Kauli ya Kubenea Kuhusu Kukamatwa Kwa Meya wa Ubungo


TAARIFA KWA UMMA*

NIMEPOKEA kwa masikitiko makubwa taarifa kuwa Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Yakoub amekamatwa na jeshi la polisi kwa amri ya "wanaodai wako madarakani."

Kukamatwa kwake kunatokana na hatua yake ya kumpokea Mwenyekiti wa Chadema, Kanda ya Pwani, waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye.

Mhe. Sumaye alikuwa na ziara ya kikazi ya kukagua shughuli za Manispaa za Dar es Salaam ambazo ziko chini ya vyama vinavyounda umoja wa UKAWA.

Napenda kuufahamisha umma kuwa amri; na au maelekezo yoyote yaliyotolewa iwe na polisi au mkuu wa mkoa ama wilaya juu ya kukamatwa kwa Meya ni batili na haikubariki.

Hivyo basi, ni jukumu letu kuhakikisha kuwa tunapigana kufa na kupona kutetea haki za wananchi waliotuchagua na kuhakikisha Meya wetu anakuwa huru kwa gharama yoyote ile.

Ninawaomba wanachama, viongozi na wananchi wa jimbo la Ubungo na Kanda ya Pwani kusimama nasi, pamoja na Meya wetu katika kipindi kigumu cha kudai demokrasia ya kweli ndani ya Nchi yetu.

Ninaahidi kuwa mstari wa mbele kutetea wananchi na kuhakikisha haki zao zinapatikana.

Ni jukumu letu sote kuhakikisha "udikteta ulioanza kuingia nchini taratibu," unatokomezwa.

Taifa hili siyo mali ya CCM. Ni letu sote.

*Saed Kubenea*
Mbunge wa Ubungo, M/M- Kanda ya Pwani.

Comments

Popular posts from this blog