Waziri Shonza Kina Pretty Wapo Wengi, Bado Wanatamba!
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa, na Michezo, Juliana Shonza. .
KWAKO mheshimiwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa, na Michezo, Juliana Shonza. Habari na pole na majukumu yako ya kila siku.
Najua Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk John Pombe Magufuli ni ya kazi. Watendaji wake mpo bize naweza kusema kuliko awamu zote zilizotangulia.
Ukitaka kunijulia hali yangu, mimi ni mzima wa afya. Naendelea kupambana katika taaluma yangu ya uandishi wa habari. Mungu anasaidia bado tunaendelea kupambana na changamoto ya kuusuka uchumi wa nchi yetu.
Baada ya salamu hizo, moja kwa moja niende kwenye dhumuni la mimi kukuandikia barua hii leo. Mheshimiwa waziri, hivi karibuni niliona ulivyomchukulia hatua msanii Pretty Kind kutojishughulisha na shughuli za muziki katika kipindi cha miezi sita.
Nilifurahi kusikia hivyo maana nilijua kweli serikali ila dhamira njema ya kulinda maadili ya Mtanzania. Kuvaa nusu utupu si jambo jema na hakuna muungwana yeyote anayeweza kufurahia vitendo kama hivyo.
Pretty Kind.
Aliwataka watendaji wake wahakikishe wanasimamia maadili, ndivyo ambavyo wewe ulionesha mfano kwa kumfungia huyo huku wengine kama Gigy Money na Sanch ukiwaita ofisini kwako.
Kama hiyo haitoshi, siku chache baadaye nakumbua pia ulimfungia msanii Ibrahim Mussa R.O.M.A kwa kosa la kutoa wimbo ambao una lugha chafu.
Na ulifanya hivyo baada ya kumuita mara kadhaa na yeye kutotii wito wako, kwa hili pia nikupongeze maana hakuna mtu anayefurahia lugha chafu kwani nyimbo hizi, mbali na kuzisikiliza sisi watu wazima, wanasikiliza pia watoto.
Gigy Money.
Lakini pamoja na pongezi hizo, mheshimiwa waziri nikukumbushe tu tatizo hili la wasanii kuvaa nusu utupu bado lipo. Kina Pretty Kind bado wapo wengi tu. Sanch na Gigy Money ambao uliwaita, bado wanaendelea na matukio yao ya nusu utupu kama kawa!
Kuna mwingine anaitwa Agness Mmasi naye huyu ni balaa kwa picha za utupu. Siyo anapiga nusu, yeye ni kama anapiga utupu kabisa na kuposti kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Tukiishia kwa wale wachache itakuwa ni kama tumewatoa tu mhanga na pengine tukaonekana hatukuwa na dhamira ya kukomesha tatizo balSanchi.tumefanya kama ‘nguvu ya soda’.
Kwa kuwa wewe umeonesha dhahiri mwanzo mzuri, ni vyema zoezi hili likawa endelevu ili kukomesha kabisa vitendo hivi si tu katika video za wasanii bali hata kwenye mitandao ya kijamii. Tutafute muarobaini wa kweli kukomesha suala hili.
Ni matumaini yangu utalifanyia kazi suala hili, nikutakie majukumu mema!
Mimi ni ndugu yako;
Erick Evarist.
Comments
Post a Comment