Marekani: FBI Aliyetambua Shamulio la Osama Afariki kwa Sumu
SHIRIKA la Uchunguzi la Marekani (FBI)
limesema limempoteza mwanamama mmoja ambaye ni miongoni mwa waliotambua
shambilizi la kigaidi la Septemba 11, 2001 lililofanywa na Osama
BinLaden, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 48.
Melissa S. Morrow alifariki juzi Alhamisi
akiwa na miaka 48 kwa kansa ya ubongo huku ikielezwa kuwa, huenda kifo
chake kilisababishwa na kuwekewa vitu vyenye sumu (kemikali).
Mtaalam huyo wa uchunguzi, amefanya kazi
ndani ya FBI kwa miaka 22, na wakati umauti unamfika alikuwa ana siku
chache tangu ahamishiwe katika kituo kipya cha kazi, Kansas City.
Taarifa ya FBI imeeleza kuwa, Morrow
alikuwa amejitoa kwa kiasi kikubwa kulitumikia taifa lake kwa kuchunguza
na kubaini ukweli wa shambulio la Spetemba 11, katika Makao Makuu ya
Jeshi la Marekani, Pentagon,.
Inadaiwa mama huyo baadaye alikutwa
kwenye ghala lenye sumu mwaka 2013 jambo lilliloplekea kuzorota wa kwa
fya yake licha ya kutibiwa kwa zaidi ya wiki 10 huku akikusanya taarifa
kuhusu shambuilio hilo lililotikisa dunia.
Morrow alijiunga na FBI mwaka 1995 na
mazishi yake yatafanyika Country Club Christian Church eneo la Kansas
City, Jumanne mchana.
Msiba huo umetokea ikiwa ni wiki moja tu
tangu kifo cha aliyekuwa kapteni kwenye kikosi cha uokoaji, Thomas
Phelan aliyewaokoa waathirika wa shambulio la September 11 ambaye naye
amefariki kwa Kansa akiwa na miaka 45 huko Lower Manhattan.
Thomas Phelan, March 16 ambapo naye anadaiwa kifo chake kimesababishwa na kuwekewa mvuke wa sumu huko Ground Zero.
Comments
Post a Comment