa na Baraza la
Mitihani la Taifa (Necta) jana na kutangazwa na Katibu Mtendaji wa
baraza hilo, Dk Charles Msonde.
Ofisa Habari wa Necta, John Nchimbi
amesema mabadiliko hayo aliyatangaza Dk Msonde katika mkutano mkuu wa
tano wa maofisa elimu mkoa na wilaya unaofanyika Dodoma.
Nchimbi amesema katika muundo huo mpya
kila somo litakuwa na maswali 45, kati ya hayo, maswali 40 yatakuwa ya
kuchagua jibu sahihi na matano yasiyo ya kuchagua (yatakuwa ya
kujieleza/kuonyesha njia na jibu nk).
Amesema maswali 40 kila swali litakuwa
na alama moja na maswali matano kila swali litakuwa na alama mbili huku
majibu ya maswali 40 yatajibiwa kwenye OMR FORM na maswali matano
yatajibiwa kwenye karatasi maalum itakayoandaliwa.
Kutokana na muundo huo mpya, Necta
imetoa wito kwa walimu wakuu kuanza kuwapima wanafunzi kwa kutumia
mabadiliko hayo ili kuwajengea uzoefu.
Comments
Post a Comment