Sherehe ya kula nyama ya mbwa Ilivyofanyika China
Sherehe ya kula nyama ya mbwa iliogubikwa na utata katika mji wa Yullin
nchini China imeanza licha ya ripoti za awali kwamba ilikuwa imepigwa
marufuku mwaka huu.
Sherehe hiyo hufanyika kila mwaka katika mkoa wa Guangxi.
Mapema mwaka huu ,wanaharakati walidai kwamba wafanyibiashara waliagizwa na mamlaka kutouza nyama ya mbwa.
Lakini wamiliki wa vibanda vinavyouza nyama hiyo waliambia BBC hawajasikia lolote kuhusu hatua hiyo kutoka kwa maafisa.
Mnamo tarehe 15 mwezi Mei, maafisa wa mji walithibitisha kwamba hakuna marufuku yoyote.
Siku ya Jumatano, ripoti kutoka Yullin zilisema kuwa mbwa waliokufa
walionekana wakiwa wametundikwa katika ndoano za nyama katika vibanda
ndani ya soko la Dongkou ambalo ndio kubwa mjini humo.
Mwanaharakati mmoja aliambia BBC kwamba alikatazwa na maafisa wa polisi
kuingia katika soko la Dashichang ambapo inaaminika mbwa walikuwa
wanauzwa.
Katika sherehe za miaka ya nyuma kumekuwa na mzozo kati ya wauzaji nyama
ya mbwa na wanaharakati waliojaribu kuwaokoa mbwa waliopangiwa
kuchinjwa.
Comments
Post a Comment