MTOTO ALIYECHOMWA SINDANO KIMAKOSA NA MADAKTARI KICHWANI,CHAANZA KUOZA


Leo stori ninayokusogezea ni kuhusu matukio ya kutokuwa makini katika idara ya afya hasa kwa madaktari yanazidi kuzua wasiwasi kwa wananchi nchini Kenya, tukio lililotokea siku za hivi karibuni ni la mtoto kuchomwa dawa isiyofaa na kumfanya aanze kuoza kichwa.
Tukio hili limefanyika katika hospitali ya Malava General Hospital katika jimbo la Kakamega na linatokea huku kukiwa na kesi dhidi ya Madaktari wa hospital ya Kenyatta inaendelea baada ya Daktari kumfanyia upasuaji mgonjwa asiyestahili.
Mtoto huyo aliyejulikana kwa jina Clinton Luchivya alikuwa amepelekwa katika hospitali hiyo baada ya kuwa mgonjwa na madaktari kumchoma kichwani baada ya kukosa mshipa wa kumwekea dawa.

Kulingana na mama wa mtoto huyo, mwanae alikuwa na ugonjwa wa Malaria kabla ya kupokea matibabu katika hospitali hiyo. Alisema kuwa mwanae alikuwa ameanza kubadilika badilika kabla ya kufahamu kuwa kichwa chake kinaoza.

Comments

Popular posts from this blog