Posts

Kauli ya Yanga Kuhusu Kuondoka kwa Niyonzima

Image
TAARIFA KWA UMMA ​ Yanga SC kupitia kwa Katibu Mkuu Boniface Mkwasa inapenda kuwajulisha wanachama, wapenzi na washabiki wa Yanga juu Mchezaji raia wa Rwanda Haruna Niyonzima ambaye amekua Mchezaji wetu kwa misimu 6 mfululizo katika kiwango cha juu. Hata hivyo Haruna Niyonzima bado ana mkataba mpaka mwezi Julai na Yanga Sc, lakini hatutaweza kuendelea kuwa nae kwa msimu ujao kwani hatukuweza kufikia mwafaka katika mazungumzo yetu na yeye licha ya timu yetu kuwa na nia za kuendelea nae kwa misimu miwili ijayo. Klabu inamtakia kila la kheri katika maisha yake na soka kwa ujumla. Imetolewa na Idara ya Habari na Maelezo Young Africans Sports club. 21-06-2017.

Hii ndio Sababu ya Wabunge wa Upinzani Kumsusia Spika Ndugai Futari

Image
WABUNGE wa kambi ya upinzani bungeni, jana waliamua kumsusia futari, Spika wa Bunge, Job Ndugai, Taarifa kutoka kiongozi mmoja mwandamizi kutoka ndani ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) zinasema, uamuzi wa wabunge hao kususia futari umetokana na madai kuwa Spika amekuwa akiendesha Bunge kwa upendeleo. Hoja ya kususia futari iliwasilisha kwenye kikao kilichofanyika jana kabla ya Bunge kukutana kupitisha bajeti. “Tulikutana jana na tukakubaliana kwa kauli moja kususia futari hiyo. Hatuwezi kushirikiana na watu wanaotubagua waziwazi,” ameeleza mbunge mmoja wa Ukawa aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina. Habari zinasema, mbali na mkakati huo, Ukawa umejipanga kukabiliana na serikali hasa kutokana na kauli kuwa “wabunge waliopinga bajeti wanyimwe fedha za maendeleo.”

Sherehe ya kula nyama ya mbwa Ilivyofanyika China

Image
Sherehe ya kula nyama ya mbwa iliogubikwa na utata katika mji wa Yullin nchini China imeanza licha ya ripoti za awali kwamba ilikuwa imepigwa marufuku mwaka huu. Sherehe hiyo hufanyika kila mwaka katika mkoa wa Guangxi. Mapema mwaka huu ,wanaharakati walidai kwamba wafanyibiashara waliagizwa na mamlaka kutouza nyama ya mbwa. Lakini wamiliki wa vibanda vinavyouza nyama hiyo waliambia BBC hawajasikia lolote kuhusu hatua hiyo kutoka kwa maafisa. Mnamo tarehe 15 mwezi Mei, maafisa wa mji walithibitisha kwamba hakuna marufuku yoyote. Siku ya Jumatano, ripoti kutoka Yullin zilisema kuwa mbwa waliokufa walionekana wakiwa wametundikwa katika ndoano za nyama katika vibanda ndani ya soko la Dongkou ambalo ndio kubwa mjini humo. Mwanaharakati mmoja aliambia BBC kwamba alikatazwa na maafisa wa polisi kuingia katika soko la Dashichang ambapo inaaminika mbwa walikuwa wanauzwa. Katika sherehe za miaka ya nyuma kumekuwa na mzozo kati ya wauzaji nyama ya ...

MSANII JINI KABULA ALAZWA MUHUIMBILI

Image
Staa wa filamu za Kibongo, Miriamu Jolwa ‘Jini Kabula’. Nasikitisha!  Staa wa filamu za Kibongo, Miriamu Jolwa ‘Jini Kabula’ anadaiwa kudata ‘kuchanganyikiwa’ na hivi sasa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako anapatiwa matibabu,  Risasi Mchanganyiko  limetonywa. Chanzo makini kilicho karibu na msanii huyo kililiambia  Risasi Mchanganyiko  kuwa mwanamama huyo alikuwa kwa rafiki yake ambaye pia ni msanii wa filamu, Esha Buheti kabla ya hali yake kuanza kubadilika na kuzungumza mambo yasiyoeleweka. “Jini Kabula amechanganyikiwa kabisa yaani, kwani alikuwa kwa rafiki yake huyo, ndipo alipoanzia kuumwa ikabidi ndugu zake wamchukue na kumpeleka Muhimbili ambako mpaka sasa anaendelea na matibabu. “Ukimuona anakutambua, lakini anayoyaongea hayaeleweki, ni kwamba amedata kabisa licha ya kwamba kama alikuwa anakufahamu awali hata sasa akikuona anakutambua, lakini ndiyo hivyo anaongea vitu mchanganyi-kochan-ganyiko, ...

Upinzani Wampeleka Spika Ndugai Mahakamani

Image
Wabunge Watatu Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo Chadema Wamemfungua Mashitaka Mahakama Kuu Ya Dodoma Kupinga Uamuzi Wa Bunge Kuwapa Adhabu Halima Mdee, Estar Bulaya Na John Mnyika . Mdee, Mnyika Na Bulaya Wawashitaki Spika Na Mwanasheria Mkuu Hakuna kanuni inayosema Spika anao owezo wa kumfungia Mbunge siku saba. Haipo, bali anaingiza kanuni zake mwenyewe kutoka kichwani mwake.

RC ANNA MGHWIRA AMKALIA KOONI FREEMAN MBOWE

Image
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amesema kuwa hatua zilizochukuliwa na Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gellasius Byakanwa za kuondoa miundombinu ya umwagiliaji katika shamba la Kilimanjaro Veggies si za kisiasa bali ni taratibu za kisheria za kulinda vyanzo vya maji. Mghwira alitoa kauli hiyo jana alipotembelea shamba hilo lililopo Kijiji cha Nshara ili kujionea hali ya uharibifu wa mazingira uliofanywa katika shamba hilo linalomilikiwa na Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe. “Sheria iko wazi, inasema tusifanye shughuli zozote za kibinadamu zenye madhara kwenye vyanzo vya maji ndani ya mita 60 kwa mujibu wa sheria na shughuli hii ina madhara makubwa kwa mazingira na hata kwa binadamu,” alisema Mghwira. “Shughuli hii nzuri na ni uwekezaji mkubwa. Ninavyofahamu kilimo cha strawberry kikishatema maji lazima yaende mahali hata kama unatumia umwagiliaji wa kisasa wa matone. Maji yanakuwa na madhara kwa binadamu wanayoyatumia.” Mghwira alisema k...

Rais Magufuli atuma rambirambi kifo cha Ali Yanga

Image
Rais John Magufuli ametuma rambirambi kwa familia, wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), uongozi wa Klabu ya Yanga na wanamichezo wote kwa jumla kutokana na kifo cha shabiki wa Klabu ya Yanga, Ali Mohamed maarufu Ali Yanga. Ali Yanga amefariki dunia jana (Jumanne), Juni 20 kwa ajali ya gari iliyotokea katika Kijiji cha Chipogolo wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma. Taarifa iliyotolewa leo (Jumatano) na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa imemkariri Rais Magufuli akisema atamkumbuka Ali Yanga kwa uzalendo na mchango wake wa kuhamasisha na kushabikia masuala mbalimbali ya kitaifa na hasa michezo, ikiwamo kuishabikia timu yake ya Yanga, timu ya soka ya Taifa, CCM  na shughuli za kiserikali kama vile Mwenge wa Uhuru na ziara za viongozi. “Nimeguswa sana na kifo cha Ali Yanga, nilikuwa naye wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na alitoa mchango mkubwa katika uhamasishaji wa wananchi kukipigia kura chama changu cha CCM, pia amekuwa ak...

WATOTO WA BOSI WA FREEMASON WAFUNGUKA HAYA BAADA YA KIFO CHA BABA YAO

Image
Takriban miezi miwili baada ya kifo cha aliyewahi kuwa Bosi wa Jamii ya Siri (Secret Society) ya Freemason kwa Afrika Mashariki, Jayantilial Andy Chande ‘Sir Chande’, aliyefariki dunia Aprili 7, mwaka huu, watoto wake wawili wamefunguka mazito juu ya jamii hiyo. Kabla ya kupata neno la watoto hao, kufuatia kifo cha Sir Andy, kumekuwa na maswali mengi juu ya nini kinaendelea kwenye jamii hiyo kwa sasa hivyo  Wikienda  lilijipa kazi ya kutafuta majibu ya maswali. NINI KINAENDELEA FREEMASON? Katika nusanusa yake,  Wikienda  lilifika kwenye Hekalu la Freemason lililopo Mtaa wa Sokoine, mkabala na Hoteli ya Hyatt Regency, The Kilimanjaro jijini Dar, jirani na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na kutaka kujua kinachoendelea kwa kujigeuza mhitaji wa kujiunga na jamii hiyo. Gazeti hili lilipofika mahali hapo mishale ya mchana, hakukuwa na pilikapilika nyingi zaidi ya mama ntilie aliyekuwa akisubiria wateja wa msosi. Baada ya kuona kimya, ‘pand...

Kabila Linalohusudu Vitambi Linalotembea Utupu

Image
B AADA ya wiki zaidi ya 20 kukuletea kabila la wala watu lililopo Papua New Guinea, leo tutaanza kukuleta kabila dogo nchini Ethiopia katika Bara la Afrika ambalo ni la ajabu kutokana na vitendo vyao visivyo vya kawaida katika jamii yetu. Naamini utafuatilia habari za kabila hilo kuanzia leo hadi nitakapofika tamati ambapo utakuwa umeelewa mila na desturi za baadhi ya makabila yaliyopo barani Afrika. Kabila hilo kama nilivyosema hapo juu, linaitwa Bodi ama hapa kwetu tungewaita Wabodi lakini pia huitwa Wame’en, jamaa hawa huishi katika Bonde la Omo Kusini mwa Ethiopia na baadhi ya wanaume hutembea uchi wa nyama; wanapofika sehemu zilizostaarabika hushangaza wengi. Kwenye bonde hilo hawapo peke yao kwani kuna makabila mengine mengi madogomadogo arobaini na tano lakini kwa mila na tabia wanafanana na Wabodi japokuwa hao wengine hawana tabia ya kipekee ya Wabodi ya kujinenepesha kwa sababu maalum kama tutakavyoona mbele. Arbore ni moja ya kabila linaloishi katika ...

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA RAIS MSTAAFU WA NIGERIA MHE. OLUSEGUN OBASANJO IKULU DAR ES SALAAM

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimlaki Rais Mstaafu wa Nigeria Mhe. Olusegun Obasanjo aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 20, 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na  Rais Mstaafu wa Nigeria Mhe. Olusegun Obasanjo aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 20, 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimsindikiza Rais Mstaafu wa Nigeria Mhe. Olusegun Obasanjo baada ya kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 20, 201 PICHA NA IKULU

Jaji Mwengine wa Mahakama kuu ajiuzulu

Image
Rais John Magufuli ameridhia ombi la  Kujiuzulu kuwa Jaji wa Mahakama kuu Nchini Mwenda Judith Malecela. Taarifa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu inasema Leo Juni 20, 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli ameridhia ombi hilo.

Urusi yatoa onyo kali dhidi ya Marekani

Image
Urusi imeonya kuwa itashambulia ndege za muungano unaoongozwa na Marekani nchini Syria iwapo ndege hizo zitapaa katika maeneo ambayo jeshi lake linahudumu. Hii ni baada ya ndege ya kivita ya Marekani kutungua ndege ya kivita ya serikali ya Syria. Muungano huo unaoongozwa na Marekani ulisema ndege yake moja  ilitungua ndege ya Syria aina ya Su-22 baada ya ndege hiyo kuwaangushia mabomu wapiganaji  waasi wanaoungwa mkono na Marekani katika mkoa wa Raqqa, Jumapili. Urusi, mshirika mkuu wa serikali ya Syria, imesema pia kwamba itakatiza mawasiliano yote na Marekani ambayo lengo lake huwa kuzuia ajali angani. Syria imeshutumu shambulio hilo la Marekani na kusema litasababisha "matokeo mabaya sana". "Ndege yoyote, ikiwa ni pamoja na ndege za kawaida na ndege zisizokuwa na rubani ambazo ni za muungano wa kimataifa unaohudumu magharibi mwa mto Euphrates, zitafuatiliwa na majeshi ya kukabiliana na ndege angani na ardhini na zitachukuliwa kama kitu kinacho...

Mganga aua, aondoka na kiganja cha mkono

Image
WATU watatu wamefikishwa mahakamani akiwemo mganga wa kienyeji kwa tuhuma za mauaji ya Elizabeth Charles (45), mkazi wa kijiji cha Tambalale kata ya Nsimbo wilayani hapa. Waliofikishwa mahakamani hapo ni Juma Idd(25), Tatu Juma (20) wote wakazi wa kijiji cha Tambalale pamoja na mganga wa kienyeji, Shida Mwanansimbila (54) mkazi wa kijiji cha Kipungulu kata ya puge wilayani Nzega. Mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi wilaya, Mengo Kamangala alidai mbele ya Hakimu mkazi mfawidhi, Ajali Milanzi kuwa Mei 25 mwaka huu majira ya saa 5:00 usiku katika kijiji cha Tambalale Tarafa ya Nsimbo wilaya hapa, washitakiwa wote kwa pamoja walimpiga kisha kumuua na kuondoka na kiganja chake cha mkono wa kulia. Alisema washitakiwa wote kwa pamoja walitenda kosa hilo kinyume na kifungu 196 kanuni ya adhabu sura ya 16 mapitio ya 2002 inayozuia kutenda makosa kama hayo. Hata hivyo, washitakiwa hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza shauri hilo...

Aliyetaka Kuingiza Simu Gerezani afahamika

Image
DAR ES SALAAM: Kijana mmoja, Ramadhan Nombo, mkazi wa Jiji la Dar jana amenaswa na askari magereza katika Gereza la Mahabusu la Keko akitaka kuingiza simu tano alizokuwa amezificha ndani ya mapande ya nyama yaliyorostiwa. Tukio hilo la ajabu limetokea jana baada ya Nomba kuwapelekea ndugu zake chakula. Kwa mujibu wa chanzo, Nombo alipanga kuingiza simu tano ambazo alizipachika kwenye mapande ya nyama iliyorostiwa kisha kuwapelekea ndugu zake walioko gerezani hapo.  Hata hivyo, haikufahamika alikuwa anawapelekea kwa sababu gani, na wafungwa wa kesi zipi. Mtandao huu ulimtafuta Ofisa Habari wa Jeshi la Magereza, ASP Lucas Mboje ili kuzungumzia tukio hilo ambapo alikiri kutokea na akaelekeza aonwe Mkuu wa Magereza wa Dar. Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam, DCP Augustine Mboje alipoulizwa alisema ni kweli kijana huyo amekamatwa. Kama akikutwa na hatia atakuwa amevunja Kifungu cha 86 (1) cha Sheria za Magereza sura ya 58 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002...

Kauli ya Kubenea Kuhusu Kukamatwa Kwa Meya wa Ubungo

Image
TAARIFA KWA UMMA* NIMEPOKEA kwa masikitiko makubwa taarifa kuwa Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Yakoub amekamatwa na jeshi la polisi kwa amri ya "wanaodai wako madarakani." Kukamatwa kwake kunatokana na hatua yake ya kumpokea Mwenyekiti wa Chadema, Kanda ya Pwani, waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye. Mhe. Sumaye alikuwa na ziara ya kikazi ya kukagua shughuli za Manispaa za Dar es Salaam ambazo ziko chini ya vyama vinavyounda umoja wa UKAWA. Napenda kuufahamisha umma kuwa amri; na au maelekezo yoyote yaliyotolewa iwe na polisi au mkuu wa mkoa ama wilaya juu ya kukamatwa kwa Meya ni batili na haikubariki. Hivyo basi, ni jukumu letu kuhakikisha kuwa tunapigana kufa na kupona kutetea haki za wananchi waliotuchagua na kuhakikisha Meya wetu anakuwa huru kwa gharama yoyote ile. Ninawaomba wanachama, viongozi na wananchi wa jimbo la Ubungo na Kanda ya Pwani kusimama nasi, pamoja na Meya wetu katika kipindi kigumu cha kudai demokrasia ya kweli ndani ...