Posts

TAZAMA PICHA ZA MWANAMAMA HUYU AMBAYE ANAMIMBA YA MIEZI NANE LAKINI AKIFANYA MAZOEZI YA HATARI

Image
Julia Sharpe is a mom of twins, a mechanical engineer, and competes in men's gymnastics. Impressive photos of her doing handstands, as well as gymnastic exercises on the rings and parallel bars while 7 months pregnant with twins have emerged and they are a must-see! Dear men, would you let your wives try this at home when they are this heavy? See more photos below...

MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA YA MAUAJI DHIDI YA MTOTO WAKE YATOKANAYO NA IMANI ZA KISHIRIKINA WILAYANI MAGU.

Image
TAREHE 13.06.2017 MAJIRA YA SAA 01:00HRS USIKU KATIKA KIJIJI CHA KISABO KATA YA BUJASHI TARAFA YA SANJO WILAYA YA MAGU MKOA WA MWANZA, NUNGHU MGETA, MIAKA 35, MSUKUMA, MKAZI WA KIJIJI CHA KISABO, ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA MAUAJI DHIDI YA MTOTO WAKE AITWAYE MISUNGWI NUNGHU MIAKA 06, MTOTO WA KIUME, AMBAPO INADAIWA KUWA ALIMUUA KWA KUMZIBA MDOMO NA PUA KWA MUDA MREFU HALI ILIYOPELEKEA MTOTO KUSHINDWA KUPUMUA NA BADAE KKUPOTEZA MAISHA, KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI. INADAIWA KUWA MTUHUMIWA ALIKUWA AKIISHI NA WATOTO WAKE MWENYEWE HAPO NYUMBANI KWAKE, KWANI TAYARI ALIKUWA AMETENGANA NA MKEWE KWA MUDA MREFU. INADAIWA KUWA BAADA YA MTUHUMIWA KUTELEKEZA MAUAJI HAYO ALIMCHUKUA MAREHEMU KISHA KWENDA KUMTUPA KWENYE DIMBWI LA MAJI LILILOPO MBALI NA NYUMBA YAKE ILI IONEKANE AMEKUFA MAJI. ASUBUHI WAKATI WANANCHI WANAPITA MAENEO HAYO NA KUONA MWILI WA MTOTO ALIYEPOTEZA MAISHA UKIELEA KWENYE MAJI WALIPATA MASHAKA KISHA WALITOA TAARIFA KWENYE KI

LADY JAY DEE AACHIPA PICHA ZA MJENGO WAKE MPYA

Image
Mambo yanazidi kumnyookea mkongwe wa muziki wa Bongo Flava, Lady Jaydee. Msani huyo ameonyesha picha za mjengo wake mpya wa kisasa alioujenga ambao upo maeneo ya Kimara Temboni jijini Dar es Salaam. Kupitia mtandao wa Instagram, mrembo huyo ameweka baadhi ya picha za jumba hilo na kuandika, “Jide Ville.” Mashabiki wameanza kujiuliza, je huo ndio mjengo ambao yatakuwa makazi mapya ya Jide na mpenzi wake Spicy kutoka Nigeria?

Kesi ya waziri Mstaafu Adam Malima, mapya yaibuka

Image
Upelelezi dhidi ya kesi ya kumshambulia askari polisi inayomkabili aliyekuwa Naibu Waziri wa fedha na mbunge wa Mkuranga, Adam Kigoma Malima umekamilika. Mwendesha Mashtaka, Wakili wa Serikali Esta Martin amemueleza Hakimu Mkazi, Godfrey Mwambapa wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa kesi hiyo jana ilikuja kwa kutajwa. "Mheshimiwa, kesi hii Leo(jana) imekuja kwa kutajwa lakini upelelezi umekamilika, tu naomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuja kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali (PH), alidai Martin. Hakimu Mwambapa aliiahirisha kesi hiyo kwa niaba ya Hakimu Mkazi Respecious Mwijage ambaye ndio amepangwa kusikiliza kesi hiyo kwa kuwa anaudhuru. "Hakimu aliyepangwa kusikiliza kesi hii anaudhuru, naiahirisha hadi Julai 10 itakapokuja kwa ajili ya kusomewa PH mbele ya Hakimu husika", alisema Hakimu Mwambapa Malima anashtakiwa pamoja na dereva wake Ramadhani Mohamed Kigwande anayekabiliwa na tuhuma za kujeruhi. Katika hati ya mashtaka ilidaiwa

Musukuma aitaka Serikali iwatie Mbaroni ,Ngeleja Chenge na Kafumu

Image
JOSEPH Musukuma  Mbunge  wa Geita Vijijini (CCM),, ameiomba serikali iwakamate Wabunge wote wa CCM  waliotajwa kwenye kashfa ya kusafirisha mchanga wa dhahabu, maarufu kama makinikia, nje ya nchi. Amesema wabunge hao William Ngeleja (Sengerema), Andrew Chenge (Bariadi Mashariki) na Dk. Dalali Kafumu (Igunga), wanapaswa kukamatwa kwa kuwa hawana kinga inayozuia serikali kuwatia nguvuni. Musukuma aliyasema hayo jana wakati akichangia mjadala wa Bajeti ya 2017/2018, ambapo alisema kwa muda mrefu serikali imekuwa ikipata wakati mgumu kwenye kashfa mbalimbali zilizotokana na wabunge hao ambao wako kwenye chama tawala. “Mheshimiwa Mwenyekiti, hao watu wanaotajwa tunao humu humu na hawana kinga. Kwa nini sasa wasikamatwe?" Alihoji Musukuma. "Kuna mwingine yuko humu baada ya kutajwa kaandika kwenye (mtandao wa kijamii wa) twitter kuwa hawezi kuhojiwa hadi atakapofikishwa mahakamani. "Sasa mtu ametuhumiwa halafu anatamba kwenye mitandao ya kijamii kana

Maneno ya Tundu Lissu juu ya ripoti ya pili ya kamati maalum ya uchunguzi wa madini

Image
For the Record: What Goes Around Comes Around!!! Leo wapinzani wa Serikali ya Magufuli tumesemwa sana na kutishiwa kushughulikiwa bungeni na nje ya Bunge. Kwa sababu hiyo, naomba niweke rekodi ya masuala haya sawa sawa. Mwezi Machi '97 Bunge lilipitisha Sheria 2 kwa siku moja kwa kutumia Hati ya Dharura. 1) Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbali mbali za Fedha ya '97 ilifuta au kupunguza kodi nyingi kwa ajili ya makampuni ya kigeni ya madini. 2) Sheria ya Uwekezaji Tanzania '97 iliwapa wawekezaji wa kigeni ulinzi mkubwa na manufaa mengi kama vile kuondosha nje fedha na faida yote wanayopata kwa uwekezaji wao nchini. Mwaka '98 Bunge lilipitisha Sheria ya Madini '98 ambayo ilitamka kwamba mwenye milki ya madini na fedha yote itokanayo na mauzo ya madini ni mwenye leseni ya kuchimba madini hayo. Sheria hizo tatu nimeziita 'Utatu Usio Mtakatifu' (Unholy Trinity) katika maandiko yangu mbali mbali, na nimezichambua sana tangu mwaka &

MO AKUBALI KUISAIDIA SIMBA MILLIONI 200

Image
Wachezaji muhimu wanataka kusepa Simba baada ya mikataba yao Kuisha Simba walimshirikisha tajiri Mohamed Dewji Kwa Ajili ya kuwasaidia kuwabakiza wachezaji hao mhimu. Kutokana na ripoti ya kocha wa Simba ameshauri waongezwe wachezaji sita wa kazi golikipa mmoja, beki watatu, Winga mmoja, na Mshambuliaji mmoja, Katika ripoti hiyo inatabainisha kuwa wachezaji ambao hawajaisaidia timu hata kwa asilimia 20 waachwe hata kwa kupelekwa Kwa mkopo. Pia ripoti ikasisitizia wachezaji mhimu wasiondoke kwenye timu kama mikataba imeisha waongezewe. Baada ya ripoti hiyo kukabidhiwa kamati ya utendaji ya kupelekwa Kwa kamati ya usajili chini ya Zacharia Hanspope ikajadiliwa na ikaonekana Mapendekezo ya Omog yatafuatwa Kwa asilimia zote tatizo likaja Kwa wachezaji mhimu ambao wanamaliza mikataba ikawa changamoto kubwa. Ndio kamati ikapeleka barua ya ombi Kwa tajiri kijana MO aweze kuwasaidia. Baada ya Mo kupokea barua hiyo aliwakubalia Simba Kwa Sharti moja tu fedha

Ngereja, Chenge, Kafumu wavunja ukimya

Image
VIGOGO waliotajwa katika ripoti ya pili ya kuchunguza makontena yenye mchanga wa madini (makinikia)  kuisababishia Serikali hasara ya matrilioni ya fedha kupitia sekta ya madini, walipokuwa wakihudumu katika nyadhifa zao serikalini wamevunja ukimya. Vigogo hao wamezungumzia ripoti hiyo ya pili iliyowasilishwa kwa Rais Dk. John Magufuli Ikulu Dar es Salaam jana, ambapo kamati husika ilichunguza hasara ambayo nchi imepata tangu 1998 usafirishaji wa mchanga wa dhahabu nje ya nchi ulipoanza. Mbunge wa Bariadi, Andrew Chenge (CCM), alipoulizwa maoni yake juu ya kutajwa na kamati hiyo, alisema hataki kuzungumza chochote juu ya ripoti hiyo, huku Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja (CCM), akisema sheria ya madini ya 2010 ingefuatwa, nchi isingekuwa hapa ilipo. Kwa upande wake Kamishna wa Madini wa zamani, Dk. Dalaly Kafumu, alisema kwa sasa  hawezi kuzungumza jambo lolote kwa kuwa ni yeye ni mmoja wa watuhumiwa waliotajwa kwenye ripoti hiyo. Chenge Baada ya kutok

DIAMOND PLATINUMS AFICHUA SIRI NZITO KUHUSU WEMA SEPETU KWENYE CHIBU PERFUME

Image
Msanii wa muziki, Diamond platnumz amefunguka kuuzungumzia mchango wa malkia wa filamu, Wema Sepetu kwenye perfume yake ya ‘Chibu Perfume’. Diamond amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM kuwa, yeye na Wema wanakutana na kuongea sana na wakati mwingine hushauriwa mambo mengi ya kibiashara na mwanadada huyo ambae alikuwa mpenzi wake .“Mimi na Wema labda watu hawajui sisi tunaongea sana wakati mwingine tunakutana tu sana lakini sio kwenye media. Tushakuwa kila mtu ana mahusiano yake tofauti yeye ana familia yake hata ukiangalia katika Perfume yangu lile neno THE SCENT YOU DESERVE alilitoa Wema” alisema Diamond. Muimbaji huyo kwasasa yupo kwenye mahusiano ya Zari na tayari wamefanikiwa kupata watoto wawili.

Alichosema Zitto Kabwe baada ya ripoti ya madini

Image
"Mwisho wa siku historia inaandikwa tu. Uzalendo ni kufanya jambo ambalo wengi hawakuelewi lakini wewe unajua Ni jambo sahihi na unakubali kutukanwa, kususubikwa, kusimangwa, kuzushiwa, nk. Unapambana tu. Mwisho wa siku waliokuita msaliti watakuita shujaa. Waliokuzomea wanashangilia. Wewe unafanya nini? Unakaa kimya kwani kwenye kukaa kimya pia kuna kusema kukubwa zaidi. Muhimu Nchi ifaidike.  Huko nyuma nilipata kusema, hata mungu akinichukua sasa unakwenda ukiwa umetabasamu kwani unakuwa umetimiza wajibu wako duniani. Kina Josina Umm Kulthum wataishi Kwa heshima inshallah" Ameandika Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Facebook mara baada ya ripoti ya pili ya mchanga wa madini kuwasilishwa

Pogba kutua Tanzania

Image
Klabu ya Everton inajiandaa kuja nchini Tanzania kwa ziara ya kujiandaa na msimu ujao wa ligi ambapo wakiwa hapa wtacheza na washindi wa kombe la Sports Pesa timu ya Gor Mahia kutoka nchini Kenya. Sasa Everton wanaweza kuja na Pogba nchini Tanzania kama dili lake la usajili kujiunga nao likikamilika kabla hawajaja Tanzania, tetesi zinasema Everton wanajaribu kumsajili Florentin Pogba kutoka katika klabu ya St Etienne. Taarifa kutoka nchini Ufaransa zinasema timu za Everton na Red Bull Leipzig zote zinapambana kumnunua mlinzi huyo wa kushoto mwenye umri wa miaka 26 lakini Everton wanapewa nafasi kubwa kwani Florent anatamani kucheza ligi moja na Paul Pogba. Katika msimu uliopita wa ligi mlinzi huyo amecheza michezo 17 tu na alishacheza dhidi ya Paul Pogba msimu uliopita katika michuano ya Europa na jarida la Jeune Afrique limeshatabiri kwamba Florent anaweza kuitosa Red Bull na kujiunga na Everton.

Serikali imezuia Passport za Chenge, Muhongo, Kafumu, Karamagi `

Image
Serikali imeagiza, Mawaziri, Wanasheria Wakuu wa Serikali na Manaibu wao, Wakurugenzi wa idara za mikataba, na Makamishna wa madini, wanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini na watumishi wengine wa Serikali na watu wote waliohusika katika kuingia mikataba ya uchimbaji madini, utoaji wa leseni za uchimbaji wa madini na kuongeza muda wa leseni, watumishi na wamiliki wa makampuni ya madini kuto toka nje ya mipaka ya Tanzania. Agizo hilo lilitolewa jana  na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba ambaye alisema kuwa, wote waliotajwa kuhusika katika kulisababishia taifa hasara kupitia sekta ya madini, hawaruhusiwi kutoka nje ya mipaka ya Tanzania isipokuwa kwa kibali maalum kutoka serikalini. “Naelekeza wote waliotajwa kuhusika hakuna kutoka nje ya mipaka ya nchi yetu isipokuwa kwa kibali maalum kutoka serikalini. Vyombo vitekeleze maagizo ya Rais kwa utimamu,” aliandika Waziri Nchemba kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii. Agizo hili limekuja ikiwa ni

ACACIA Wapinga Ripoti ya Kamati ya Pili ya Rais JPM Kuhusu Mchanga wa Madini

Image
12 Juni 2017 Mwitikio wa Acacia kwenye matokeo ya kamati ya pili ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli. Acacia imeona matokeo ya kushtua ya kamati ya pili ya Rais iliyowasilishwa kwa Rais wa Tanzania Mh. Dk John P. Magufuli leo asubuhi ambayo imeangalia nyanja za historia za kiuchumi na kisheria ya mauzo ya nje ya makanikia ya madini. Kamati ya Pili imetoa matokeo yake kwa kutumia matokeo ya Kamati ya Rais ya Kwanza, iliyotangazwa tarehe 24 Mei 2017, ambayo Acacia imeikanusha vikali. Kamati hiyo ilipata matokeo yake kwa kutumia sampuli ya kontena 44. Kwa mujibu wa data za zaidi ya miaka 20 tulizonazo ni vigumu kuoanisha matokeo yetu na yaliyokutwa na kamati, na kamati imetoa thamani ya juu kwa zaidi ya mara 10 kuliko thamani halisi ya makanikia Kamati ya Pili inadai kuwa Acacia imetangaza kiasi cha chini cha mapato kuliko inavyopata na kulipa kodi kidogo kuliko inavyostahili kwa miaka mingi na kuficha mabilioni ya dola ya Marekani. Na hivyo imefanya mapen

Spika Ndugai apigilia msumari Ripoti ya madini

Image
"Hakuna kitu kibaya kuwa katikati ya dhiki ambayo hukuistahili"-amesema Spika Ndugai baada ya kukabidhiwa ripoti ya pili ya kamati maalumu iliyoundwa na Rais Magufuli kuchunguza sakata la mchanga wa Madini Leo Ikulu Jijini Dar es salaam "Haya ni mambo ya ajabu, ni mikataba ya kijinga na ya hovyo, Mimi na wabunge wenzangu wote kuhakikisha sheria zote zitakazoletwa tutazitendea haki"- Alisema Spika Ndugai Hatua hiyo imefuata baada ya Mapendekezo ya kamati ya hiyo iliyotaka sheria za nishati Madini zifanyiwe marekebisho ya haraka, ambapo Rais Magufuli ametaka bunge lifanye haraka iwezekanavyo.

Kilichouzwa nje ni Madini, Sio mchanga

Image
  "Biashara ya uuzwaji wa Makinikia haikufanyika kwa ushindani na si kweli kwamba wanauza Makinikia, kinachouzwa ni madini." amesema Mwenyekiti wa Kamati ya kuchunguza mchanga wa madini, Profesa Nehemiah Osoro Prof. Osoro ameyasema hayo wakati akikabidhi ripoti ya kamati yake kwa Rais John Magufuli leo katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa gharama za shughuli za utafutaji na upembuzi madini nchini zimejumuishwa katika mauzo yake kwa kupunguza faida hivyo hawatozwi kodi. "Faida yote iliyopatikana katika uuzwaji wa dhahabu nje haikujumuishwa katika mahesabu ili kukwepa malipo ya mrabaha" alisema Prof. Osoro Ameongeza kuwa uchunguzi wa kamati yake umebaini kuwepo kwa utakatishwaji haramu wa fedha na faida kurudishwa kama mkopo kwa makampuni ya madini kitu ambacho ni kinyume cha taratibu.

KAMPUNI YA KUCHIMBA MADINI ACACIA ILIINGIA KINYEMELA NA HAINA KIBALI CHOCHOTE

Image
Taarifa ya pili ya wachumi na wanasheria iliyofanya uchunguzi wa madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga wa madini iliyoundwa na Rais Joseph Magufuli, imebaini kuwa kampuni ya ACACIA Mining Plc haina kibali na inafanya kazi kinyume cha sheria.Prof. Osoro amesema kwamba Kamati yake imebaini kuwa Acacia haina uhalali wa kufanya shughuli zake hapa nchini na imetenda makosa yakiwemo kujipatia mali kwa udanganyifu, uhujumu uchumi, jinai na kuitia hasara taifa.Aidha Kamati ya Prof. Osoro imebaini kwamba Makinikia yaliyouzwa nje ya nchi hayakuwa makinikia hasa, bali yalikuwa ni madini mbalimbali huku ikiongeza kwamba katika mikataba ya uuzwaji wa makinikia hayo, serikali haikuwa sehemu ya mikataba hiyo.Prof. Osoro ameongeza kwamba jumla ya mapato yote ambayo serikali imepoteza ni Tsh. trilion 68.6 sawa na bajeti ya miaka miwili ya nchi kodi ya mapato ambayo taifa imepoteza ni Tsh. tril 55.07, mrahaba tril 11, bandari tril 1.6. na kwamba jumla ya thamani ya madini

MTOTO WA MIAKA 12, MOHAMED ABDULLAH AIBUKA MSHINDI MASHINDANO YA KUHIFADHI QURAN BARANI AFRIKA

Image
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi , Mohammed Abdullah Aden (12) wa Somalia hundi ya shilingi milioni 15, 750,000/= mshindi wa kwaza wa mashindano ya 18 ya Afrika ya Kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Juni 11, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) MTOTO wa miaka 12 kutoka Somalia, Mohammed Abdullahi Aden ameibuka kidedea na kitita cha dola za Marekani 7,000 (sawa na sh. milioni 15.75) katika mashindano ya 18 ya Afrika ya kuhifadhi Quran kwenye kundi la washiriki wa juzuu 30.  Mohammed ambaye ni miongoni mwa washiriki wadogo zaidi wawili kuliko wote (mwenzake anatoka Burundi), amejishindia pia IPAD, cheti, kompyuta iliyotolewa na Balozi wa Kuwait, ahadi ya sh. milioni moja kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na ahadi ya kwenda nchi yoyote aitakayo kutoka kwa kampuni ya Sky Bus Travel Agency ya jijini Dar es Salaam.  Akizungumza na maelfu ya waumini na Watanzania waliofurika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar

Fundi Seremala Mbaroni kwa kuwabaka binti zake

Image
FUNDI Seremala, Japhet Lendiman (38) mkazi wa Daraja Mbili, anashikiliwa na Jeshi la Polisi, baada ya kubaka watoto wake wa kike wa darasa la sita na kidato cha kwanza. Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi ili kubaini kiini cha tatizo hilo ni nini na kufuatiwa na hatua ya kufikishwa mahakamani. Mtuhumiwa huyo anashikiliwa na Jeshi la polisi tangu Juni 6, mwaka huu na upelelezi unaendelea kubaini undani wa tukio hilo. Akimzungumzia mtuhumiwa huyo, mmoja wa majirani wa eneo hilo la Daraja Mbili (jina limehifadhiwa) alidai kuwa mzazi huyo amezoeleka kwa tabia hiyo mbaya mtaani kwao. Alidai kuwa mtuhumiwa huyo amezoea kubaka watoto wake mara kwa mara wakati mama yao akiwa kazini na kwamba Mei 28 majira ya saa 9:00 alasiri alimbaka tena mtoto wake (Jina tumelihifadhi) wa darasa la sita shule ya Msingi Daraja Mbili ndipo taarifa zilipoanza kuzagaa mtaani. “Siku hiyo ya tukio lililo

Zaidi ya wanafunzi 2000 watemwa kidato cha tano

Image
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi) George Simbachawene ametoa idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano na vyuo vya ufundi kwa mwaka 2017 huku jumla ya wanafunzi 2,999 wakiachwa. Simbachawene ametoa kauli hiyo leo mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa ufaulu kwa mwaka huu umeongezeka kwa asilimia 3.75 ukilinganisha na matokeo ya mwaka 2015. Waziri amedai kati ya wanafunzi 96,018 waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu ni wanafunzi 93,019 tu ndiyo waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi. Waziri Simbachawene amesema kuwa jumla ya watahiniwa wote waliofanya mtihani wa kidato cha nne kwa shule kwa mwaka 2016 ni 349,524 huku waliofanya mtihani wa kujitegemea ni 47,751 ambapo watahiniwa waliofanya mtihani wa shule waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60 ya watahiniwa waliofanya mtihani Tanzania Bara. Simbachawene alisema

Dalili za Madhara ya Tezi Dume

Image
Tezi dume ni ile hali ya chembe chembe za uhai katika tezi la kiume kukua bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili katika eneo linalozunguka mirija ya kupitisha haja ndogo( mkojo).Ugonjwa huu kwa sasa unaweza kuwapata vijana wa kiume kuanzia miaka 25 na kuendelea tofauti na awali ilikuwa miaka zaidi ya 50. Dalili za ugonjwa huu; Kwenda haja ndogo mara kwa Mara,hasa usiku. Haja ndogo Za ghafla zisizoweza kudhibitiwa. Mkojo unaotoka kwa udhaifu ama kwa kukatika katika . Damu kuchanganyikana na mkojo. Maumivu  yanaendelea kwenye maeneo ya mgongoni sehemu Za kiunoni,kwenye kinena au sehemu juu ya mapaja. Madhara yake: 1.Kupungua kwa uwezo kufanya tendo la ndoa.Pia kusikia maumivu wakati wa kufikia kilele Na kukosa amani au kuhangaika  wakati wa tendo la ndoa. 2.Uambukizo wa magonjwa kwenye kipofu 3.Uambukizo  mwenge njia ua mkojo au figo. Ndugu ugonjwa huu unaua hata wenye uwezo wa kifedha maana ni hatari sana chukua tahadhari sasa pia msaidie na mtu mwingine