Mzee Mkapa Ataka Mjadala wa Kitaifa
RAIS Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamini William Mkapa amesema ipo haja ya kuitishwa mjadala wa kitaifa wa kujadili hali ya elimu nchini kufuatia shule za serikali kuendelea kufanya vibaya katika matokeo ya mitihani ya kitaifa.
Mkapa ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma amesema hayo mkoani Dodoma wakati wa tukio la kumuingiza kazini Makamu Mkuu mpya wa chuo kikuu hicho cha Dodoma Profesa Egid Mubofu na kumuaga Makamu Mkuu wa chuo hicho aliyemaliza muda wake Profesa Idrisa Kikula.
Mzee Mkapa amesema mjadala huo unatakiwa kuhusisha makundi yote ya jamii bila kujali kama ni ya sekta binafsi ama ya umma sambamba na watu wa kawaida siyo wasomi pekee ambapo kupitia njia hiyo anaamini suluhu ya kudumu itapatikana.
Hata hivyo, Serikali ya awamu ya nne inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli imefanya juhudi kubwa kuondoa ada kuanzia elimu ya msingi hadi kidato cha nne pamoja kuongeza madawati, nyumba za walimu, madarasa, vitabu, kulipa stahiki za walimu wanaoidai serikai huku ikiboresha maabara na majengo ya baadhi ya shule kongwe za serikali hapa nchini.
Comments
Post a Comment