MSANII JINI KABULA ALAZWA MUHUIMBILI
Nasikitisha! Staa
wa filamu za Kibongo, Miriamu Jolwa ‘Jini Kabula’ anadaiwa kudata
‘kuchanganyikiwa’ na hivi sasa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili ambako anapatiwa matibabu, Risasi Mchanganyiko limetonywa.
Chanzo makini kilicho karibu na msanii huyo kililiambia Risasi Mchanganyiko kuwa
mwanamama huyo alikuwa kwa rafiki yake ambaye pia ni msanii wa filamu,
Esha Buheti kabla ya hali yake kuanza kubadilika na kuzungumza mambo
yasiyoeleweka.
“Jini
Kabula amechanganyikiwa kabisa yaani, kwani alikuwa kwa rafiki yake
huyo, ndipo alipoanzia kuumwa ikabidi ndugu zake wamchukue na kumpeleka
Muhimbili ambako mpaka sasa anaendelea na matibabu.
“Ukimuona
anakutambua, lakini anayoyaongea hayaeleweki, ni kwamba amedata kabisa
licha ya kwamba kama alikuwa anakufahamu awali hata sasa akikuona
anakutambua, lakini ndiyo hivyo anaongea vitu mchanganyi-kochan-ganyiko,
ukweli anatia huruma sana,” kilisema chanzo hicho.
RISASI LAMSAKA MZAZI MWENZAKE CHUZ!
Ili kuujua ukweli na kujiridhisha zaidi, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta
mzazi mwenzake, ambaye pia ni msanii wa filamu, Tuesday Kihangala
‘Chuz’ na kutaka kujua hali ya mwenzake, ambako mkali huyo wa tamthiliya
ya Closed Chapter, alikiri Jini Kabula kuugua.
“Nilipata
taarifa za Kabula kwamba anaumwa na alikuwa kwa rafiki yake, lakini
ndugu zake walimchukua na baadaye kupelekwa Muhimbili ambapo mpaka sasa
anaendelea na matibabu, nimeambiwa anaongea vitu ambavyo havieleweki,”
alisema Chuz.
Ili kupata ukweli zaidi, Risasi Mchanganyiko halikuchoka
na safari hii lilimtafuta rafiki wa muda mrefu wa muigizaji huyo ambaye
pia ni msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya akiwa na Kundi la Scorpion,
Esha Buheti, ambaye naye alikiri shoga yake kupata matatizo.
Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ na Kocha wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm.
“Ni
kweli anaumwa, niliwasiliana na ndugu zake wakaja kumchukua kumpeleka
Muhimbili, siwezi kusema hasa nini tatizo, lakini anaonekana hayuko
sawa, maana kuna maneno anayaongea ambayo si ya kawaida.
“Kuna
wakati tukaona tumpeleke kanisani kwa ajili ya maombi, tukaenda pale
Kawe akaombewa, lakini hakukuwa na mabadiliko yoyote, ndiyo maana
tukawaomba ndugu zake wampeleke hospitali,” alisema Esha.
Alipoulizwa kama ameshakwenda kumtembelea tangu aende huko, alisema hajakwenda kwa vile hali yake ya afya siyo nzuri.
Naye
dada wa Jini Kabula aliyejitambulisha kwa jina la Dayness alithibitisha
kuwa mdogo wake huyo amelazwa katika chumba cha wagonjwa
waliochanganyikiwa kutokana na maleria kupanda kichwani na hali yake
bado siyo nzuri.
Comments
Post a Comment