Aliyetaka Kuingiza Simu Gerezani afahamika
Kwa mujibu wa chanzo, Nombo alipanga kuingiza simu tano ambazo alizipachika kwenye mapande ya nyama iliyorostiwa kisha kuwapelekea ndugu zake walioko gerezani hapo. Hata hivyo, haikufahamika alikuwa anawapelekea kwa sababu gani, na wafungwa wa kesi zipi.
Mtandao huu ulimtafuta Ofisa Habari wa Jeshi la Magereza, ASP Lucas Mboje ili kuzungumzia tukio hilo ambapo alikiri kutokea na akaelekeza aonwe Mkuu wa Magereza wa Dar.
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam, DCP Augustine Mboje alipoulizwa alisema ni kweli kijana huyo amekamatwa.
Kama akikutwa na hatia atakuwa amevunja Kifungu cha 86 (1) cha Sheria za Magereza sura ya 58 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002, inakataza kwa mtu yeyote kuingiza kitu chochote kisichoruhusiwa gerezani na atahukumiwa kifungo kisichozidi miezi sita(6) au faini au vyote kwa pamoja.
Hadi sasa Nombo anashikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Comments
Post a Comment